Housegirl alipwe Mshahara wa elfu 80 hadi laki 3

Kumbe mwizi hiloooo...!
 
mimi sina u-corperative wowote! naongelea watu wanaofanya hivi! sawa kila mtu na mtazamo wake, si unajua eeh!
 
Hili suala ni mtambuka linapaswa kufanyiwa mchakato sana, sipingani na hoja ila modality ya utekelezaji ndo ikoje?.
Kuna baadhi ya familia dada wa kazi ni sehemu yao, analipwa labda 50K lakini anatibiwa, ananunuliwa mavazi, anapewa hela ya kusuka, anapewa hela ya vocha kwa kuwa simu yake inatumika kama ya nyumbani (ofisini kwake), anasaidiwa familia yake ikiwa na shida, akienda kwao anapewa nauli ya kwenda na kurudi na zawadi. Wengine wamesomeshwa ufundi, wameendelezwa kimasomo mpaka wengine wamewezeshwa mitaji wakajitegemea baada ya muda fulani.
Kwa hiyo lisiwe swala la uwana harakati tu.
 
Anajifurahisha huyu
Serikali yenyewe kima cha chini cha watumishi wake mia 3 sitini afu huyu anayelipwa 360 ndo amlipe mfanyakazi wa ndani 160 hiyo familia wanakula hewa?
 
Na ndivyo inavyotakiwa kuwa, utashangaa humu kuna waajiriwa ambao kutwa kuilalamikia serikali iwaongeze kima cha salary, wakati huo wao wanawalipa wafanyakazi wao wa ndani pesa ambayo kiuhalisia haitoshi hata kununua mifuko 5 ya simenti.

Hovyo kabisa, roho mbaya na ubinafsi wa watanzania ndio unaorudisha nyuma maendeleo ktk jamii, hivi kama unajiona huna pesa kwanini utoe ajira kwa mtu usiyemmudu mpaka mpigishane makelele?, na kuna watu hata kula yao shida lkn wanataka wawe na wafanyakazi ndani.

Kuna hawa ambao wanalipwa pesa nzuri kazini/ktk biashara zao lkn hawawalipi vizuri wafanyakazi wao, ndiomaana mnaibiwa waume wenu na wengine kutiliwa sumu/kuibiwa/kuchawiwa na kila aina ya matukio kisa ushenzi wenu wa kuwanyanyasa mabinti wa watu.

Kama mnaona rahisi kwanini msifanye wenyewe hizo kazi?, au kwanini msiwape ndugu zenu wazifanye?.

Kuna ulazima wa kudeal upya na sheria zitakazosaidia kuwalinda waajiriwa wote nchini bila ubaguzi.
 
Hili la wafanyakazi wa ndani wangeachana nalo, muhimu wahakikishe usalama wao upo vizuri. Waache wakubaliane wao na wanaowasaidia majukumu ya ndani
Ili muwanyonye mabinti wawatu?, hili ni jukumu la serikali kulinda maslahi ya kila raia, na kila mfanyakazi anatakiwa alipwe kiuhalali hailajishi uchumi wako uko vipi.

Kama unaona huna pesa za kuwalipa vzr mabinti wa kazi kwanini usizifanye mwenyewe?, au kwanini usiwape ndugu/watoto wako wazifanye bure, suala la ukoloni/utumwa tunalisema limekwisha lkn kiuhalisia bado linafanywa na watu wamehalalisha, kisa serikali haijatilia mkazo wa sheria zinazodhibiti ukiukwaji wa haki za kila mwananchi.

Acheni utapeli, lipeni vizuri mabinti, hizo 50k-100k mnazowapa hazitoshi hata kuanzia maisha wakirudi makwao, pesa ngumu sawa! Kwanini ukimbilie majukumu yaliyokuzidi?
 
Ukikaa na kutulia utaelewa nilichosema, nyumba hazifanani, na wanaokaa na hawa mabinti hawafanani vipato. Wengine wanataka watu wa kubaki nyumbani, hakuna kazi ngumu zaidi ya kufagia nyumba na kuosha vyombo. Serikali haitaweza kulisimamia hili zaidi ya kuleta vurugu.
 
Huko liliko kusuduwa ombi la mahausi girl na sie waajiri wao tumepeleka maombi yetu ili tuongezwe mishahara watuvumilie kidogo
 
Hapo saaa ni makubaliano yenu ninyi wawili, umlipe 100k ila kila kitu ajitegemee cha kwako ale chakula tu ila matumizi binafsi kama hizo losheni, pedi, sijui kisuka afanye mwenyewe. Wewe unakuwa unafanya mara mojamoja ukipata nafasi
Atakuwa mwizi balaa, kwenye mafuta ya mtoto, na vijisent vya dukani vikibaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…