Nimepata ushauri na nashukuru kwa wale wote walionipa ushauri wa kuachana na ex-girlfriend ambaye kwa sasa ni mke wa mtu (japo bado kinaniuma anavyoteswa). Lakini tatizo linalobaki ni kwamba mke wangu bado yupo. Kwa vile yeye anawahi kurudi job, nikifika wala hastuki - hanipokei mizigo! Nguo hajawahi kunifulia na kila kitu kama kunyoosha nguo zangu (na zake), kupika, kung'arisha viatu vyangu anafanya housegirl ambaye tumekaa nae miaka karibu 4.
Watu wengi wakimuona huwa wanamheshimu kuliko mke wangu kutokana na upole na urembo wake. Mke wangu ni kinara wa kuchonga maneno! Kila siku ni ugomvi tu na hana shukrani. Huyu HG, ni mzuri kuliko mke wangu. Nimemlea na anapendeza mtoto wa watu akipita anaita vilivyo. Naona ni vema mke wangu ampishe huyu housegirl. Naomba ushauri nifanyeje jamani maana housegirl anavyong'ara itaniuma akienda kwa mtu mwingine.