Wiyelelee
JF-Expert Member
- Nov 9, 2012
- 1,071
- 348
- Thread starter
- #121
Kusema ukweli siwezi kuunga mkono hili la my wife wako kumpisha HG! Sikushauri ingawa nimeshawahi kushuhudia haya yakitokea!
Lakini hebu wadada mliokwisha olewa tayari tuambieni tu! Shida ni nini? Kwa nini huwa mnabadilika sana? Kulikoni mnakabidhi (sio wote) majukumu yenu kwa wadada wasaidizi wa nyumbani? Chakula! Dada. Maji! Dada. Mkoba wa safari ama ofisini! Dada. Kufua na kupasi! Dada! Kulea dogo! Dada. Kudeki! Dada............and many more you can name! Huwa mnajisahau ama ni ugonjwa wenu? Halafu sikiliza anavyobwabwaja asubuhi tena kwa ukali utafikiri askari wa K.A.R!
Jirekebisheni!
You are so objective kwa vile umetazama pande zote. Mtu eti mkiwa wachumba anakazana kumbe linataka kuolewa tu na watu wale ubwabwa! Unamwingiza ndani anaanza kuleta za kuleta anasahau kila kitu. Sasa zigo kama hili la nini? Halafu cha ajabu mtu mwenyewe nae ni graduate ambae lazima awe muelewa. Mimi sivuti sigara wala sinywi na nina akili timamu, iweje mke anitese kiasi hiki?