Mkuu MAKEBO kwa heshima na taadhima,na kwa niaba ya wapenda elimu humu jukwaani nakumba sana utupe wewe majibu ya maswali haya uliyomuuliza huyo uliemjibu.
Nimeona Kuna kitu Cha kujifunza hapa ambacho ukweli nilikua sikijui,na natamani kulikua.
Na ikikupendeza unaweza kujibu hapahapa au unaweza kuanzisha thread yake maalumu,pia ukiongeza nyama na nyongeza ya vitu ambavyo naamini wengi hatuvijui.
Nitakushukuru ikiwa utanitag.
Natanguliza shukurani.
Karibu sana Mkuu
Nitajibu hapa hapa, kwakweli sina muda wa kuanzisha thread samahani
Wewe unajua funders wa Al Qaeda na Taleban miaka yote walikuwa wananchi wa nchi gani ?
Hili liko wazi hata serikali ya US inajua, na kuna kesi lukuki zimefunguliwa na wananchi wa US waliopoteza ndugu zao katika mashambulizi yaliyowahusisha Al Qaeda.
Familia za zaidi ya waathiriwa 600 Septemba 11 ziliwasilisha kesi ya dola trilioni 3 , zikiwatuhumu wanamfalme wa Saudi Arabia, benki za kigeni, mashirika ya kutoa misaada na serikali ya Saudi Arabia kwa kufadhili mtandao wa kigaidi ulioanzisha mashambulizi hayo.
Mwanamfalme mmoja wa Saudi Arabia aliyetajwa kama mshtakiwa, Sultan Bin Abdulaziz al Saud, amekuwa waziri wa ulinzi wa ufalme huo tangu 1963. Kesi hiyo ilinukuu lawama zake dhidi ya "ushawishi wa Kizayuni na Kiyahudi" wa Marekani baada ya Septemba 11 na kusema kwamba alikuwa amechangia dola milioni 6 tangu 1994 kwa mashirika ya Kiislamu yanayofadhili al Qaeda, huku pia akihudumu kama msimamizi mkuu wa serikali wa ukusanyaji wa fedha za hisani.
Mshtakiwa mwingine wa kifalme, Turki al-Faisal al Saud, alikuwa hadi mwaka mmoja uliopita mkuu wa shirika la ujasusi la Saudia, ambalo kesi hiyo ililielezea kama "mshikamano wa Osama bin Laden na mtandao wa mashirika ya kutoa misaada, taasisi na vyanzo vingine vya ufadhili." Jukumu la mkuu wa tatu aliyetajwa katika kesi hiyo, Mohammed al-Faisal al Saud.
Unajua Taleban ni washia au wasunni? na nani kawarudisha pale ?
Taleban ni wasunni walioazishwa na vikundi vya waarabu wa Saudia Arabia, UAE na Qatar,
Marekani kwa muda mrefu wamekuwa wakishutumu baadhi ya nchi - ikiwa ni pamoja na Pakistan, Iran na Urusi kwa kutoa msaada wa kifedha kwa Taliban. lakini hawana ushahidi wa hilo
Ila inajulikana sana ni , raia binafsi kutoka Pakistani na nchi kadhaa za Ghuba ikiwemo Saudi Arabia, Falme za Kiarabu na Qatar wanachukuliwa kuwa wachangiaji wakubwa zaidi wa kibinafsi, vyanzo hivi vya ufadhili vinadhaniwa kutoa sehemu kubwa ya mapato ya Taliban. Kulingana na wataalamu, inaweza kufikia dola milioni 500 kwa mwaka.
Abstract Studying Qatar’s relationship with illicit financing of terror, this paper seeks to understand the complicated relationship between Qatar’s counterterrorism efforts and the resultingimplications for United States foreign policy. The author argues that Qatar maintains a worryingly
www.iar-gwu.org
Al Qaeda wa Syria leo wanashika nchi, unajua kwanini Marekani na Israel wamekubali yaishe ?
Syria leo hii inaongozwa na Ahmed al-Sharaa, kumbuka huyu alikuwa kati ya makundi ya Al Qaed yalikuwa yakipigana vita nchini Syria na Iraq yaliyojulikana kama HTS Hayat Tahrir al-Sham na hapo zamani alikwa kingozi wa kundi la Al Nusra Front na pia allishawahi kufungwa na wamarekani katika gereza maarufu la Abu Ghraib nchini Iraq.
Leo hii kwa US kukubaliana na Raisi mpya wa Syria hakukuanza leo, tokea kuanzia mwaka wa 2015, mkurugenzi wa zamani wa CIA David Petraeus alipendekeza kwamba Marekani inapaswa kufikiria kufanya kazi na wanachama wa mtangulizi wa HTS, Jabhat al-Nusra, katika vita dhidi ya Islamic State (IS). Na ingawa HTS iliorodheshwa rasmi kama shirika la kigaidi na Marekani mnamo 2018.
Kitu kikubwa ambacho US anataka Syria mpaka kumkubali Al Sharaa ni kutaka kufugua kambi ya jeshi ya US mjini Damascus alipokuwepo Russia, ili aweze kukabiliana na Russia na Iran kwa karibu zaidi.
Na hii ilipata pingamizi kubwa kutoka Israel kwa US kumsapoti Al Sharaa.
Kwamba marekani aliuungana Russia kuzuia al qaeda, hivi unajua kwanini Russia alienda Syria ?
Russia hakwenda Syria kwa madhumuni ya kupigana na IS, alieenda kwa ajili ya kujitutumua kwa US baada ya Obama kusema atapeleka US kama Assad atatumia silaha za maangamizi, na baada ya Russia kuingia na pia kutumiwa kwa silaha za maangamizi dhidi ya waasi wake, US alipeleka vikosi vya kijajusi kimya kimya na walisha wahi kupigana vita kabisa na vikosi vya Wagner huko Syria mpaka Washington akaomba Russia wasimamishe mashambulizi.
Habari hii hapa
This battle became one of the rare occasions American and Russian combatants exchanged fire—one of the deadliest battles the Americans had faced in Syria.
thewarhorse.org
Unajua Bahrain ina washia wangapi kulinganisha wasunni na mpaka leo wanakandamizwa na Saudi?
Nchi ya Bahrain ni koloni la falme za Saudi Arabia na wala sio nchi kamili kama inavyoonekana, wananchi Bahrain wengi ni Washia na kuna kipindi walikuwa 80% kwa 20% ya sunni ambao wote wasunni walikuwa ni asili ya Saudi Arabia waliopandikizwa ili baadae waonekane kama raisa wa Bahrain
Viongozi wa Bahrain ni ukoo mmoja na wafalme wa Saudi Arabia na haina jeshi lake bali wanategemea jeshi la Saudi Arabia, ndo maana machafuko ya yaliyotokea 2011, Saudi Arabia ilipileka jeshi lote kule na kuua sana na kukamata washia wengi sana ambao ni wananchi wa Bahrain.
Kwahiyo Bahrain sio nchi kama nchi bali iko chini ya Saudi Arabia.
Twende Yemen, unajua hao washia wa Yemeni wametokea wapi? Ulisha wahi kusikia nchi inaiitwa North Yemen ?
Hii imepitia machafuko mengi sana na yote yalisababishwa na US na wakoloni wa zamani UK,
UK alikuwa anatawala kusini ya Yemen, na alipata uhuru wake kutoak kwa UK mnamo mwaka 1937 baada ya vita kubwa kutokea huku wa Yemen wa kusini wakisaidiwa na Urusi ya zamani yaani USSR.
Kaskazini walikuwa chini ya utawala wa Ottoman na ilipata uhuru wake kabla ya Yemen kusini mnamo mwaka 1918 na kuwa chini ya utawala wa washia.
Baada ya UK kushindwa kuebdelea na vita nchini Yemen kusini ndipo walipoaachia nchi, na Yemen kusini ikawa nchi ya kikomunisti kwa msaada mkuwa wa Urusi.
Kama kawaida yao US na UK wakaanza kuchochea vita kwa kuwasapoti Yemeni kaskazini ambao ni washia ili kuushinda utawala wa kikomunisti wa Yemeni kusini, hii yote ilileta hali ya machafuko miaka yote hizi nchi mbili zikiwa kama nchi kamili lakini kila siku ni vita ya kichochezi.
Ni baada ya utawala wa kikomunisti wa Urusi ulivyoanguka ndio Yemen Kaskazini wakajikuta wako peke yao na wakawa hawana budi kuanza mazungumzo na Yemeni Kaskazini, huku chini uvungu Yemen kusini ilishajisalimisha kwa waarabu na wazungu kisirisiri kwa kuwatangaza Yemen kusini ni vibaraka wa Iran kwa kuwa ni ya washia wengi kuliko wasunni.
Yemen kaskazini bila kujua ikiingia muungano na Yemen kusini mnamo 1990, lakini hakupita muda machafuko ya kichichini yakaanza Yemen kaskazini baada ya kujua wameingizwa cha kike na wasunni, na ndio vita ya kutaka kujitenga ikaanza mnamo 2014, na ndio maana Yemen kaskazini leo hii watu wasiojua wanashanga magaidi gani wanajeshi kamili na uwezo mkubwa wa kupigana ha Saudi Arabia bila kujua ilikuwa ni nchi kamili kabla ya hapo.