HUBA vs JUA KALI: Tamthiliya ya Huba wamekosea wapi?

HUBA vs JUA KALI: Tamthiliya ya Huba wamekosea wapi?

Mi kuna kipindi nilikuwa naenda sebuleni kuangalia taarifa ya habari saa mbili nakuta wanaangalia ile ya shambani, nikasema ngoja niwaunge tukae kama familia tuenjoy, sema niliipenda kiaina yule mzee na wake zake kama wote.
Ile ni nzuri
 
KARMA ya Wema Sepenga ilikufa kibudu, tulishtuka tu imefia njiani.......Sijui wenye majengo walidai majengo yao
 
Lenie em taja huo mshahara wako nikupigie mahesabu ya bajeti kali 😂😂😂i
 
Mi kuna kipindi nilikuwa naenda sebuleni kuangalia taarifa ya habari saa mbili nakuta wanaangalia ile ya shambani, nikasema ngoja niwaunge tukae kama familia tuenjoy, sema niliipenda kiaina yule mzee na wake zake kama wote.
Inaitwa Mpali 😂
 
Mpali mbona hamuijadili??

Hiyo Jua Kali imeanza kuboa kama ilivyoboa Selina kule Maisha Magic East wakati ule.
 
Jua kali inazungushwa sanaa. ilitakiwa iishe tangu mwaka jana tena sio mwishoni.

Tushaichoka mana jambo lililotakiwa litokee mwaka jana mwezi wa7 linazungushwa mpaka march 2023. Kila siku Hamu hamu na hamna jipya.

Mimi sijaangalia tangu mwezi wa2 na vile niliunganishiwa Dstv ya mchongo saizi sina ndo kabisa
Hapo Kwenye Hamu Hamu, Nimecheka [emoji1787], Nimemkumbuka Mwanangu
 
Mi kuna kipindi nilikuwa naenda sebuleni kuangalia taarifa ya habari saa mbili nakuta wanaangalia ile ya shambani, nikasema ngoja niwaunge tukae kama familia tuenjoy, sema niliipenda kiaina yule mzee na wake zake kama wote.

Mpali [emoji2][emoji2] shupiwe ananifurahisha sana
 
Maigizo na uzungu mwingi
Watu maisha ya ndotoni Wanayaleta kwenye kamera

Wengine ni makapuku na makwao tunapajua ila sasa wanavyoigiza ushua,

Chai kitandani,mara hawali ugali wanakuwa baga na pizza eti Kila siku vikao vya kampuni,mara sijui CEO,sijui body of directors,hukute wakiwa mitaani ni makapuku watoa ukurutu

Hao huba hamna kitu kazi kujichubua tu
Inaelekea hujui maana ya maigizo.
 
Huba sijawahi kuielewa haina uhalisia ata kidogo.
Mara huyu kanunua nyumba, kaiuza, kapoteza kazi niliacha kuangalia mwaka juzi.
Juakali walianza vizuri na mpaka sasa wanaenda vizuri, ila changamoto ilianza pale walivyoongeza siku kutoka siku 3 hadi siku 5 kwa wiki.
Kipindi cha siku 1 kinarefushwa kuwa siku 2. Yaani dakika 15 zote ni Luka na Femi wanabembea tu na kucheza tennis.
All in all Juakali wanajitahidi sana.
 
Back
Top Bottom