Huduma mbovu za Mtandao wa TTCL: Malalamiko ya wananchi

Nimevunja line yao..Vodacom ndo kila kitu,tukubali tukatae
Voda wapo ghali sana... hao ndo usiwataje kabisa

Tigo ofa zao zinachagua kati ya mteja na mteja... hovyo kabisa

TTCL wanawapendelea wafanyakazi zaidi wakati (pengine) wanaotumia zaid huo mtandao sio wafanyakazi

Zantel na halotel... tupige magoti tuswali

Me naona tutazunguka wee ila tutarudi pale pale kwenye mtandao wa airtel tu maana ndo wenye angalau

Lakini bado tuendelee kukumbusha na kupiga kelele kwanini bando liexpire? Mitandao ya simu ni wezi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakazia... hivi yupo aliyewahi kupiga simu customer care (huduma kwa wateja) akasaidiwa/akapokelewa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mie nimetengeneza booster Ina convert 2G Hadi 9G
 
Airtel nawakubari ila vijijini hawana hata 3g. Yaani ni E kwa kwenda mbele
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hovyo kabisa. Namaanisha hovyo. Nashangaa wao ndo wauzaji wa internet kwa makampuni mengine ya simu vipi wenyewe wanashindwa kutoa huduma inayoeleweka ata katikati ya miji ukiachana na vijijini. Ningekuwa nauwezo ningewatumbua wote waliipo maofisini.
Nyie Washindani wa TTCL mmekosa hoja sasa mmeanzisha Viroja! Tunaotumia lune za TTCL tunakula raha tu hata mtukatishe tamaa kiasi gani. Nani ata opt kwenda kwenye mitandao ya WIZI kama yenu? Unanunua MB 500 kwa elfu 5? Si upuuzi huo? Wakati TTCL 5000 napata GB 3 mwezi mzima!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu lini shirika la umma au taasisi za umma zikatoa huduma bora?

TBC

TANESCO

NIDA

SHULE ZA SERIKALI

HOSPITALI ZA SERIKALI

NK

we bado unashangaa tu?
Sijawahi kuwa na mtandao wowote mbali na TTCL. Kama ni On and Off hizo hutokea sio kwa TTCL pekee. Juzi hapa siku nzima Tigo hawakuwa hewani. Nilikuwa Mbeya wiki mbili zilizopita Voda walupotea Tukuyu siku 2. Hao Airtel nina line yao ni hovyo plus plus. Mimi sijawahi kuzima data ya TTCL na kwa kulinganisha na mitandao mingine TTCL ni the best.
Achana na hao washindani wa TTCL wanaoanzisha threads baada ya kuuona Muziki wa TTCL.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipo Bora .kununua gb 1 kwa 2000 ukaitumia au ununua gb 5 kwa 500 ambayo Ni useless..ukijibu hapo utasaidia wengi
 
Mzee mbona unatoa povu kama ni kitu personal vile?
TTCL sio mtandao wa kutegemea kwenye intaneti, spidi yake haitabiriki, yaani ni mtandao wa hovyoo
Mimi nilikuwa natumia voda, mb 500 shs 2000, nikahamia TTCL GB 1 tshs 1500
Nikatumia mwezi mmoja tu nikatupa ile line, nikarudi voda japo ni gharama.

Halafu naishi Dar sasa, sijui mkoani inakuaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda intaneti hutumii sana..kama unaingia YouTube au hata Instagram, kuangalia video ni shida sana hawa jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…