Huduma mbovu za Mtandao wa TTCL: Malalamiko ya wananchi

Huduma mbovu za Mtandao wa TTCL: Malalamiko ya wananchi

Hovyo kabisa. Namaanisha hovyo. Nashangaa wao ndo wauzaji wa internet kwa makampuni mengine ya simu vipi wenyewe wanashindwa kutoa huduma inayoeleweka ata katikati ya miji ukiachana na vijijini. Ningekuwa nauwezo ningewatumbua wote waliipo maofisini.

Mtu unasomea Business Adminstation huko mamtoni halafu hana hata ubunifu
 
Sote tunakumbuka jinsi Rais alivyowafagilia TTCL baada ya kupewa mgawo na kuagiza watumishi wa umma wote wanaopata muda wa maongezi wahamie kwenye mtandao huo.

Ama kweli wahenga walisema mgema akisifiwa tembo hulijaza maji. Ndicho kilichotokea watu walihamia huko ila sasa mtandao wao unaboa huwezi kupiga, kutuma sms wala mtandao wa internet hamna.

Sasa najiuliza kwani wanashindwa wapi? Au kwa vile wana uhakika wa kulipwa mishahara kila mwisho wa mwezi kwa kutumia kodi za wananchi walala hoi?

Mbona wenzao wa makampuni binafsi wanaweza na wako vizuri sana lazima kuna uzembe mahali fulani.

Eti unaenda kusajili laini unaambiwa mtandao hakuna na hawana mawalala kama wenzao. Umesafiri toka Mwanerumango halafu unapewa majibu mepesi tu halafu anayekujibu ametulia hana hata chembe ya wasiwasi.

Mimi niliambiwa anayehusika kaenda msikitini nikasubiri masaa mawili mwisho nikaondoka na kutupa laini yenyewe.

Hebu rekebisheni mambo jamani kwani mnakwama wapi? Kuna vijana kibao wana ujuzi wa kutosha hebu wachukueni wawawekee mambo vizuri!

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo 'ttcl' kwenye elo weka emu halafu tulia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom