KERO Responded Huduma ya Ambulance iboreshwe Hospitali ya Amana, kuna changamoto kubwa

KERO Responded Huduma ya Ambulance iboreshwe Hospitali ya Amana, kuna changamoto kubwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Nina malalamiko yangu kuhusu Hospitali ya Amana iliyopo Ilala Jijini Dar es Salaam huduma za pale zina huzunisha sana, tulimpeleka ndugu yetu alipata ajali ya Pikipiki, Jumatatu Juni 23, 2025 walikaa nae pale takribani siku nzima akapimwa kipimo cha CT Scan baada ya hapo mida ya Saa 10 Jioni akapewa transfer ya kwenda Muhimbili.

Wakasema tusubirie gari la kubebea Wagonjwa (Ambulance) likija watatupigia simu, tulisubiri pale mpaka Saa Mbili Usiku, tukaenda kuwafuata tena wakatuambia tuendelee kulisubiri bado halijafika na mgonjwa yupo katika hali mbaya sana.

Kitu cha kushangaza pale tuliona Ambulance inabeba Wafanyakazi badala ya Wagonjwa, huwezi amini tulitoka pale Saa 7 Usiku kwenda Muhimbili baada ya kusubiri muda wote huo na sio sisi tu tuliokuwa tukisubiri huduma hiyo, walikuwepo wagonjwa wengine ambao nao hali zao hazikuwa nzuri.

Yaani huduma ni mbovu sana, tulivyomuhoji yule ambaye anaongoza pale, ofisi yake inatazamana na ilipo Emergency, alitupa maelezo mazuri kuwa hospitali yao ina gari mbili tu za Wagonjwa na Dereva yupo mmoja.

Ni kweli pia hata sisi tuliona kuna dereva mmoja tu ambaye alikuwa anakuja na kubadili gari na kuondoka.

Ilipofika Saa saba Usiku alipofika tu dereva huyo tukamvaa, akawa mstaarabu akaomba anywe chai japo apashe tumbo kisha atupeleke.

Kwa hali hiyo tutafika kweli na tunaona Wabunge na Serikali yetu kila siku wanajinadi kuwa Wananchi wapo katika hali nzuri.

Serikali inatakiwa kuongeza Derev ana magari ya Wagonjwa kwa kuwa ni muhimu kuliko hata hayo ma-V8 ya Wabunge yanayonunuliwa kwa gharama kubwa huku Wananchi tukiendelea kuteseka.

Tunaomba hao Wabunge waache kutusemea vitu ambavyo hawavijui ikiwa hii ni Amana inatambulika kuwa ni hospitali ya mkoa halafu ambulance zipo mbili tu na dereva mmoja.

Viongozi waache kusifia ujinga ikiwa Wananchi wanateseka sana hasa kwenye hizi sekta za afya maana kipaumbele chao ni hela ndo upate tiba inaumiza sana kwa kweli.

Japo lingine la muhimu uongozi wa Hospitali uangalie ‘customer care’ ya Wauguzi wa kike, wana majibu ya hovyo sana na yanayokera, mtu umeshavurugwa na matatizo wao nao wanakujibu kama vile unaomba msaada wakati ile ni huduma na wao wapo kazini.

Majibu ya Amana Hospital ~
Hospitali ya Amana yatoa majibu kuhusu hoja ya Mwananchi aliyedai kuna changamoto ya Huduma ya Ambulance Hospitalini hapo
 
Mbunge hana Habari za Namna hii,
Yeye muulize tu inakuwaje akisikia wenzake wanagonga Meza na yeye anaunga humohumo je Huwa ameelewa kilichozungumzw

Nchi ngumu hii Kaka Mkubwa
 
Back
Top Bottom