Kwa uzoefu wangu,Magari ya Kisouth Africa sio rafiki kwa mtu anayenza maisha.
Nfano unaweza kununua Lend Rover Discovery 3 kwa bei ya 15ml pamoja na usafiri,ukalipia ushuru 17ml jumla 35ml,likizingua buster zake linagoma kunyanyuka juu likishuka chini linataga mazima uwezi kulitoa ,bei ya buster 4 hapo dar nikati ya 4ml lakini ukifunga mkataba unaweza tumia zaidi ya miaka minne.
Kama unaanza maisha bora ukaangalia Japan spare zake zipo nyingi used pale ilala na mikoani, bei zake ni ndogo ukilinganisha na spare za Land Rover,Ford au 4Turner na Hilux . Pia Spare za Toyota za kisouth zinagoma kuingilina na Toyota ya Japan.
Magari ya kisouth spare zake hapo dar zipo nyingi pia, lakini sio bei rafiki kwa watu wenye kipato kidogo.
Kwenye ubora,ugumu, confability magari ya kisouth ni magumu sana mazuri,yametengezwa kulingana na mazingira ya barabara zetu za kiafrica ukilinganisha na magari ya Kijapan.