Huduma ya usafirishaji wa magari kutoka Afrika Kusini - Tanzania

hii kitu ni nzuri sana, though huwa siamini sana magari yanayotoka south kama sio ya wizi au kama ni bora. sikatishi tamaa, wahusina mtueleweshe tu tuwe na imani katika hilo.
SouthAfrica kuna wizi wa magari lakini sio kila Gari likitoka SouthAfrica la wizi, ukiangalia hapo juu kwenye list ya Ducoments ni pamoja na police clearance,uwezi kujua kama Gali la wizi au la bila kukaguliwa na police,kabla ya kununua Gari lazima likaguliwe na Police lasivyo utalia.

Kuhusu swala la ubora SouthAfrica kuna viwanda vya makampuni yale yale yanayouza Magari bongo nfano Toyota,Benz,Scania,Mitsubishi sioni kampuni mpya sijui hofu yako ya ubora inatokea wapi?
 
shukran kwa ufafanuzi. kama kuna police clearance basi interpol hawatakusumbua ukiwa bongo. thanks.
 
shukran kwa ufafanuzi. kama kuna police clearance basi interpol hawatakusumbua ukiwa bongo. thanks.
Pomaja na police clearance boda ya SouthAfrica Police wana access ya kuangalia kama Gari lina issues au la wakati wa ku exit pia kila boda kuna police wana access ya kuangalia kama gari limeripotiwa kuibiwa au linatafutwa,nadhani wezi wa magari watakuwa nakazi kubwa sana kama wapo.
 
kama ni hivyo, basi kuna uwezekano ukasafirisha gari toka south kwa bei ndogo kuliko hizo tunaagiza japan na uingereza.
 
kama ni hivyo, basi kuna uwezekano ukasafirisha gari toka south kwa bei ndogo kuliko hizo tunaagiza japan na uingereza.
Iko hivyo kunatofauti kubwa ya bei kwasabu
1.watu wanaogopa kununua magari SouthAfrica kwanjia ya mtandao kwasabu ya utapeli kwaiyo ushindani kwa wanunuzi ni ndogo.
2.Usafiri kwanjia ya barabara ni nafuu ukilinganisha na bahari.
3.unaepuka gharama za bandari,
4.utaepuka gharama za shipping line kwajili ya Derivery Order
5.kuna unafuu boda wa agent fees ukilinganisha na bandarini.
6.Utapata Gari lako ndani ya muda mfupi sana ukililinganisha na ugazaji wa ulaya na Japan.
 
wengi wanasema gari ya kijapani ni nzuri kuliko ya kisouth mkuu... sina utaalam na magari hivyo mimi msikilizaji tuuu
 
wengi wanasema gari ya kijapani ni nzuri kuliko ya kisouth mkuu... sina utaalam na magari hivyo mimi msikilizaji tuuu
Kwanza hakuna Gari za SouthAfrica na Kijapan bali ni kampuni moja tu,nfano Toyota ni kampuny ya Kijapani yenye branch Duniani kote pamoja na SouthAfrica,pili kampuni utengeneza magari kulingana na mazingira ya sehemu magari yataenda kutumika.
 
Vipi mku inayo ofisi kwa Dar es Salaam? Na vipi unatumia Instagram? Page yako ni ipi?.
Kama unatumia Instagram ni vema ikawa unaweka picha na details za Magari ili iwe rahisi kwetu kupata taarifa. Kuna namna mtu anaweza kudharau pesa yake kumbe ingetosha kuagiza gari
Pia unaweka makadirio ya gharama mpaka kufika Bongo
 
Office dar ipo mkuu,jirani na kigogo Polisi Post njia ya kwenda Matumbi,kuhudu instagram sina account ila na plan kufungu website yangu kwajili ya kuweka bei za gharama za usafirishaji wa Magari kutoka SouthAfrica kwenda nchi mbalimbali.
 
Sidhani kama Bima wanaweza kukulipa,na kama wanaweza kulipa ni Bima ya wapi?Wakati kote huko utapita kama transit.
Kuna wakati nilikuwa napeleka gari za IT congo kupitia rwanda. Kabla ya kutoka hapa dar kuanzia safari kuelekea congo lazima ikatwe insurance ya mda mfupi ukiwa ndani ya tz. Tukiwa boda ya RUSUMO upande wa tz, kuelekea rwanda tunakata tena ya muda mfupi. Tukiwa boda bukavu upande wa rwanda/goma upande wa congo tunakata tena insurance kuelekea congo.. Kwa ufupi utaratibu ndio huo.

Mfano hai mwingine nikiwa naelekea MOMBASA kupitia border ya horohoro upande tz/Lunga Lunga upande wa kenya. Kabla hatujavuka lazima ukate insurance ata kama unaenda leo unarudi kesho.. Natamani nikewee baadhi ya document [emoji405] kwa uhakika na ushahidi zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…