Kwanza utaratibu wa wanasiasa kuzungumza Altareni haukua wa Kilitrujia. Mafundisho ya mama kanisa, yanazuia mtu asiye na Daraja katika Kanisa, kuhutubu kwenye Mimbari.
Ndio maana, hata siku ya mazishi ya Pope Francis au siku ya Kuapishwa kwa Pope Leo, hukuona Wanasiasa wakipewa nafasi ya kuhutubia despite kwamba walikuwepo. Hata Mkatoliki mwenzetu Primier wa Italy, Georgia Meloni hakuruhusiwa.
Hivyo, uamuzi wa kanisa la Tanzania, umekuja wakati sahihi, ili kulinda heshima ya mama kanisa. Wana siasa wana majukwaa yao. Wakafanye siasa huko. Wakija kanisani, wakae wahubiriwe injili ya kweli. Kama wakiipokea itawaponya, wakikaidi, wataangamia.
#MSILETE SIASA KANISANI.