Huenda Mkoa wa Morogoro ukagawanywa na kuwa mikoa miwili; Morogoro na Kilombero

Naunga mkono hoja. Wilaya tatu za Kilombero, Malinyi na Ulanga zinajitosheleza kabisa kutengeneza Mkoa! Ikitokea hivyo, walau hata raslimali za maeneo hayo mfano zao maarufu la mpunga litatambulika ipasavyo na hivyo kuwa la kibiashara zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
 
Kilometa 800 hapo sio kweli
 


Kwahiyo usipogawanywa mabonde hayatakuwa na rutuba!.Usipogawanywa madini ya ulanga yatatoweka,hifadhi za Udzungwa na Selou zitakufa.

Hivi unafahamu kuanzisha office ya RC ni kiasi gani au unabwabwaja tu.Ni kwanini fedha za kuanzisha mikoa au wilaya zisipekekwe eg elimu au afya.
 
Ukigawanywa Mpaka utakua Mto Ruaha- Kidatu, kwahiyo Kiwanda cha Sukari Kilombero kitakua mkoa wa Morogoro sio Kilombero. Pia Makao Makuu ya Selous/ Nyerere National Park yatakua Morogoro, maana kisaki itakua Morogoro sio Kilombero, ingawa Selous ya Mahenge itakua Kilombero.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gawa mikoa hadi nyumba kumi iwe mkoa ili kila nyumba ipate RC.
 
Itakuwa vizuri sana naamini ata miundombinu itaboreshwa hasahasa barabara...Mana kumekuwa na changamoto ya barabara kutoka ifakara adi mlimba,barabara mbovu sana kipnd cha mvua ndo usisemee....kutoka ifakara adi mlimba ni km 120 lakini inachukua zaid ya masaa manne adi matano.

Pia itasaidia kuunganisha barabara ya kutoka ifakara adi mlimba na barabara ya iringa Mana pale mlimba masagati kuna border unatokea mkoa wa iringa...
So Kama hvyo tutarajie mazur kwa ujumla
 
Kilombero sugar Mashamba yao yapo kilombero na hata kiwanda kwa sasa kinahesabika kipo kilombero sio kilosa
 
Pia malinyi kutokea songea/
 
limkoa Ni likubwa sana hili aisee hata wakilikata kutoa mikoa miwili au mitatu bado litatosha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanga nayo inahitaji kugawanywa ili ardhi yake itumike vema na utajiri makubwa uliofichwa na wakoloni uweze kuwanufaisha watanzania wanyonge.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…