Huenda Mkoa wa Morogoro ukagawanywa na kuwa mikoa miwili; Morogoro na Kilombero

Kwa jografia ya Mkoa wa Morogoro ni sahihi

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
Kwa jografia ya Mkoa wa Morogoro ni sahihi

Mungu Ibariki Tz - MITz
 
watu wanaposema mkoa ugawanywe ili maendeleo yafike nashindwaga kuelewa
ina maana barabara na huduma muhimu zinashindwa kupelekwa kwasababu mkoa ni mkubwa?
ukigawanya si ndo gharama zinakuwa mara2 kujenga maofisi kulipa watumishi wapya alafu ndo waanze kupeleka maendeleo?
kama ndo ivyo basi naona hata nchi igawanywe naona
 
1. Rukwa uligawanywa wakatoa mkoa wa Katavi na mkoa wa Rukwa; wamepata maendeleo gani?

2. Arusha iligawanywa wakapata mkoa wa Arusha na Manyara; nipe maendeleo waliyopata?

3. MBEYA iligawanywa wakapata mkoa wa MBEYA na Songwe; wamepata maendeleo gani?

Hizi ni siasa tu kama zilivyosiasa nyingine.

Baada ya kugawanywa unahitaji ofisi ya mkuu wa mkoa, pesa ambayo ingetosha walau kujenga hospitali

Kisha utahitaji ofisi ya halmashauri, pesa ambayo ingetosha kufanya jambo lingine la kimaendeleo.

Tunaenda mbele na kurudi nyuma.

Dar es Salaam ni ka-mkoa kadogo, wananchi wake wana maendeleo gani?
Kuna hospitali ambazo hawamudu hata gharama za matibabu huku huduma zikiwa mbovu kabisa. Nenda Mwananyamala, nenda Amana wanateseka tu.

Wengi wanaishi kwenye mitaa na uswahilini pasipo na ramani.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu hii bongo ukiwa na tafakur sana waweza juta kwann ulizaliwa hapa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata ukiona kwenye ramani mkoa huu ni mkubwa sana makao makuu yako mbali. Mkoa sehemu ya kusini kuna fulsa kubwa ya maendeleo ila kuna kazi kubwa kufungua maeneo kwa miundombinu.
 

Umesahahu mkoa wa Mwanza kupata mkoa wa Geita..Mkoa wa Shinyanga kupata mkoa wa Simiyu.
Sijajua penye maendeleo kama Dar /Kilimanjaro iligawanywa toka wapi.
 
Ukitaka kujua moro ni kubwa angalia umbali wa kutoka moro town kwenda malinyi ni sawa na safari ya kutoka mwanza kwenda dodoma. Kwa umbali huo, wazo la kuugawa ni sahihi kabisa
 
Ukitaka kujua moro ni kubwa angalia umbali wa kutoka moro town kwenda malinyi ni sawa na safari ya kutoka mwanza kwenda dodoma. Kwa umbali huo, wazo la kuugawa ni sahihi kabisa
Karibu Msowero tule Ndizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…