Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Kawaida mzee
Nmekaa
Texas
London
Na new york kule chini
Nlikua nalala kwenye toyota NOAH umehaso sana yangu nliokua nabebea takataka
Maisha yakawa yanaenda poa kabisa
Shida ni ilikua mfano nisahau kutoa li palachichi au masalu ya nyanya ile harufu yake 🙌🏻

Nasema uwongo Kelsea ?
Dah umehaso sana pole mungu asikie kilio chako upate unapohitaji dah difficult situation
 
Labda athibitishe Kiranga ndio nitaamini, eti mkuu ni kweli?
Kuna watu wengine wana matatizo ya akili, wengine wana matatizo ya madawa ya kulevya, wengine wamefukuzwa kazi hawawezi kulipia nyumba, wanaishia kukaa kwenye magari. Ila si wengi kihivyo.

Na pia, hawa watu wengine wanakataa msaada, hawataki kukaa sehemu za kusaidiwa na serikali, nyingine zina changamoto lakini si zote. Kwa hivyo kuna masuala ya mtu kuamua kifalsafa hataki kusumbua wengine.

Maisha ya ughaibuni si lelemama, ukisikia mtu kasumama na famikia yake anaendesha maisha yake ujue si nchezo. Huku wakiweka kodi unalioa kodi sawasawa.

US is especially notorius, jealth care system yake ina matatizo sana, ukipata ugonjwa mkubwa unaweza kufilisika.

So yeah, hayo mambo yapo.

Lakini pia sehemu kama Marekani ina opportunities nyingi sana na unaweza kulala kwenye gari leo halafu ukapigana ukaitoa ukawa milionea, kwa hiyo kuwa homeless Marekani si sawa na kuwa homeless Mchafukoge.

Marekani hivi vikazi vya dola 10 mpaka 20 kwa saa huwezi kukosa. Na ukiwa na vikazi hivyo hata viwili huwezi kushindwa kulipia ki aoartment cha kiushkaji, depending on where you are kama si miji mikubwa kama New York City au San Francisco etc.

Wale ma homeless wengi wanakuwa mateja, wengine wagonjwa wa akiki na wachache watu waliokosa kazi ambao wanezoea miji yao hawataki kujiingeza kuhama.

Kuna sehemu Marekani huko Detroit na Indiana unanunua nyumba kwa $1 ukitaka.

Sasa hapo ukiwa homeless umependa mwenyewe tu kukaa mji wako ulioutaka.

Ni kama Bongo tu mtu anaweza kuwa honeless Dar lakini akienda Mlandizi tu au Kisarawe anaweza kuungaunga maisha akapata shamba akaendeleza mambo.

Tatizo ni kung'ang'ania sehemu wakati huna means za kutoboa sehemu hiyo.
 
Hearsay stories
Mkuu nyumba huku, watu wananunua kwa ma agent na uchumi wa nchi una determine market price yake, eneo pia hu determine price na factor nyingine.

Viwanja vyote vimepimwa, na unanunua kwa real estate company. Mtu unakuta na haice yake au mfano wa gari kama hizo anapark mahali analala kwenye gari, kuoga sahau ila kujisaidia vyoo ni visafi hatari, choo cha pulic huwezi linganisha hata compare na mlimani City..

Gharama za ujenzi ni kampuni unatafuta inaingia mkataba inakujengea au vipi kuna DIY.

All in all kila kitu kinawezekana ila wewe tu umejipanga vipi? Na uwezo wako wakufikiri ni upi kwenye kupanga nakutekeleza jambo husika....

Ukiwa mjamja vilevile kumiliki nyumba ni rahisi, kama ilivyo ngumu kumiliki.
 
Back
Top Bottom