Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Eeh Mercedes wametoa la Brabus ni Mansion yenye matairi.😁
Kuna diaspora mmoja alisema aliiishi kwenye gari linaloitwa Toyota Route Van changamoto ilikuwa ni kipindi cha winter baridi ni kali mno, anawasha heater kwenye gari ni shida

BW256491_94adaf.jpeg
 
So parking nayo ni bure au walipia na kma wallpa ni dollar ngp
Kuna public parking nahisi hawalipii na pia kuna public toilets pia wanaenda kuoga kumaliza mambo yao huko.
Kuishi Africa ni bahati nzuri ila wengi hatujui tu.
Huko kwa wenzetu maisha ghali sana na weather yao pia mbaya sana. Imagine wakati wa winter mabarafu kila kona wewe unaishi kwenye gari
 
Mi nadhani inatokana na seasonal employment .Kwa mfano hasla anaweza kuwepo miami florida anauza labda ice cream kipindi cha summer kunapokuwa na high season ya watalii. Msimu ukiisha anarudi new york kwenda kusafisha na kukwangua theluji barabarani. Mtu wa aina hii mtafutaji ni ngumu kupanga chumba. Hivyo kulala kwenye gari ni must. Na magari ni yale yanakuwa na caravan.
Naunga mkono hoja
 
Hata mimi nilikua najiuliza maswali kama haya inakuaje nchi yenye uchumi mkubwa kuna watu homeless.Mimi mtanzania siwezi kua homeless kwanza nina kwangu kwa wazazi na kwa bibi huko kote nina haki ya kuta nyumbani na nikienda napokelewa.Nilipofika ughaibuni nikagundua homeless wengi wazawa ni wa kujitakia hasa matumizi ya madawa sasa system inakutema ukiwa teja huwezi fanya kazi.Hawa watu bwana ubepari umewaharibu hawana huruma hata kwa watoto wao unaweza kuta teja ana wazazi matajiri hawataki hata kumuona.Tatu wahamiaji haramu hawa pia ni shida maana huwezi fanya kazi utapata wapi kupata.
Ila kuhusu kulala kwenye gari hilo sio ajabu mwingine mishe ndio zinamfanya hivo ila ni kwa msimu
 
Una uhakika Tz hakuna homeless?
 
Wakuu kuna jambo naomba tuwekane sawa, haswa kwa wale ambao wameshakaa nchi tofauti tofauti kuna taarifa nimeiona huko USA, kuna watu wanaishi kwenye magari kwasababu hawana uwezo wakulipa pango ya nyumba!

Inakuwaje mtu anaweza kumudu kuwa na gari na akalihudumia lakini akashindwa kukodi nyumba ama kununua nyumba!.. Huu ni uchumi wa namna gani.. naombeni ufafanuzi juu ya hili tafadhari
nilishawahi kuishi apartment ya hali ya chini kabisa yenye kitanda kimoja tu, eneo la kupikia, bedroom self na padogo pa kukaa kwa Euro 500. hiyo ilikuwa ni kodi ya kimaskini kwa mtu kama anayetoka tz. ila kawaida ni euro 1000 hivi kwa mwezi. kodi hio ukiwa hapa bongo utalipa masaki. usije kuondoka na kwenda kule ukiamini utalipa kodi zako za kimara na sinza, utalala barabarani hakika.
 
Back
Top Bottom