Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Kwahiyo Kiranga Anaishi kama tumbili na kuruka ruka hatulii sehemu moja?

Hebu comrade njoo ututoe tongotongo
Mkuu,

Hata mabilionea wenye majumba mengi kila sehemu wanaishi kama tumbili wanarukaruka hawatulii sehemu moja.

Mimi sijafikia level hiyo bado nina viunga vichache tu, sijafikia level ya "I got cribs in the the suburb, the hood and the city" like AZ.

Msikilize Mnyamwezi wa ukweli wa Queens New York City huyu kwanza.

View: https://youtu.be/BsY8dJXf5ko?si=9Ri2WiWXIeYrjPXM
 
Kuna watu wengine wana matatizo ya akili, wengine wana matatizo ya madawa ya kulevya, wengine wamefukuzwa kazi hawawezi kulipia nyumba, wanaishia kukaa kwenye magari. Ila si wengi kihivyo.

Na pia, hawa watu wengine wanakataa msaada, hawataki kukaa sehemu za kusaidiwa na serikali, nyingine zina changamoto lakini si zote. Kwa hivyo kuna masuala ya mtu kuamua kifalsafa hataki kusumbua wengine.

Maisha ya ughaibuni si lelemama, ukisikia mtu kasumama na famikia yake anaendesha maisha yake ujue si nchezo. Huku wakiweka kodi unalioa kodi sawasawa.

US is especially notorius, jealth care system yake ina matatizo sana, ukipata ugonjwa mkubwa unaweza kufilisika.

So yeah, hayo mambo yapo.

Lakini pia sehemu kama Marekani ina opportunities nyingi sana na unaweza kulala kwenye gari leo halafu ukapigana ukaitoa ukawa milionea, kwa hiyo kuwa homeless Marekani si sawa na kuwa homeless Mchafukoge.

Marekani hivi vikazi vya dola 10 mpaka 20 kwa saa huwezi kukosa. Na ukiwa na vikazi hivyo hata viwili huwezi kushindwa kulipia ki aoartment cha kiushkaji, depending on where you are kama si miji mikubwa kama New York City au San Francisco etc.

Wale ma homeless wengi wanakuwa mateja, wengine wagonjwa wa akiki na wachache watu waliokosa kazi ambao wanezoea miji yao hawataki kujiingeza kuhama.

Kuna sehemu Marekani huko Detroit na Indiana unanunua nyumba kwa $1 ukitaka.

Sasa hapo ukiwa homeless umependa mwenyewe tu kukaa mji wako ulioutaka.

Ni kama Bongo tu mtu anaweza kuwa honeless Dar lakini akienda Mlandizi tu au Kisarawe anaweza kuungaunga maisha akapata shamba akaendeleza mambo.

Tatizo ni kung'ang'ania sehemu wakati huna means za kutoboa sehemu hiyo.
Wewe umeelezea kiupana na umeeleweka....asante sana.....ila hapo kwenye dollars 1 kununua nyumba umenichanganya medulla umekosea au?
 
🤣🤣🤣🤣unajua naweza kukuharibia kwenye moja na mbili?I respect ur respect 🙏
Mwenyewe nimepita sehemu, nikaambiwa "Ngoja tumuulize dada mkubwa kwanza".

Haya, dada mkubwa mwenyewe kutoka sasa ikabidi tu nicheke kwanza.
 
Wewe umeelezea kiupana na umeeleweka....asante sana.....ila hapo kwenye dollars 1 kununua nyumba umenichanganya medulla umekosea au?
Kuna miji imepigika haina watu, ina nyumba zinaharibika, wanatafuta watu waje kukaa, kuzitengeneza hizo nyumba zisiharibike zaidi, na wapate walipa kodi.

Kwa hivyo kuna sehemu nyumba walikuwa wanauza mpaka $1.
 
Kweli kabisa kumiliki nyumba kama usa unatakiwa uwe una kipato aswa kwanza ardhi ni garama kubwa kuzipata na asilimia kubwa wengi ni wapangaji
 
Kuna miji imepigika haina watu, ina nyumba zinaharibika, wanatafuta watu waje kukaa, kuzitengeneza hizo nyumba zisiharibike zaidi, na wapate walipa kodi.

Kwa hivyo kuna sehemu nyumba walikuwa wanauza mpaka $1.
Aiseee hii kali....kumbe kulala kwenye gari kupenda
 
Wakuu kuna jambo naomba tuwekane sawa, haswa kwa wale ambao wameshakaa nchi tofauti tofauti kuna taarifa nimeiona huko USA, kuna watu wanaishi kwenye magari kwasababu hawana uwezo wakulipa pango ya nyumba!

Inakuwaje mtu anaweza kumudu kuwa na gari na akalihudumia lakini akashindwa kukodi nyumba ama kununua nyumba!.. Huu ni uchumi wa namna gani.. naombeni ufafanuzi juu ya hili tafadhari
Huko ughaibuni mbona nasikia Wabongo wengi kazi yao kuhudumia wazee na wenye utindio wa ubongo mshahara wake kwa Mwezi n kama 15m anashimdwaje kulipa kodi....huko maisha safi sana mshahara wa Mbunge huo kwa Bongo
 
Wakuu kuna jambo naomba tuwekane sawa, haswa kwa wale ambao wameshakaa nchi tofauti tofauti kuna taarifa nimeiona huko USA, kuna watu wanaishi kwenye magari kwasababu hawana uwezo wakulipa pango ya nyumba!

Inakuwaje mtu anaweza kumudu kuwa na gari na akalihudumia lakini akashindwa kukodi nyumba ama kununua nyumba!.. Huu ni uchumi wa namna gani.. naombeni ufafanuzi juu ya hili tafadhari
Karibu home pale kwenye lile gorofa....

1733769364014.png
 
Dah umehaso sana pole mungu asikie kilio chako upate unapohitaji dah difficult situation
Ahsante sana mkuu
Maisha haya yanataka kupambana
Texas pazuri sana ,mfano wali na mboga mboga inagonga dolla 1,
New York maisha ni ghali sana
Wali tu wenye mbilimbi dolla 3
Kelsea usichafue gazeti tafadhali 😁
 
Endelea kuota 😃😃
 
Back
Top Bottom