Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Huko ughaibuni ni kweli watu wanaishi kwenye magari kwasababu kodi ya pango ni kubwa

Huko kwa nyumba za bei hio ni Kama Lindi au Mbinga ya Marekani😁 hamna mtu anapenda kuishi Lindi Compared to Dar au Arusha za Marekani. Watu wanataka ishi New York, Atlanta, Florida au California ndio kwenye mishe.
Umenikumbusha kuna ndugu zangu wako hapo Dar miaka zaidi ya 25 sasa hawana hata mia. Kila ukiwaambia jamani tokeni hapo kaangalieni fursa sehemu nyingine wanakataa kata kata kwa madai kwamba Dar ndio kuna mishe. Sasa hua najiuliza hizo mishe zina faida gani kama hazijaweza kukusaidia miaka yote hiyo..?

Inakuaje mtu aone ni bora kulala kwenye boksi ilimradi awe anaishi mjini, kuliko kulala kwenye nyumba nzuri ila nje ya mji?
 
duh! hatari sana wakati wa baridi si huwa wanapata tabu hawa
Asikuambie mtu mkuu. Hakuna maisha magumu kama ya kuishi kwenye gari.

1. Wengi wanaishi kwenye gari ndogo za kawaida sio campers. Humo kwenye gari unakuta kabeba kila kitu yaani kuanzia nguo, vyombo, vitendea kazi nk. Wengi inabidi walale wakiwa wamekaa maana hamna pa kugeukia.

2. Kipindi cha baridi au mvua ni shida sana. Kumbuka unapolala kwenye gari huwezi kupandisha vioo mpaka juu, na pia huwezi kuwasha heater/AC usiku kucha maana itabidi gari iwe on.

3. Kiusalama pia ni hatari sana unaweza kuvamiwa saa yoyote na kujeruhiwa/uawa na mateja nk

Ni maisha ya wasiwasi na mashaka mno.
 
Wakuu kuna jambo naomba tuwekane sawa, haswa kwa wale ambao wameshakaa nchi tofauti tofauti kuna taarifa nimeiona huko USA, kuna watu wanaishi kwenye magari kwasababu hawana uwezo wakulipa pango ya nyumba!

Inakuwaje mtu anaweza kumudu kuwa na gari na akalihudumia lakini akashindwa kukodi nyumba ama kununua nyumba!.. Huu ni uchumi wa namna gani.. naombeni ufafanuzi juu ya hili tafadhari
Nipo Ingoldtsdt kwenye makao makuu ya AUDI. Huku unatumia 45% mpaka 50% ya mshahara kulipa kodi ya pango. Lakini misosi ni bei rahisi kuliko Tanzania. Ukienda Supermarkt unanunua bila kuangalia salio.
 
Zile gari ambazo ziko kama nyumba hata mimi nazihusudu sana😁 nadhani wanaziita "Camping Vans."

Ile nikiipata hata sijengi, nakuwa nalipaki Masaki tu nakula upepo wa Coco Beach
Hata Tanzania hizo caravans zipo, baada ya uhuru ikulu ilikuwa nayo ambayo alikuwa akiitumia rais Nyerere akienda vijijini enzi zile.
 
Kuna public parking nahisi hawalipii na pia kuna public toilets pia wanaenda kuoga kumaliza mambo yao huko.
Kuishi Africa ni bahati nzuri ila wengi hatujui tu.
Huko kwa wenzetu maisha ghali sana na weather yao pia mbaya sana. Imagine wakati wa winter mabarafu kila kona wewe unaishi kwenye gari
Public toilet zinajifunguaga automatically baada ya dakika 20kitu kama hicho
 
Ndio ndio.

Maisha marekani magumu sana bora hata hao wanaishi kwenye magari wengine tunaishi nje baridi na mvua vyote vyetu. Hatuna kazi, hatuna hela wala nauli za kurudi bongo. Hatuna msosi tumedhoofu, hatuna mawasiliana hapa natumia net ya library.

Ushauri wangu, watu wasije Marekani watateseka sana. Bora wabaki TZ kwenye maisha bora kwa kila mtu yaliyoletwa na CCM.
 
Back
Top Bottom