Labda athibitishe
Kiranga ndio nitaamini, eti mkuu ni kweli?
Kuna watu wengine wana matatizo ya akili, wengine wana matatizo ya madawa ya kulevya, wengine wamefukuzwa kazi hawawezi kulipia nyumba, wanaishia kukaa kwenye magari. Ila si wengi kihivyo.
Na pia, hawa watu wengine wanakataa msaada, hawataki kukaa sehemu za kusaidiwa na serikali, nyingine zina changamoto lakini si zote. Kwa hivyo kuna masuala ya mtu kuamua kifalsafa hataki kusumbua wengine.
Maisha ya ughaibuni si lelemama, ukisikia mtu kasumama na famikia yake anaendesha maisha yake ujue si nchezo. Huku wakiweka kodi unalioa kodi sawasawa.
US is especially notorius, jealth care system yake ina matatizo sana, ukipata ugonjwa mkubwa unaweza kufilisika.
So yeah, hayo mambo yapo.
Lakini pia sehemu kama Marekani ina opportunities nyingi sana na unaweza kulala kwenye gari leo halafu ukapigana ukaitoa ukawa milionea, kwa hiyo kuwa homeless Marekani si sawa na kuwa homeless Mchafukoge.
Marekani hivi vikazi vya dola 10 mpaka 20 kwa saa huwezi kukosa. Na ukiwa na vikazi hivyo hata viwili huwezi kushindwa kulipia ki aoartment cha kiushkaji, depending on where you are kama si miji mikubwa kama New York City au San Francisco etc.
Wale ma homeless wengi wanakuwa mateja, wengine wagonjwa wa akiki na wachache watu waliokosa kazi ambao wanezoea miji yao hawataki kujiingeza kuhama.
Kuna sehemu Marekani huko Detroit na Indiana unanunua nyumba kwa $1 ukitaka.
Sasa hapo ukiwa homeless umependa mwenyewe tu kukaa mji wako ulioutaka.
Ni kama Bongo tu mtu anaweza kuwa honeless Dar lakini akienda Mlandizi tu au Kisarawe anaweza kuungaunga maisha akapata shamba akaendeleza mambo.
Tatizo ni kung'ang'ania sehemu wakati huna means za kutoboa sehemu hiyo.