Huko USA huwezi kutenganisha haki za binadamu na haki za mashoga/LGBT!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Hivi watanzania wanaelewa maana ya demokrasia na haki za binadamu kama zinavyofahamika na marekani? Kwa marekani demokrasia na haki za binadamu zinaambatana na haki za mashoga almaarufu kama LGBT!! Ukikubali demokrasia na haki za binadamu zinazoigiwa debe na marekani duniani kote maana yake ni kukubali haki za mashoga! Misaada hii iliyoahidiwa ya mamilioni ya dola za marekani itatekelezeka kwa masharti ya uhuru wa haki za binadamu ikiwemo ya LGBT! Hii ni hatua ya kwanza ambayo lugha ya awali inayotumika hadharani ni DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU!! Wakati wa kutaka kupokea hiyo misaada ndio ufafanuzi wa demokrasia na haki za binadamu kwa mujibu wa marekani hufuata na hapo ndio suala la haki za mashoga/LGBT hujitokeza!! Je tutakua na ubavu wa kukataa misaada hii lukuki?? Yetu macho!! Ila Malawi walishindwa wakajikuta wanahalalisha ushoga rasmi!!

Taarifa ya Marekani iliyotolewa rasmi kuhusu makubaliano ya demokrasia na haki za binadamu hapa Tanzania wakati wa ziara ya makamu wa rais wa Marekani hapa nchini ni hii hapa:

• Kuimarisha Haki za Kidemokrasia na Utawala Bora:
Katika maombi yake ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024, utawala wa Biden-Harris umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusu demokrasia, haki na utawala nchini Tanzania. Hili ni ongezeko kubwa la msaada kwa jitihada za Tanzania katika eneo hili. Zaidi ya hayo, USAID imeichagua Tanzania kama nchi itakayopokea usaidizi kusaidia jitihada zake za kukuza ushiriki wa wanawake na wasichana katika uongozi wa kiraia na kisiasa, hivyo kutoa takriban Dola za Kimarekani Milioni 1 za ziada kugharimia programu hizi kuanzia mwaka huu.

Huko GHANA Makamu wa rais wa Marekani ambako ndiko alikoanzia ziara yake barani afrika hakumung'unya maneno kuhusu mfungamano wa demokrasia na haki za mashoga-LGBT. Huu hapa msimamo wake wakati anaongea na Rais wa GHANA:

In a joint press conference with President Nana Akufo-Addo on Monday, Harris did not directly address the bill, but affirmed that LGBT rights were “an issue that we consider to be a human rights issue, and that will not change.”
Last week, National Security Council spokesman John Kirby told reporters at the White House that LGBT rights were “something that’s a core part of our foreign policy, and it will remain so.”

Tusijidanganye kuwa msimamo huo wa Marekani kuhusu haki za binadamu na ushoga utabadilika hapa Tanzania tofauti na kwingineko!! Wamesema kabisa kuwa hilo halitabadilika na ni sehemu muhimu sera ya nchi za nje ya marekani!!

Watanzania tusije tukajikuta tumeingia mikataba kama enzi za kina MANGUNGU!! Tutaambiwa ukipenda boga penda na ua lake!!! Kwa mujibu wa Marekani huwezi ukatenganisha haki za binadamu na haki za mashoga!! Marekani ikiongea haki za binadamu ujue inaongea haki za mashoga. Tafadhali tusijitoe ufahamu tukajifanya hatujui Marekani anamaanisha nini anaozungumza habari ya demokrasia na haki za binadamu!!
 
Tungekuwa tunajiamini wenye misingi isiyoyumba tungeweka msimamo wetu wazi, ambao hata Kamala angeujua akiwa kwao Marekani, ndio maana hajakanyaga Kenya wala Uganda, amekuja straight Tanzania akijua fika sisi tuna kigugumizi ni wepesi kutongozwa, na tumeshatongozwa kwa hizo $560m.

Sasa tumebaki kutafuna kucha tu!.
 
hope kwa east Africa, Tanzania kinaweza kuwa kituo au head quarter yao... Nikiangalia naona tunazihitaji sana hela za beberu na ushirikiano nae kuliko jirani zetu.

Jirani zetu naona kama wana machale machale na ka ujasiri juu ya hili.

Hakuna Urafiki wa Beberu USA na Mwafrica, hili sahau "eti wanatusaidi masikini kama unavyotoa misaada mtaani kwa maskini" USA is about interest, kama sio leo basi kesho na kama sio wewe basi unatumika kwa niaba... Beberu hana undugu na mtu mweusi ( muwe na tahadhari juu ya hilo)
 
Spika wa bunge la GHANA ameng'aka sana kuhusu Hotuba rasmi ya makamu wa rais wa marekani aliyoitoa kwenye ziara yake nchini Ghana. Harris hakumung'unya maneno kuhusu haki za ushoga!! Lakini spika wa bunge la Ghana amesema watapitisha sheria ya kupinga ushoga. Je watanzania tuna ubavu huo?

Ghana slams ‘undemocratic’ meddling by US​

Remarks by visiting US VP Kamala Harris on LGBT laws should not be tolerated, the country's parliamentary speaker has said
Ghana slams ‘undemocratic’ meddling by US

US Vice President Kamala Harris conducts a roundtable of women entrepreneurs to discuss economic empowerment, inclusion and leadership in Accra, Ghana, March 29, 2023 © AP / Misper Apawu

Ghana intends to pass its family values act regardless of what the US says, Speaker of the Parliament Alban Bagbin has told lawmakers. He was speaking in response to remarks by US Vice President Kamala Harris on her African tour in Ghana this week, that LGBT rights were a human rights issue.

Bagbin dismissed Harris' remarks. “These things should not be tolerated. That is undemocratic! What is democracy? That somebody else would have to dictate to me, as to what is good and what is bad? Unheard of!” Bagbin said

Museveni amefanikiwa kuwapinga marekani wazi wazi kuhusu ushoga na amepitisha sheria kali sana kuhusu ushoga. Nauliza tena je Tanzania tuna ubavu huo?
 
Anajidanganya haki na kuwa huru ni maridhiano ya Mbowe na ccm?

Kumbe kuruhusu nguvu kazi kupasuliwa marinda kuwa mafaruku
 
Wadau karibuni tulipigie kelele hili kungali mapema!! Waswahili husema "mnyonge mnyongeni lakini mpeni haki yake" Rais Kikwete alisimama kidete sana kupinga ushoga wakati wa awamu yake. Aliwahi kumkataa balozi wa nchi moja ya ulaya ambaye alikuwa shoga na "mkewe alikuwa mwanaume mwenzake". Je ubavu huo upo kwa sasa? Spidi ya kuvutia misaada ya Marekani inatisha!!
 
Tungekuwa tunajiamini wenye misingi isiyoyumba tungeweka msimamo wetu wazi, ambao hata Kamala angeujua akiwa kwao Marekani, ndio maana hajakanyaga Kenya wala Uganda, amekuja straight Tanzania akijua fika sisi tuna kigugumizi ni wepesi kutongozwa, na tumeshatongozwa kwa hizo $560.

Sasa tumebaki kutafuna kucha tu!.
Kenya si ndio wamekubali kabisa LGBT kusajili NGO zao? In fact mke wa Biden alienda huko so hao sio mfano kabisa.
 
Chonde chonde viongozi wetu wasijifanye hawaelewi Marekani anamaanisha nini anapozungumza juu ya demokrasia na haki za binadamu!! Someni hapa japo najua mnafahamu sana!!

In a joint press conference with President Nana Akufo-Addo on Monday, Harris did not directly address the bill, but affirmed that LGBT rights were “an issue that we consider to be a human rights issue, and that will not change.”
Last week, National Security Council spokesman John Kirby told reporters at the White House that LGBT rights were “something that’s a core part of our foreign policy, and it will remain so.”
 
Kenya si ndio wamekubali kabisa LGBT kusajili NGO zao? In fact mke wa Biden alienda huko so hao sio mfano kabisa.
Mahakama kuu yao iliruhusu, lakini Raila na Ruto wote kwa pamoja walipinga maamuzi yale ya mahakama wazi.

Kama ikitokea Kamala akikutana na Ruto popote, anajua msimamo wake kuhusu hilo suala.
 
Anajidanganya haki na kuwa huru ni maridhiano ya Mbowe na ccm?

Kumbe kuruhusu nguvu kazi kupasuliwa marinda kuwa mafaruku
Acheni utoto kwahiyo Taliban wakisema waislam duniani wafanye Jihad basi Ina maana hata Hawa waislam wa Tanzania nao tuwaone ni jihadists?

Demokrasia Ina misingi 11, mfano uhuru wa habari, uhuru wa mahakama, Minority rights, uchaguzi huru, haki ya kusikilizwa, uwajibikaji n.k Sasa kivipi hayo yote yanalenga ushoga??

Wanachofanya USA ni minority rights ndio maana sera zao ni kulinda makundi kama watu weusi, mashoga, wanawake, haki za wanyama, mazingira n.k and not necessarily tu ushoga kama tunavyopotoshana humu.

Kingine demokrasia haukuanzia USA ilikuwepo Ugiriki huko miaka na miaka Cha kushangaza mnaigeuza kama ni ya wamarekani.

JF Haina GT siku hizi
 
Hiyo misingi 11 ya haki za binadamu ni kama unavyoifahamu wewe. Marekani wana msimamo wao tofauti kuhusu kutotenganisha kati ya demokrasia, haki za binadamu na haki za mashoga! Demokrasia na haki za binadamu kwa mujibu wa marekani ni hivyo wala hawafichi hilo!!

In a joint press conference with President Nana Akufo-Addo on Monday, Harris did not directly address the bill, but affirmed that LGBT rights were “an issue that we consider to be a human rights issue, and that will not change.”
Last week, National Security Council spokesman John Kirby told reporters at the White House that LGBT rights were “something that’s a core part of our foreign policy, and it will remain so.”
 
Hivi watanzania wanaelewa maana ya demokrasia na haki za binadamu kama zinavyofahamika na marekani? Kwa marekani demokrasia na haki za binadamu zinaambatana na haki za mashoga almaarufu kama LGBT!! Ukikubali demokrasia na haki za binadamu zinazoigiwa debe na marekani duniani kote maana yake ni kukubali haki za mashoga! Misaada hii iliyoahidiwa ya mamilioni ya dola za marekani itatekelezeka kwa masharti ya uhuru wa haki za binadamu ikiwemo ya LGBT! Hii ni hatua ya kwanza ambayo lugha ya awali inayotumika hadharani ni DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU!! Wakati wa kutaka kupokea hiyo misaada ndio ufafanuzi wa demokrasia na haki za binadamu kwa mujibu wa marekani hufuata na hapo ndio suala la haki za mashoga/LGBT hujitokeza!! Je tutakua na ubavu wa kukataa misaada hii lukuki?? Yetu macho!! Ila Malawi walishindwa wakajikuta wanahalalisha ushoga rasmi!!

Taarifa ya Marekani iliyotolewa rasmi kuhusu makubaliano ya demokrasia na haki za binadamu hapa Tanzania wakati wa ziara ya makamu wa rais wa Marekani hapa nchini ni hii hapa:

• Kuimarisha Haki za Kidemokrasia na Utawala Bora:
Katika maombi yake ya bajeti ya Mwaka wa Fedha 2024, utawala wa Biden-Harris umetenga takriban Dola za Kimarekani milioni 16.4 kugharimia programu zinazohusu demokrasia, haki na utawala nchini Tanzania. Hili ni ongezeko kubwa la msaada kwa jitihada za Tanzania katika eneo hili. Zaidi ya hayo, USAID imeichagua Tanzania kama nchi itakayopokea usaidizi kusaidia jitihada zake za kukuza ushiriki wa wanawake na wasichana katika uongozi wa kiraia na kisiasa, hivyo kutoa takriban Dola za Kimarekani Milioni 1 za ziada kugharimia programu hizi kuanzia mwaka huu.

Huko GHANA Makamu wa rais wa Marekani ambako ndiko alikoanzia ziara yake barani afrika hakumung'unya maneno kuhusu mfungamano wa demokrasia na haki za mashoga-LGBT. Huu hapa msimamo wake wakati anaongea na Rais wa GHANA:

In a joint press conference with President Nana Akufo-Addo on Monday, Harris did not directly address the bill, but affirmed that LGBT rights were “an issue that we consider to be a human rights issue, and that will not change.”
Last week, National Security Council spokesman John Kirby told reporters at the White House that LGBT rights were “something that’s a core part of our foreign policy, and it will remain so.”

Tusijidanganye kuwa msimamo huo wa Marekani kuhusu haki za binadamu na ushoga utabadilika hapa Tanzania tofauti na kwingineko!! Wamesema kabisa kuwa hilo halitabadilika na ni sehemu muhimu sera ya nchi za nje ya marekani!!

Watanzania tusije tukajikuta tumeingia mikataba kama enzi za kina MANGUNGU!! Tutaambiwa ukipenda boga penda na ua lake!!! Kwa mujibu wa Marekani huwezi ukatenganisha haki za binadamu na haki za mashoga!! Marekani ikiongea haki za binadamu ujue inaongea haki za mashoga. Tafadhali tusijitoe ufahamu tukajifanya hatujui Marekani anamaanisha nini anaozungumza habari ya demokrasia na haki za binadamu!!
Tatizo ni kuwa, inawezekana Bi Harris anajua msimamo wa serikali ya Tanzania juu ya jambo hili:-
👇👇

1680191525886.png
 
Hiyo misingi 11 ya haki za binadamu ni kama unavyoifahamu wewe. Marekani wana msimamo wao tofauti kuhusu kutotenganisha kati ya demokrasia, haki za binadamu na haki za mashoga! Demokrasia na haki za binadamu kwa mujibu wa marekani ni hivyo wala hawafichi hilo!!

In a joint press conference with President Nana Akufo-Addo on Monday, Harris did not directly address the bill, but affirmed that LGBT rights were “an issue that we consider to be a human rights issue, and that will not change.”
Last week, National Security Council spokesman John Kirby told reporters at the White House that LGBT rights were “something that’s a core part of our foreign policy, and it will remain so.”
Sasa ushoga unaangukia kwenye minority rights ambacho ni kipengele kimoja tu Cha Demokrasia. Na nimesema sio kwa mashoga tu ila Kwa wanyama, mazingira, wanawake, watoto, Sasa why una force kwamba democracy is all about Gender Moja tu? Mnapotosha hapa kwa faida ya nani?
 
Tatizo ni kuwa, inawezekana Bi Harris anajua msimamo wa serikali ya Tanzania juu ya jambo hili:-

View attachment 2571237
Du! Nakumbuka Makonda alipinga sana ushoga kwa nguvu zote na aliamua kuwasaka. Naona Tanzania kwa kuogopa kunyimwa misaada, ikasema kupinga ushoga ni mawazo binafsi ya Makonda!! Hii ilikuwa mbaya sana! Hii taarifa kwa vyombo vya habari imeifedhehesha sana nchi yetu!
 
Sasa ushoga unaangukia kwenye minority rights ambacho ni kipengele kimoja tu Cha Demokrasia. Na nimesema sio kwa mashoga tu ila Kwa wanyama, mazingira, wanawake, watoto, Sasa why una force kwamba democracy is all about Gender Moja tu? Mnapotosha hapa kwa faida ya nani?
Hatujasema kuwa demokrasia kwa mujibu wa Marekani inaegemea kwenye ushoga tu, bali kuwa kwa mtazamo wa marekani ushoga ni sehemu muhimu sana ya demokrasia na haki za binadamu. Kwa maneno mengine kama ukitimiza vipengele vyote vya demokrasia lakini ukakataa kuruhusu uchafu wa ushoga, utahesabika kuwa taifa lisiloheshimu demokrasia na haki za watu!
 
Back
Top Bottom