Huku mtaani kwa sasa hakuna mwanasiasa maarufu kuliko Makonda

Wanafanya vizuri sababu wanakibomoa chama Chao Kwa kuifanya Serikali nzima ionekane Si kitu mbele ya Mwenezi.

Wananchi tunafurahia move hii kama tu itasababisha chama kuangukia pua 2025.
CCM haitegemei kura yako, ina NEC Fake na polisi
 
CCM haitegemei kura yako, ina NEC Fake na polisi
Kama haitegemei kura za wananchi,

Kwanini wanatumia nguvu kubwa kuigiza kuwa wanakubalika?

Ingekuwa ni Kweli isemayo, wangeweka nne na wasijihangaishe na chochote wakiamini polisi na Jeshi kama usemavyo!!
 
Kama haitegemei kura za wananchi,

Kwanini wanatumia nguvu kubwa kuigiza kuwa wanakubalika?

Ingekuwa ni Kweli isemayo, wangeweka nne na wasijihangaishe na chochote wakiamini polisi na Jeshi kama usemavyo!!
Kwahiyo unaamini CCM huwa inashinda kihalali?
 
UMASHUHURI WA MAKONDA NI WA MUDA TU UTAPOROMOKA PALE TU ATAKAPOSHINDWA KUWATETEA HAO WANYONGE KWA KILE WALICHOAMINI WATAWAPA KUPITIA YEYE NI SUALA LA MUDA TU

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Tatizo watanzania wanamuona Jpm kwa Makonda. Na sio uongo Jpm anawafuasi wengi sana
T
JPM hakupendwa kwa Madaraja wala kwa Barabara alizojenga alipendwa kwa KUTUMBUA😁.

Nakuapia leo hii afufuke arudi Ikulu halafu akae KIMYA asiwafilisi Matajiri na Wafanyabiashara ASITUMBUE asiongee kwa Ukali aongee kama Mbalawa halafu uone😄

Utasikia huyu Magufuli Feki huyu🤣😆

Hii Nchi ilishalaaniwaga zamani.
 
Naomba thread za wajinga wanaolipwa kumsifia Makonda huku ndani zipelekwe kwenye vichekesho… au waende huko instagram
 
Huku Mtaani Walalahoi wanafuatilia kwa makini sana BIFU la Bashe na Makonda Walalahoi wamesahau hata kama wanashindia mlo mmoja au hata nusu mlo lakini wameanza KUBETI wengine wanasema BASHE anatumbuliwa wengine wanasema Makonda ndie ATAKAEUFYATA Mkia😁

Kwa Mtu anaehangaika kumjua Mtanzania au labda unataka KUMKOMBOA Mtanzania😆 zaidi ni kupoteza muda tu.
 
Makonda ana akili za kuzaliwa, ni mzalendo na mchapa kazi. Mungu ambariki sana Makonda wetu.
Labda akili za Makonda ziko kwenye msambwanda, ila kama ni kichwani nakataa, hakuna kitu. Yaani ZEROBRAIN
 
Labda umaarufu wa Makonda ni mkubwa kuliko wanasiasa wengine kwa kigezo cha mtaani kwako. Huyu ni mfungwa mtarajiwa tu baada ya awamu ya 6. Mark this post
 
Mkuu, tuweke umaarufu (populism) pembeni. Hii “style ya uongozi” ya Makonda unaamini ndiyo itakayowezesha serikali kuongeza utendaji (performance) wake? Kwamba ufanisi utaongezeka kwenye utatuzi wa matatizo ya wananchi na utekelezaji wa majukumu yake kwa ujumla?

Sio kwamba serikali ya CCM inatafuta “kupendwa” na wananchi kwa kuwalaghai (hoodwinking) na hizo populism gimmicks za Makonda? Eti kutatua matatizo hadharani, mubashara mbele ya vyombo vya habari! Yaani baada ya kushindwa kutimiza majukumu na wajibu wake kwenye taasisi zake sasa serikali imehamia kwenye propaganda za kilaghai mitaani.

Ndio tunatarajia wapinzani nao washindane na serikali ya CCM kwa siasa za kilaghai kama hizi ili waipate “trust” ya wananchi? That’s really sad.
 
Wanasiasa na viongozi wote na sisi pia tunajua haki huwa haitendeki kwa asilimia kubwa sana
Kila mmoja anajua Tz ingeendelea kama hakuna wizi na uongo na kubebana
Sasa huyu jamaa anapiga mule mule ingawa kwa nchi masikini ni nguvu za soda kwani hata anaemuiga alipita humo humo ila tatizo alikuwa peke yake

Nchi ukiona masikini sio kwa upumbavu bali walioko juu ndio wanakula asilimia yote
Kila mahali kuna ulaji na viongozi wanalijua hilo na wao wanakula humo na maisha ya wizi na dhulma ni kawaida

Mpaka Mawaziri wote waungane na wakurugenzi kukataa tabia hizi basi tutabakia masikini tu
Hata huyu Makonda anajua fika baada ya Uchaguzi tunarudi kule kule
 

Punguza uchawa. Unamwita maarufu na hujui kafanya Nini?.
 
Labda umaarufu wa Makonda ni mkubwa kuliko wanasiasa wengine kwa kigezo cha mtaani kwako. Huyu ni mfungwa mtarajiwa tu baada ya awamu ya 6. Mark this post

Kwa umaarufu ndio hoja
Kesi ya uhalifu ni ishu nyingine Mkuu.
Kwa nini hutaki kukubali ukweli maana ukweli wako mimi nimekubali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…