Huku ndoa yake ikipumulia mashine, Jack Wolper apata bwana mpya!

Huku ndoa yake ikipumulia mashine, Jack Wolper apata bwana mpya!

Maisha ya ndoa ni ibada huna Mungu ndani yako sahau kuhusu ndoa
Mungu ana siri kubwa, njia zake Mungu hazichunguziki kamwe, kuhusu mustakabali wa binadamu humpa amtakaye humnyima yeyote. Wangapi wametulia hawana ndoa, wangapi wahuni wana ndoa?!!
Ndoa ni mapenzi ya Mungu akikupangia hata binti awe anajiuza barabarani ataolewa tu hata akiwa hoyahoya atampata wa kumstiri,hata wanaume sisi tuwe walevi kupindukia au hauna maisha utampata wa kukufaa.
Mungu hajali nini wala nini, akitaka kukupa mchongo anakupa tu,hana baya.
 
Mungu ana siri kubwa, njia zake Mungu hazichunguziki kamwe, kuhusu mustakabali wa binadamu, humpa amtakaye humnyima yeyote, wangapi wametulia hawana ndoa, wangapi wahuni wana ndoa?!!
Ndoa ni mapenzi ya Mungu akikupangia hata binti awe anajiuza barabarani ataolewa tu hata akiwa hoyahoya atampata wa kumstiri,hata wanaume sisi tuwe walevi kupindukia au hauna maisha utampata wa kukufaa.
Mungu hajali nini wala nini, akitaka kukupa mchongo anakupa tu,hana baya.
Leo wadau mnatema madini mazito mazito 🙌🏾🙌🏾

Hii ndio kusema, Mungu ni wetu sote.
 
View attachment 2831270Ndoa ndoano! Mambo sio mambo!

Muigizaji aliyegeukia biashara, mwanadada Jackline Wolper Massawe ‘Wolper’ inaripotiwa kupata bwana mpya baada ya ndoa yake kukumbwa na sintofahamu nyingi.

Ikumbukwe Wolper alifunga ndoa takatifu na aliyekuwa baba wa mtoto wake Richard ‘Rich Mitindo’ 19/11/2022.

Wawili hao walioonekana kuwa na huba la moto, shatashata lililokolea nazi enzi za uchumba wao uliopelekea Wolper kufikia uamuzi wa kumzalia kabisa mtoto Rich hata kabla ya kufunga ndoa.

Mara nyingi walionekana wenye furaha na mapenzi tele, wakipop champagne kila uchwao na kushona sare!
Wambea na wenye husda walinyanyasika vya kutosha!

Jinamizi liliyasogelea mapenzi yao baada ya kufunga pingu za maisha, na Wolper kubarikiwa mtoto wa pili.

Ilianza kuripotiwa ndoa kuingia mdudu baada ya mumewe kuonekana akila maraha China, mbaya zaidi kwa kipindi kirefu aliendelea kubaki huko bila kurejea nchini ilipo familia yake kitendo kilichozua minong’ono!

Wolper alishindwa kujizuia, akaanza kuongea mengi ya uchungu hata alipopata nafasi ya kuhojiwa na waandishi aliongea ambayo wengi waliyatafsiri kama alama nyekundu ktk ndoa yao.

Baada ya kipindi kirefu cha mumewe kuwa nje ya nchi, ni wazi Wolper uvumilivu umemshinda nae kaamua kujipa ‘raha’ kwa kutoka kimapenzi na mwanaume anayefahamika kama Vincent Azrone almaarufu G Nex.

Mwanaume huyo imebainika kuwa ni meneja katika ukumbi maarufu wa starehe, Havoc Night Spot uliopo Masaki jijini Dar Es Salaam.

Wapenzi hao wameonekana mara nyingi pamoja, hadi katika sherehe ya kuzaliwa kwa mwaume huyo, wawili hao walikaa pamoja bila kificho!

Taarifa za uhakika ni kwamba G Nex yeye bado hajaoa, na kiumri anaonekana mdogo kuliko Wolper.
Mara nyingi ameonekana akiwa anaendesha gari yake Toyota Crown nyeusi.

My take; Wolper, najua ilivyo vigumu kuishi ktk stress za mapenzi na ndoa kwa mwanaume asiyeeleweka.

Sitaki kukuhukumu kwamba ulikosea kuolewa na kijana mdogo kwako kiumri ambaye damu bado ya moto anahitaji kufanya mengi kama ambavyo wewe ulifanya kwa wakati wako…

Nakuombea kheri, haya yawe ni mapito mpate kuyaweka sawa na mumeo, ndoa na iheshimiwe na watu wote!

Pichani ni mpenzi mpya mjini wa Jack Wolper, Vincent Azrone ‘G Nex’

Wenu katika ubuyu,

Nifah.
Wolper angetulia tu asije akavuka mkojo akaenda kwenye majanga zaidi bora ajikite kwenye kazi sasa hvi ni mama
 
Baada ya kipindi kirefu, nimeweka thread hii ya ubuyu katika jukwaa hili kama sehemu ya kumuenzi rafiki & binamu yangu warumi

Endelea kupumzika kwa amani binamu, niko hapa kuendeleza kile ulichokuwa unakipenda zaidi hapa JF.

Hadi tutakapoonana tena, RIP!
Andiko la dhati namna hii lazima ka[emoji485] kahusike pia, otherwise umeandika in a very real and touching!
 
Back
Top Bottom