Huku ni Kuchanganyikiwa Kwa Wanaharakati

Asante sana kungwi mbobevu,nimependa maoni yako

Njoo na part 2 ya kuichapa au kuikula halafu mwishoni unachomekea waheshimu sikukuu za kidini
 
kama kuipigania amani ya nchi ni kujidhalilisha na iwe hivyo tu
Kama lengo lako la kweli ni kupigania amani nadhani umepotoka kwa hii approach mkuu. Bilashaka wewe mwenyewe umeona mapokeo ya wachangaji kwenye threads na comments zako kuhusu maandamano ni hasi kwa asilimia kubwa. Sasa kuna haja gani kueneza ujumbe uleule ambao ni wazi wengi wanaukataa. Hata kama upo sahihi kuna haja gani kuendelea kueneza ujumbe unaokataliwa. Au unalipwa kuandika chochote? Kama unalipwa kuandika chochote basi anayekulipa naye hana akili.
 
Safi sana
 
Mkuu Kalamu,


Huenda nimekuwa kati kwa kati pale mambo mambo yamekuwa hayana madhara sana kwa jamii yetu au kwa watu wengi

Lakini kinachotokea sasa kinawaumiza watu wengi sana,kwa mazingira kama haya inabidi tujitokeze baadhi tuyakemee haya

Huwezi amini mimi sipo Lumumba wala sina kadi ya chama cha mbogamboga,lakini mambo yakiharibika hakuna mwenye chama na asiye na chama wote tunaharibikiwa


Na binafsi sifanyi hivi kwa mlengo wa kidini,kwani dini yangu inasema tenda haki hata kwa asiye kuwa muislamu au hata kwa mpagani

Upande wa Serikali pamoja na maovu yao mengi lakini wameomba wapewe muda kuleta mchakato wa katiba ambayo naamini itakuwa ni suluhu kwa mambo mengi sana

Tuwe na subira
 
Hizo ni game minds za wahuni. Hakuna maandamano any more. Wanataka kutengeneza chaos itakayoshusha uchumi na kuhangaisha jeshi na wanasiasa. Kama watafanya hivyo wananchi watawachukia vibaya sana. Wasijaribu kabisa kufanya hivyo maana krismas ni muda wao wa kuomba mungu na kutumia na familia.
 
Mtu nikishachat nae kwa muda,anaweza fake muandiko ila hawezi fake personality,

Anaweza fake mawazo ila hawezi fake thinking pattern na flow yake.

Issue ni dini au nini, mbona upo too intelligent for such gibberish.
Ndg Eyce,
Sipo kidini hata kidogo ila naona madhara ambayo yanaweza kutokea iwapo hili swala la maandamano yasiyo na Dira wala mwelekeo yakiachwa bila kukemewa

Sasa yanapopangwa kwenye sikukuu za kidini je yanakusudia nini?
 
Ndg Eyce,
Sipo kidini hata kidogo ila naona madhara ambayo yanaweza kutokea iwapo hili swala la maandamano yasiyo na Dira wala mwelekeo yakiachwa bila kukemewa

Sasa yanapopangwa kwenye sikukuu za kidini je yanakusudia nini?
Nyie ndio mnaendeleza hili suala la udini kwa kuchukulia kila kitu katika lenzi ya udini...
Wakristu hatupo hivyo mkuu ndio maana hujasikia mapadre, wachungaji au wakristu wakilalamika.

Na kwa mtu mwenye akili kama wewe, this is too low yani. Hufanani na hizo posts mkuu
 
Kwa hiyo unawaomba na kuwasihi vijana wapuuze na wasiandamane kwa sababu watauliwa..

Kwa hiyo unakiri serikali haina njia nyingine zaidi ya kuua
 
Mazingira ya kuandamana sio salama kabisa .

Sioni Kama hiyo ni njia sahihi .

Kwakuwa hao vijana wakiuliwa na kupata ulemavu je mtawasiidia .


Au jiulize vijana ambao wako katika wheel chair mpaka sasa mnawasiadia !?
 
Tupo tunaolalamika πŸ‘‹πŸΌ

Mimi ni mkristo ambaye naunga mkono maandamano na mabadiliko ila napinga kwa nguvu zote kupangwa siku ya Krismas.

Hii ni siku muhimu kiimani na ni sikukuu ya kifamilia, mbali na kuwa ya kidini.
 
Tupo tunaolalamika πŸ‘‹πŸΌ

Mimi ni mkristo ambaye naunga mkono maandamano na mabadiliko ila napinga kwa nguvu zote kupangwa siku ya Krismas.

Hii ni siku muhimu kiimani na ni sikukuu ya kifamilia, mbali na kuwa ya kidini.
Naheshimu maoni na msimamo wako. πŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎπŸ‘πŸΎ
 
Mazingira ya kuandamana sio salama kabisa .

Sioni Kama hiyo ni njia sahihi .

Kwakuwa hao vijana wakiuliwa na kupata ulemavu je mtawasiidia .


Au jiulize vijana ambao wako katika wheel chair mpaka sasa mnawasiadia !?
Ni jukumu langu mimi au aliyewaumiza ?...

Kwa nini wengi mnakwepa hili kuwa waliopiga risasi hata kwa watu waliokuwepo majumbani ndio wanapaswa kuwa accountable.

Sio mimi, sio wewe..

Kama misiba ya ajali, watu hupelekwa hospitali na kugharamiwa. Why not kwa hawa

Hujui kuna watoto wameona wazazi na ndugu zao wakiuliwa?..

Ni nani atakaeponya nafsi na kutuliza hasira ya hiyo trauma.

Unadhani watu wasipoingia barabarani ndio usalama..

Bhasi hujasoma historia za mauaji ya halaiki yaliyotokea nchi nyingi ikiwemo Rwanda..

Mioyo iliyojeruhiwa huwa haiponi na ikifanyika suppression. Au kumpa mbwa jina baya. Surely, huo ubaya utarudi tena..

Sitaki baya litokee nchi hii, sisupport chochote kiovu ila, kwa nchi yetu kupona, inabidi ukweli uruhusiwe, watu waponywe majeraha.. This is important
 

Sisi ni armless kwahiyo lazima tufanye hesabu vizuri.

Hata ile 29/10 VIJANA hawakupaswa kutoka kabisa that was a mistake.

Kwakuwa mazingira ya kuandamana hayapo safe .

Mimi nalaumu aliyesema vijana watoke na aliyewashambulia.

Wengi hapa tunakuwa Kama wanafiki familia zetu zipo salama Ila tunaambia watoto wa watu watoke this is another kind of selfish.

Hatuwezi kufanikiwa kwa style hii.
 
Upande wa Serikali pamoja na maovu yao mengi lakini wameomba wapewe muda kuleta mchakato wa katiba ambayo naamini itakuwa ni suluhu kwa mambo mengi sana
Mchakato wa katiba ndiyo chanzo cha maandamano unayoyapinga? Watu wanaandamana kwasababu ya utekaji, kukamatwa wanaopinga matendo ya uonevu au ya kifisadi ya serikali, kukamatwa kwa kutoa tu maoni yanayopingana na mitazamo ya watawala, kukosa ajira etc. Rais Samia anahitaji katiba mpya kutatua haya? Be honest "expert" wangu . Acha kurukaruka. Ukweli unaujua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…