Huku ni Kuchanganyikiwa Kwa Wanaharakati

Huku ni Kuchanganyikiwa Kwa Wanaharakati

Samia tumemchagua sisi wakati huo nyinyi mlikuwa bize mkiandika ' no reform' humu mtandaoni. Tulimpigia kura na kafanya kazi yenye kustahili ushindi wa kiti cha urais.

Mbinu zenu chafu za kutaka kuvuruga uchaguzi zimeshafeli mazima, sasa mjipange vyema zaidi. Huwezi kuiangusha dola kwa mbinu za kizamani, hii ni dola yenye miaka 48 ya uhai haiwezi kudondoshwa na watoto wa miaka ya 2000-2003.
Uhalisia unakataa.
 
Mchakato wa katiba ndiyo chanzo cha maandamano unayoyapinga? Watu wanaandamana kwasababu ya utekaji, kukamatwa wanaopinga matendo ya uonevu au ya kifisadi ya serikali, kukamatwa kwa kutoa tu maoni yanayopingana na mitazamo ya watawala, kukosa ajira etc. Rais Samia anahitaji katiba mpya kutatua haya? Be honest "expert" wangu . Acha kurukaruka. Ukweli unaujua.
Uzuri mimi huwa mkweli kwenye nyeupe nasema nyeupe na nyeusi nasema nyeusi

Sikatai hayo madai unayosema ni kweli yapo, lakini ikiwa mpango wa maandamano ambao mnataka kuufanya utaleta madhara kwa vijana wetu,je bora ni kuuacha au kuendelea nao

Yani 29 Oct vijana wameuwawa kwa maandamano hayo hayo halafu 9 decc unafanya kitu hicho hicho je hapa tupo sawa kweli?

Kuna kipindi ukiwa umezidiwa nguvu just rudi nyuma na uwe mpole huku unafikiria namna sahihi ambayo haitakuwa na madhara kwa watu wetu
 
Walishindwa kuandamana tarehe 9 hawatampata mtu hiyo tarehe 25. Muda unavyokwenda wananchi wengi wanawaelewa hawa madogo lengo lao haswa ni lipi, wanazidi kupoteza kuungwa mkono.
Mpaka sasa wanaonekana ni wahuni tu wasiotutakia mema nchi hii

Hawa tuwapige vita kwa nguvu zetu zote
 
Maandamano hata yakiruhusiwa na ulinzi ukawepo bado wataoandamana ni wachache .


Kipindi cha Curfews (Lockdown) nimeshuhudia watu wengi wakisema bora CCM Kama wanaiba waibe ile tusirudi katika hali hii


Watu wengi watanzania ukiwaambia waandamane wakati maisha yao ni hand to mouth unategemea watakusapoti.

Na sisi wazee wa keyboard huwa hatuandamani physically tunategemea vijana wenye upeo mdogo waende wakipwe shaba ili tupate cha kujadili.


Na Mange aliitafuta mbinu ya kuwachochea ikakosa ndo akaja na ile ya Tesha na kusema jeshi kitawalinda .


Mwisho vijana wamekufa na wengine wapo ktk wheelchair

Mimi binafsi sisapoti Sisiemu Ila naijua Ccm hasa wanapokuwa wanataka kukamata Dola wanageuka Kama Mbogo


Binafsi kilichotokea nilikitegemea Ila nawalaumu Sana wanaharakati uchwara
Binafsi napenda kuona watu wanaishi bila kuhisi kuonewa kwahio hata kama watu kumi wakiamua kuandamana let them - wala msilete mamluki wa kufanya fujo...,

Nadhani huko tunapoelekea itakuwa vema iwepo sehemu (designated areas) ya watu kuweza kuandamana wakati wowote. Kama sio hivyo watu waamue kwa kila issue wachache wachache kuandamana mpaka kwenye ofisi za mbunge wao / kiongozi - ila ndio hivyo hata kama uchaguzi nao watu mmeshinda kwa namba zinazo-defy logic ni vigumu kuonekana credible...., Ndio maana nilishasema kitambo

 
Makanisani tunaomba misa za marehemu tukiamini kwamba angalau zinapunguza laana inayoambatana na kumwagika kwa damu.

Sisi tunaotumia mitandao tunabeba lawama ya kutengeneza fitina na taharuki. Mtu miezi miwili anasoma habari ya uongo kuhusiana na mali za Abdul au za waziri fulani siku ya maandamano anapoingia barabarani anakwenda kuharibu mali akitegemea taarifa za uzushi alizozisoma kwa muda mrefu.

Fitina ni dhambi mbaya huwa ina majibu yanayomgusa aliyemo na asiyekuwemo. Kalipigwa risasi katoto kana miezi sita, baba zake walileta uhuni mtaani wale askari wa kikosi maalum wakaingia ndani ya nyumba wakaua wote waliokuwemo.
Tunafarijika sana ndugu zetu kwamba tupo wengi tunaumizwa na hii hali
 
Mpaka sasa wanaonekana ni wahuni tu wasiotutakia mema nchi hii

Hawa tuwapige vita kwa nguvu zetu zote
EEEee! Bwanah!
"Ni wahuni tu"?

"....mema ya nchi hii", anayotutengenezea Samia Suluhu Hassan!

Nyinyi ndio watu wema, mnayoitakia mema Tanzania ya ndoto zenu!

Hawa wahuni mtawamaliza wote; au kama huyo mwenzio alivyosema, itawalazimu wakubali tu matakwa yenu yatimie!

Alicho nacho anayeshikilia matumaini yenu ni mitutu ya bunduki; lakini uhakika wa hii mitutu kubaki mikononi mwake haujulikaani!
 
Gen-Z kitendo cha kutufungia ndani masaa 24 bila kupenda nyie watoto!! Huku Police, JWTZ na usalama wa Taifa letu wakihaha mitaani jua lote la kwao... kweli mna kiti chenu Mbinguni.

Kwa kweli bora mngeandamana kuliko kututesea vyombo vyetu vya ulinzi namna hii juani kutwa nzima.
Yale yalikuwa ni zaidi ya maandamano.
 
Hizi hoja zipo wazi kabisa sijui kwanini wanayachukulia mambo kirahisi rahisi tu kana kwamba maisha ya vijana wa watu ni bidhaa ya dukani tu
Hivi ni kwanini hapa Tanzania mtu akijaribu kutoa maoni yake kuhusu mambo ambayo anaona hayaendi sawa anaonekana mbaya na muhamasishaji wa vurugu?

Kwa mfano ukionekana mtu unaongelea masuala ya utekaji basi unakua adui wa wenye mamlaka,.. huoni kwamba mambo kama haya ndiyo yamepelekea tufike hapa tulipo leo,.. wewe kama Mwananchi huoni kwamba kuna haja ya kukemea vitu kama hivi kama kweli tuna nia ya dhati ya kulinda amani na haki kwenye jamii yetu,..??
Kwanini mtu akifanya makosa asipelekwe kwenye mamlaka husika kuhukumiwa,.. badala yake watu wanaokotwa wamepigwa na wengine kumwagiwa tindikakali na kuuwawa... Je hiyo ndiyo amani unayoitaka na kuilingania hapa?
 
Walitaka kutugeuza mafala wa hao wanaowalipa huko USA na Ulaya. Kwamba wa huko nje wanalipwa dola milioni mbili na vijana wanaokwenda mstari wa mbele wakihatarisha maisha yao wanagawana elfu hamsini hamsini!.

Hatujawa wajinga na washamba wa pesa za kishenzi kiasi cha kushindwa kabisa kuijua thamani ya amani na utu wetu. Tunaweza kuwa malofa lakini tumeshazoea ikifika jioni mtu anarudi nyumbani kwake na kukaa na familia yake akiridhika na kidogo alichonacho.

Hasara za kugeuka mapimbi wa ford foundation ni kurudisha nyuma hali zetu na hiki kilichopatikana mpaka muda huu kitoweke kabisa kisa eti hawamtaki Samia na serikali yake!.

Hatuwezi kuishi kama kambale kwamba kila mmoja wetu ana ndevu kidevuni mwake. Lazima tuheshimiane.
Fact ndugu yangu,hatuwezi kuwa sehemu ya mipango miovu kuidhuru jamii yetu
 
Binafsi nadhani serikali ingekuwa na busara hata kuruhusu watu wachache watoe pressure zao hata kwenye designated areas - Sababu kuendelea kubana watu au baadhi kuona wanaonewa sio afya kwa jamii

Likija suala la Maandamano effectiveness yake hususan kwa kipindi hiki zaidi ya kutoa stress ni debatable hususan kwa mbinu za mamlaka kuweka mamluki au goons ili kuwaondelea credibility ndio maana nilishasema kitambo sana kuhusu maandamano hata kile kipindi cha sauti ya watanzania

SAUTI ya Watanzania na Maandamano ya Bila Kikomo - There is more Than one Way to Skin a Cat....

NB: Sio busara kulaumu hao unaosema wamechanganyikiwa bali wale ambao wamewafanya wachanganyikiwe, hususan kama hao wanaharakati wanachokipigania kina mashiko au ni kweli wanaongelea injustices
Ndg logikos,

Kwanza Asante kwa maoni yako mazuri,ni zaidi ya mara mbili nimeshawahi kukutana na wewe kweye mijadala kama sikosei, upo objective sana, huna ushabiki bali unaangalia mada iliyopo mezani

Nakubaliana na wewe kwamba ni sahihi kwa Serikali kukubali watu waandamane walau watoe dukuduku lao,ni kitu kizuri sana

Sasa ukiwasikiliza Serikali wanasema hakuna aliyeenda kuomba kibari cha Maandamano zaidi ya kusikia mitandaoni tu

Mimi kwa mawazo yangu ili kuondoa sintofahamu,wangejitokeza wanaharakati wachache kwanza Waite press waeleze wanapeleka barua polisi kuomba ruhusa ya kuandamana

Hii ina faida mbili, kwanza ni ushahidi tosha kuwa barua imeenda polisi,kwahiyo kesho polisi hawasema hawajapokea

Lakini pili,ni kinga ya usalama wao kwamba watu kadhaa wameenda polisi leo kupeleka barua hawajarudi,hapo watu wanapo pa kuanzia

Hiyo barua ifuate sheria iseme lengo husika la Maandamano,je watapita njia ipi na wanataka kuonana na nani?

Hapo taratibu zitakuwa zimefuatwa na ukweli utajukona shida ipo wapi?

Kuwalaumu Wanaharakati kwa upande wangu ni sahihi sababu wao ndio wameshika rimoti na kuwa control vijana na kuwahamasisha namna ya kuyaendea mambo
 
Maandamano hata yakiruhusiwa na ulinzi ukawepo bado wataoandamana ni wachache .


Kipindi cha Curfews (Lockdown) nimeshuhudia watu wengi wakisema bora CCM Kama wanaiba waibe ile tusirudi katika hali hii


Watu wengi watanzania ukiwaambia waandamane wakati maisha yao ni hand to mouth unategemea watakusapoti.

Na sisi wazee wa keyboard huwa hatuandamani physically tunategemea vijana wenye upeo mdogo waende wakipwe shaba ili tupate cha kujadili.


Na Mange aliitafuta mbinu ya kuwachochea ikakosa ndo akaja na ile ya Tesha na kusema jeshi kitawalinda .


Mwisho vijana wamekufa na wengine wapo ktk wheelchair

Mimi binafsi sisapoti Sisiemu Ila naijua Ccm hasa wanapokuwa wanataka kukamata Dola wanageuka Kama Mbogo


Binafsi kilichotokea nilikitegemea Ila nawalaumu Sana wanaharakati uchwara
Nakubaliana na maoni yako kwa asilimia zote

Tupo kwenye keyboard hatuendi front halafu tunataka wengine wakafe kisha tuje tujadiliane hapa

Mfano waliokufa 29 Oct leo tunajadili kuhusu wao,mbona hatukufa sisi wa mitandaoni?

Je wao tu ndio wanastahili kufa kwa ajili yetu kisha sisi kazi yetu ni kuyajadili haya matukio?
 
Gen-Z kitendo cha kutufungia ndani masaa 24 bila kupenda nyie watoto!! Huku Police, JWTZ na usalama wa Taifa letu wakihaha mitaani jua lote la kwao... kweli mna kiti chenu Mbinguni.

Kwa kweli bora mngeandamana kuliko kututesea vyombo vyetu vya ulinzi namna hii juani kutwa nzima.
Yale yalikuwa ni zaidi ya maandamano.
Kuna kitu huenda hukijui kuhusu makamanda kuwa mabarabarani

Kuna jamaa mmoja nilikaa nae kwenye daladala tukawa tunajadili kuhusiana na makamanda kukaa kwenye vituo vya mwendo kasi na pembeni mwa road

Akaniambia Kuna ndugu yake ni mjeda,ukweli ni kwamba wanafurahia kutoka nje ya kambi,kule wanaboreka sana,kwahiyo wanafurahia
 
Hivi ni kwanini hapa Tanzania mtu akijaribu kutoa maoni yake kuhusu mambo ambayo anaona hayaendi sawa anaonekana mbaya na muhamasishaji wa vurugu?

Kwa mfano ukionekana mtu unaongelea masuala ya utekaji basi unakua adui wa wenye mamlaka,.. huoni kwamba mambo kama haya ndiyo yamepelekea tufike hapa tulipo leo,.. wewe kama Mwananchi huoni kwamba kuna haja ya kukemea vitu kama hivi kama kweli tuna nia ya dhati ya kulinda amani na haki kwenye jamii yetu,..??
Kwanini mtu akifanya makosa asipelekwe kwenye mamlaka husika kuhukumiwa,.. badala yake watu wanaokotwa wamepigwa na wengine kumwagiwa tindikakali na kuuwawa... Je hiyo ndiyo amani unayoitaka na kuilingania hapa?
Umegusia point ya msingi sana,kwamba wanaosema ukwelli dhidi ya serikali wanatekwa na kuadhibiwa

Je,kwa hali hii nawe utaendelea kuisema vibaya serikali utekwe ? Au ubaki kimya uwe salama
 
Uzuri mimi huwa mkweli kwenye nyeupe nasema nyeupe na nyeusi nasema nyeusi

Sikatai hayo madai unayosema ni kweli yapo, lakini ikiwa mpango wa maandamano ambao mnataka kuufanya utaleta madhara kwa vijana wetu,je bora ni kuuacha au kuendelea nao

Yani 29 Oct vijana wameuwawa kwa maandamano hayo hayo halafu 9 decc unafanya kitu hicho hicho je hapa tupo sawa kweli?

Kuna kipindi ukiwa umezidiwa nguvu just rudi nyuma na uwe mpole huku unafikiria namna sahihi ambayo haitakuwa na madhara kwa watu wetu
Sasa kama unakiri kuna udhalimu ambao hauhitaji katiba mpya unaoweza kutokomezwa sasa bado unaendelezwa kwanini unataja mchakato wa katiba kama suluhu ya haya yanayoendelea. Tukubaliane kwamba kuna mengi yanaweza kurekebishwa amani ikarejea na kudumu bila hata ya katiba mpya. Maandamano siyo issue. Sijawahi kushiriki, stashiriki ila sioni shida watu kuandamana. Serikali iache watu waandamane ila iwasimamie waandamane kwa amani.
 
Back
Top Bottom