Huku ni Kuchanganyikiwa Kwa Wanaharakati

Waache wajichanganye tu waingie huko barabarani siku ya Krismasi.

Kibano wataanza kukipata kutoka kwa raia wema waliochoshwa na ujinga wao.
 
Walishindwa kuandamana tarehe 9 hawatampata mtu hiyo tarehe 25. Muda unavyokwenda wananchi wengi wanawaelewa hawa madogo lengo lao haswa ni lipi, wanazidi kupoteza kuungwa mkono.
 
Makanisani tunaomba misa za marehemu tukiamini kwamba angalau zinapunguza laana inayoambatana na kumwagika kwa damu.

Sisi tunaotumia mitandao tunabeba lawama ya kutengeneza fitina na taharuki. Mtu miezi miwili anasoma habari ya uongo kuhusiana na mali za Abdul au za waziri fulani siku ya maandamano anapoingia barabarani anakwenda kuharibu mali akitegemea taarifa za uzushi alizozisoma kwa muda mrefu.

Fitina ni dhambi mbaya huwa ina majibu yanayomgusa aliyemo na asiyekuwemo. Kalipigwa risasi katoto kana miezi sita, baba zake walileta uhuni mtaani wale askari wa kikosi maalum wakaingia ndani ya nyumba wakaua wote waliokuwemo.
 
Tangu lini umeona watu wakafurahia dawa chungu! Watu wengi lazima mtachukia haya Team Amani tunayofanya kwakuwa tupo tofauti na nyie kwa mitazamo na maono ya mustakabali wa nchi hii

Lau tungezungumzia kuchoma vituo vya mwendo kasi au kuharibu mali au kuandamana kusikokuwa na dira wala mwelekeo mngelike na kusapoti kwa wingi

Hatupo hapa kupata sapoti yenu bali tupo hapa kupindua Meza, hatupo hap kupendwa bali tupo hapa kusema ukweli na kukemea ujinga,ndio maana wengine dawa imekuwa chungu na kuniweka ignored list which is fine wasije kupata presha

Tutaelewana tu mdogo mdogo
 
Walitaka kutugeuza mafala wa hao wanaowalipa huko USA na Ulaya. Kwamba wa huko nje wanalipwa dola milioni mbili na vijana wanaokwenda mstari wa mbele wakihatarisha maisha yao wanagawana elfu hamsini hamsini!.

Hatujawa wajinga na washamba wa pesa za kishenzi kiasi cha kushindwa kabisa kuijua thamani ya amani na utu wetu. Tunaweza kuwa malofa lakini tumeshazoea ikifika jioni mtu anarudi nyumbani kwake na kukaa na familia yake akiridhika na kidogo alichonacho.

Hasara za kugeuka mapimbi wa ford foundation ni kurudisha nyuma hali zetu na hiki kilichopatikana mpaka muda huu kitoweke kabisa kisa eti hawamtaki Samia na serikali yake!.

Hatuwezi kuishi kama kambale kwamba kila mmoja wetu ana ndevu kidevuni mwake. Lazima tuheshimiane.
 
Tunafurahi sana kuona Kuna wazalendo kama nyie mnapinga huo mpango wenye malengo mabaya kwa nchi yetu
 
Watanzania wanakupenda mara moja na wanakuchukia mara moja wakishakujua kwa undani.

Hao madalali wa wazungu kina Heche na Lissu wameshashtukiwa na wananchi walio wengi, wasitegemee kumpata mtu wa kuandamana hiyo tarehe 25 desemba na siku yoyote watakayoipanga huko mbeleni.

Wamechukiwa kwa namna wanavyojifanya hawajui madhara ya kitu wanachotaka kukifanya wakati ukweli ni kwamba hilo ndilo lengo la wao kupewa hizo pesa haramu kutoka kwa mabwana zao.

Lengo lao ovu la kuangusha uchumi mzima wa Tanzania wakiwapigania mabeberu limewakera watu wengi.
 
Sijui kwanini unanichukulia kidini zaidi,anyway huenda ndio mtazamo wako ulivyo juu ya kila mtu ambaye anajaribu kusema ukweli

Naona tuyaache kama yalivyo,amini kile ambacho unadhani ni sahihi kwako
 
Ni hivi, Samia hana uhalali wa umma, tutafanya mambo ambayo haitakaa itokee kiongozi mwingine au chama chochote kuchezea la box la kura.
Samia tumemchagua sisi wakati huo nyinyi mlikuwa bize mkiandika ' no reform' humu mtandaoni. Tulimpigia kura na kafanya kazi yenye kustahili ushindi wa kiti cha urais.

Mbinu zenu chafu za kutaka kuvuruga uchaguzi zimeshafeli mazima, sasa mjipange vyema zaidi. Huwezi kuiangusha dola kwa mbinu za kizamani, hii ni dola yenye miaka 48 ya uhai haiwezi kudondoshwa na watoto wa miaka ya 2000-2003.
 

Wanasiasa wote awe sisiemu au upinzani wanaropoti kwa mabeberu

Ndo maana Mimi binafsi siwezi kuunga harakati za wanasiasa kwakuwa wao ndo uharibu Amani ya nchi na mshikamano.


So I vowed myself that ll never play someone's game .


Hawa GEN Z endapo wasingewafata hawa wanasiasa wa kiseahili lazima wasingandamana Ila wasingechoma Mali

Ila Sativa n.k walitoa maagizo Kama hayo ya kuchoma China

Na wapinzani Wakaja na shoot to kill so wanasiasa hawafai wote haijalishi ni upinzan au sisiemu
 
Binafsi nadhani serikali ingekuwa na busara hata kuruhusu watu wachache watoe pressure zao hata kwenye designated areas - Sababu kuendelea kubana watu au baadhi kuona wanaonewa sio afya kwa jamii

Likija suala la Maandamano effectiveness yake hususan kwa kipindi hiki zaidi ya kutoa stress ni debatable hususan kwa mbinu za mamlaka kuweka mamluki au goons ili kuwaondelea credibility ndio maana nilishasema kitambo sana kuhusu maandamano hata kile kipindi cha sauti ya watanzania

SAUTI ya Watanzania na Maandamano ya Bila Kikomo - There is more Than one Way to Skin a Cat....

NB: Sio busara kulaumu hao unaosema wamechanganyikiwa bali wale ambao wamewafanya wachanganyikiwe, hususan kama hao wanaharakati wanachokipigania kina mashiko au ni kweli wanaongelea injustices
 
Kwa hiyo unawaomba na kuwasihi vijana wapuuze na wasiandamane kwa sababu watauliwa..

Kwa hiyo unakiri serikali haina njia nyingine zaidi ya kuua
Ndg Eyce,

Mimi na wewe tunajua kabisa haya maandamano hayana tija kwa namna mbili

Kwanza hayajafuata taratibu kitu ambacho kitafanya yasiruhusiwe,na ukikaidi utapata madhara


Je unafurahia vijana wapate madhara wakati mimi na wewe hatupo huko road?

Pili, haya maandamano yana sura ya kupindua serikali,ndio maana wanasema tar 9 Dec tunaikomboa Tanganyika

Je kuna Amir jeshi mkuu atakaa tu na kuwaacha mpindue nchi kirahisi tu

Tatu hamna back up ya vyombo vya Usalama,kwa maana nyingine wapo pamoja na Serikali,je mtatoboa hapo?

Tusiote ndoto za mchana
 
Mazingira ya kuandamana sio salama kabisa .

Sioni Kama hiyo ni njia sahihi .

Kwakuwa hao vijana wakiuliwa na kupata ulemavu je mtawasiidia .


Au jiulize vijana ambao wako katika wheel chair mpaka sasa mnawasiadia !?
Hizi hoja zipo wazi kabisa sijui kwanini wanayachukulia mambo kirahisi rahisi tu kana kwamba maisha ya vijana wa watu ni bidhaa ya dukani tu
 
Na binafsi sifanyi hivi kwa mlengo wa kidini,kwani dini yangu inasema tenda haki hata kwa asiye kuwa muislamu au hata kwa mpagani
Tatizo la kauli hii ni kwamba hata hao wanaotenda maovu wanaitumia hivyo hivyo. Ni kama kila mtu anaamua kujipimia uhalali wa kuitumia atakavyo.

Sasa nakuomba ukasome tena mada yako, halafu ujipime na uhalali wa kauli hii hii uliyoweka hapa.

Samia mwenyewe, kama unavyoungana naye, anaamini kabisa kuwa kila alilofanya hadi hapa, anafuata misingi ya kauli hiyo hiyo uliyoitoa hapa.

Kwa hiyo ni kama inalazimu wengine wote wasioona kama mnavyoona nyinyi ni watu wasiokuwa sawa na nyinyi.
Hili ni tatizo kubwa ambalo haliwezi kutusaidia kama taifa lenye umoja.
 
Fact tupu
 
Maandamano hata yakiruhusiwa na ulinzi ukawepo bado wataoandamana ni wachache .


Kipindi cha Curfews (Lockdown) nimeshuhudia watu wengi wakisema bora CCM Kama wanaiba waibe ile tusirudi katika hali hii


Watu wengi watanzania ukiwaambia waandamane wakati maisha yao ni hand to mouth unategemea watakusapoti.

Na sisi wazee wa keyboard huwa hatuandamani physically tunategemea vijana wenye upeo mdogo waende wakipwe shaba ili tupate cha kujadili.


Na Mange aliitafuta mbinu ya kuwachochea ikakosa ndo akaja na ile ya Tesha na kusema jeshi kitawalinda .


Mwisho vijana wamekufa na wengine wapo ktk wheelchair

Mimi binafsi sisapoti Sisiemu Ila naijua Ccm hasa wanapokuwa wanataka kukamata Dola wanageuka Kama Mbogo


Binafsi kilichotokea nilikitegemea Ila nawalaumu Sana wanaharakati uchwara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…