Pamoja na umachinga wangu, bado nikasema nisaidie nchi yangu kwa kulipa kodi, nimechukua tin namba nikakata leseni nikafungua kiosk, nikakadiriwa nilipe laki nne kwa mwaka, kila miezi mitatu 100,000/=.
Nimelipa vizuri mara tatu, mara ya nne nimechelewa kwasababu zilizo nje ya uwezo wangu ikiwemo biashara kuchechemea,
Wiki iliyopita nikakopa ili nilipe deni la serikali nakuta kuna 100,000/= principal,
1500/= riba na 150,000/= adhabu au faini ajili ya kuchelewa kulipa,
Hivi kweli mimi nitafanya biashara halali tena?
Serikali na nyie tra mjiangalie sasa