Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Kuna shule inatwa kidoti.. skuli ya kidoti nikajua kidoti huyu tumjuae kumbe ni jina la eneo..😂
 
Kuna siku nilikuwa kwenye dala dala dada moja akasema "konda niweke tobo la pili" tulijikuta dala dala nzima tunacheka

Konda anamwambia dereva zuia mkunazini (Anamaanisha shusha mkunazini).
 
Sasa uko walipokutoeni hawakuwafundisha vitu basic kama ivo? 😀 maskini wanakuteseni kweli, kwani mnarudi tarehe 30 au 28 na boti ya jioni?
 
Wewe uongo zambi
Mkuu huo ndio ukweli,
Aslimia kubwa sanaa ya machangudoaa waliopo Zanzibar ni kutoka Bara.
Tatizo leo nyinyi watu wa bara munapenda kuyachukulia maneno munayo yasikia,
Na kuyamini kwa aslimia kubwa bila kufanya uchunguzi.
Naona humu munapigana uongo mwingi kuhusu Zanzibar yetu but hatupo kama munavyodhani.
 
Kuna shule inatwa kidoti.. skuli ya kidoti nikajua kidoti huyu tumjuae kumbe ni jina la eneo..[emoji23]
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji377][emoji377][emoji377][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Kiukweli ni pazuri na pa kipekee sana asikuambie mtu!

Kuhusu pisi sijui mkuu mimi ni KE ila kuhusu lafudhi na lugha yao kwa sisi wabara tulivyo na vichwa vibovu huwa tunaishia kushangaa na kucheka wanavyoongea vile maana sisi tunaona kama matusi kumbe wenzetu kule kwao hayo maneno ni ya kawaida tu!
Ukienda Pemba ndio utachoka

Au hapo Unguja nenda tumbatu au makunduchi. Unaweza usielewe wanaongea lugha gani
 
[emoji23][emoji23] [emoji1787][emoji1787]

Makazi (Nyumba) wanaita Makalio
Utasikia mafuriko yameharibu makalio ya watu zaidi ya 600

Kubisha wanaita Kudinda
Utasikia mie nilimuambia fanya hivi usifanye vile yeye akadinda

Majina ya maeneo sasa ndiyo utacheka uzimie sijui Mchamba wima mara Kibanda maiti! Kuna sehemu inaitwa sijui Banda la Karafuu kata ya Pita na Zako!
Bila kusahau kilima nyege
 
Ahahahahaa.
Sikutokea kupafurahia kwa mara 2 ambazo nimekwenda huko.Sijapapenda bado labda ile go&return on samesae day
 
Hata wakili wanaita vakili.....
ofisi wanaita afisi
watu wa ajabu sana wale
 
Back
Top Bottom