Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Huku Zanzibar kuna mambo ya ajabu sana

Mkuu nimeishi Zanzibar miaka 7 kwahiyo ninachokiongea Nina uhakika nacho.

Nimewala Sana wazanzibari; ukiwajulia vizuri ni maharage ya Mbeya Tena take mabichi
Mkuu,kama ww umekaa Zanzibar miaka 7
Mm ndipo nilipozaliwa na kukulia na mpaka saiv naishi Zanzibar.

Kwa maana naijuwa vzr Zanzibar yangu maana nishaishi Pembaa na Unguja pia.

Nasema tena ,tatizo lenu nyinyi munapenda kuyaamini maneno ya kuambiwa wakati mengne ni uwongo.

Ww unasema umekaa miaka 7 ,miaka 7 yenyewe umekaa Makunduchi huko au Bumbwini,sasa ww elezea kuhsu utamaduni wa Makunduchi sio wa Zanzibar .

Halafu unakuja hapa kusema uongo kuhusu utamaduni wa Zanzibar,huoni aibu kuwalisha watu matango pori mkuu?
 
Naomba nikurekebishe sio harage wanasema haragwe.
Yeah wengi wasema hivyo ila hapo mie nimemnukuu yule dereva wa bodaboda aliyenipakia ndiyo alisema "harage"
 
Usiombe uende huko vinijini, wakiongea unaweza usiam ilie kitu[emoji23]
Kabisa yani. Imagine pale mjini tu kuna vitu hauelewi halafu unaambiwa bora wa mjini kule shamba ndiyo kabisa hauelewi kitu.
 
Ukienda Pemba ndio utachoka

Au hapo Unguja nenda tumbatu au makunduchi. Unaweza usielewe wanaongea lugha gani
Kabisa yani. Kule wanaweza wakakufanya ujione haujui kiswahili.
 
Rula inaitwa mstari, Daftari linaitwa buku, Sokoni ni Markit!
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
 
Itakua maskani yako ni Kwahaji tumbo wewe au mfereji wa Wima kwabizeredi, ndio kuna wajuvi wa lugha huko!!
Mgeni akifika Zanzibar, watu wa huku ukiwatizama wanazuga kama hawana tyme nae!

Lakini lazima huwa wanamfuatilia nyuma nyuma kuona anaelekea wapi na ni mgeni wa nani!
Wakishajiridhisha mahala ulipofikia wakikuona tena!!

Utawasikia " Huyu si aishi pale kwa Ariiiiii!!" (Yaani mgeni wa Ally)

Wanawake huku Zanzibar waoga sana kusemeshwa njiani na mtu wa bara, yaani hata ukimsalimia anaitikia kwa sauti ya chini wala hasimami!

Huku Zanzibari;
  • Round about inaitwa (ikipinda) au (mviringo), kwenye daladala utasikia Shusha hapo ikipindaaah! Maana yake shusha round about
  • Huku Zanzibar sufuria linaitwa dishi,
  • Kisima cha maji kinaitwa kisima cha kuvuta
  • Huku hakuna fundi bomba Bali kuna fundi mfereji, ukitaka maji ya bomba inabidi useme unaomba maji ya mferejini
  • Pombe wanaita- moja moto moja baridi
  • Ukitafuta chupi utazunguka sana hupati hadi useme unatafuta HAFU
  • Shule huku zinaitwa skuli
  • Ukitaka kununua chepe/koleo huku hawalijui hadi useme unataka Li-PAULO
Hakika huku Zanzibar ni tabu tupu, nasubiri tarehe 30 nirudi zangu bara!
 
Pia hakipo, maana hata Mzanzibar akienda Simanjiro, Arusha au Manyara akikutana na Wasandawe wanavyoongea, je kuna cha kuchekesha kwake!?
Inategemea na aina ya mbavu zake, kwani wote tumechekeshwa na ya Zenji?
 
Back
Top Bottom