HUKUMU: Levinus Kidanabi, hajamkashifu Rais Samia, Kaonewa

Kuna mtu alishitakiwa kwa kumkashifu JPM , wakadai huyo aliyekashifiwa ni Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli , lakini Tundu Lissu alipinga na kuuliza Mahakamani kama wanaweza kuthibitisha kwamba JPM ndio Magufuli , Je akiwa Rais Magufuli ?

Mshitakiwa alishinda kesi na kuachiwa
 
Unataka mpaka kuwe na name calling ndio uone kosa?

Hapo ipo wazi alikuwa akimwongelea mh rais Mia!!!

Kuwa mkweli bwana.
Huyo kijana si tu amemkashifu mh raisi, bali pia ametukana na kudhalilisha wanawake wote, alistahili hicho kifungo.
 
Hyo katiba mpya ndiyo ya kuruhusu matusi? Mna udumavu wa akili
 
Huyo kijana alikosea sana kutukana kwa kuweka kigezo cha jinsia, angemkshifu raisi kama raisi, yeye kamkashifu kwa sababu ni mwanamke, Ametukana mawazo ya kike na kukashifu kunyonyesha kana kwamba yeye hakunyonyeshwa..

Pumbavu sana, angeongezewa kifungo..
 
Sasa hapa mbona umeweka blah blah tu na mawazo yako akuna hukumu yoyote ulioiweka
 
ki mtizamo ni sawa lakini,kwenye jicho la kisheria,hasa kwenye nchi ambazo mhimili wa mahakama upo huru,kuna ugumu sana wa kudhibitisha bila kuwepo na shaka yoyote...
Kama mhusika kakili kosa kisheria inekaaje?
 
Ila masikini wanaonewa Sana kwenye nchi hii. Yani SMS Ina mafumbo haipo clear mtu anapigwa faini ya million 15?. Duh aisee sio haki kabisa.
 
Ukiona Karne ya 21 Rais anabishana na wananchi namna ya kuongea kwenye mikutano ujue mumekwisha yaani tupo 1965

Alisema ukimparua na yeye atakuparua na kukuparara haswa. Naona dogo anaparuriwa.
 
Pambaneni apunguziwe adhabu tu ndiyo kuna mwanya, lakini kuwa alikuwa anamtukana Rais Samia na wanawake wote wa Tanzania hakuna ubishi na HAWEZI chomoa.

Sukuma gang wana hasira sana, nadhani huyu alikuwa na nafasi nyeti wakati wa Magufuli
 
Hata kama hukumu ingekuwa haijatoka tupo au mngekuwa huru kuongelea hiyo kesi.
 
Siyaungi mkono maccm, ila uko sahihi. Hiyo hukumu imetolewa kwa mihemko.
 

Hapo alipotumia jinsia ndio anapo ponea kama akikata rufaa....nchi hii ina wanawake wengi viongozi
 
Tatizo hapo ni tusi ama aliyetukanwa. Wewe kusema mwenzako anaongoza kwa upumbavu, kaandika utopolo, popoma kweli, Siyo kutukana? Na wewe ufungwe maisha?

Kwa nini unatamani huyo kijana ahasiwe. Kuhasiwa kunahusiana vipi na yeye kutukana? Kweli tusi ndio mtu afungwe maisha?
 
Amesema taifa limekuwa kama lina wanawake wote, kwa hiyo anamzungumzia kiongozi wa taifa.
Hapo alipotumia jinsia ndio anapo ponea kama akikata rufaa....nchi hii ina wanawake wengi viongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…