HUKUMU: Levinus Kidanabi, hajamkashifu Rais Samia, Kaonewa

HUKUMU: Levinus Kidanabi, hajamkashifu Rais Samia, Kaonewa

Huyo pumbafu muache kwanza achezee kifir... huko magereza ndiyo akili imkae sawa. Anayesema hajatukana akumbuke hata yeye katukaniwa mama yake.

Siasa za matusi hazina nafasi. Nani kamuambia kuwa kwa vile ana mapu..mbu basi ndiyo ana akili kuliko mwanamke?
 
Wewe ndio unahisi hivyo na umetafsiri hivyo kwani taifa hili si lina Ummy mwalimu waziri wa afya? Si lina Ndalichako?
Nyie acheni kujidai mnaleta uselamavi, umy ndio kiongozi wa taifa? Walioshindwa kumtetea ni mawakili wasomi, unafikiri hawakuziona hizo arguments zenu za vijiweni? Au mnafikiri mahakamani ni kama ubishi wa Simba na Yanga?
 
Huyo kijana si tu amemkashifu mh raisi, bali pia ametukana na kudhalilisha wanawake wote, alistahili hicho kifungo.
Plus mama yake. Mtu Wa hovyo sana huyu. Hivi inakuwaje mtu azaliwe na mama (wanamke), akatunzwa na kulelewa then akikua anaona mama hana maana. Kwamba yeye ndo mwenye akili na uwezo wa kuongoza kuliko aliyemzaa?
 
Plus mama yake. Mtu Wa hovyo sana huyu. Hivi inakuwaje mtu azaliwe na mama (wanamke), akatunzwa na kulelewa then akikua anaona mama hana maana. Kwamba yeye ndo mwenye akili na uwezo wa kuongoza kuliko aliyemzaa?
Tatizo la mfumedume ukichanganya na ujinga inakuwa shida kubwa, nahisi huyu kijana ni wale wafuasi wa mwendazake waliolewa u uvccm.
 
Nataka kuuliza swali moja tu:

Kwa hiyo nikiweza ku establish alikuwa anamwongelea Rais kosa la kukashifu na hukumu ni sawa?
 
Hili suala limekuzwa na chawa wanaotafuta u jaji na teuzi nyingine.

Naiomba mahakama kupitia tena maamuzi yake na kumuachia mhukumiwa huru. The court and justice system is being abused by some few people for personal gain.

Sioni maneno ya mhukumiwa kama yamefikia threshold ya kuwa mashtaka.
Sisi wana siasa tuna ngozi ngumu ya kuvumilia maneno mabaya, makali na magumu yanayosemwa dhidi yetu. Pia tuna uwezo wa kujizuia kuleweshwa na sifa zinazotokana na utendaji wetu uliotukuka.

Maadam maza alishakiri mwenyewe kuwa yeye 'ana ngozi ngumu', sioni kama kuna haja ya kutekeleza hukumu hii kwa kuwa mama yetu mwenye ngozi ngumu 'is in no way to be affected' na maneno ya mchangia mada ambaye sasa ni mhukumiwa.

Pia nawaomba wote kujizuia ku express our negative emotion kwa kutumia maneno makali yanayoweza kuleta tafrani kwenye jamii.
 
Wanapokosea ni wanaomwita kiongozi wetu " Mama".

Yule Si mamaetu, Mamaetu ni Tanzania.

Pia Rais kama mtu ana jinsia,dini, na kabila.

Bt RAIS kama taasisi Hana jinsia, dini, kabila, Wala ukanda ni WA wote.

Kumuita kiongozi wetu Mama kunasababisha tumhurumie, tusimuhoji, Wala kumuwajibisha anapokosea, na mawaziri wengine wanatumia nafasi hiyo kutupiga halafu wanaenda kudeka.😠😠
 
Ninachoamin hii kesi sababu jamaa ni wa ccm ndo maana kina kibatala wameachaa akaangwe ila HAKUNA KESI HAPO.
 
Wanakulana wenyewee kwa wenyewee
Kwahiyo kafungwa miaka 3. Ni michache sana!

Kapendeza kwenye picha na nguo zake za Chama chetu.

FB_IMG_1666943919597.jpg
 
Viongozi wa kiafrika mwiko kukosolewa
Kikubwa kuweni wapole, na kufata mnayo ambiwa

Ova
 
Unamfahamu mke wa Mr. Tundu A Lissu anayedai ni Rais mpokonywa? Yule mmama nwenye uso mwangavu na lugha ya staha katika familia hiyo, kizaa mapacha Kulwa na Doto? Imagine nikianza kumtukana kupitia kwa mume wake bila kumtaja jina, niseme tu hiyo lugha yake matusi yake lafudhi yake na maumbo yake. Then mwisho niseme ni Mshashi, kwani kuna Washashi wangapi hapa duniani - je, utafurahi? Na baada ya hapo nikuandame wewe na mtu maaroof kama Fatuma Karume, au Mwalimu Shule, au Zuchu, mathalani, je, utafurahi? Usilolipenda wewe usimfanyie mwenziyo.
 
Salaam Wakuu,

Tusaidiane kuangazia hii kesi, tupo huru kuongea sababu Hukumu imeshatoka.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu ilimhukumu kifungo cha miaka saba na faini ya Tsh 15 milioni, Levinus Kidanabi maarufu kama 'Chief Son's kwa makosa matatu ikiwamo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Hukumu iliyotolewa Oktoba 19, 2022 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Matha Mahumbuga SIMIYU: Levinus Kidanabi Jela miaka saba na faini mil 15 kwa kumkashifu Rais Samia

Baada ya kuona Makosa yake, nikagundua hakuna hata sehemu moja alipomkashifu Rais Samia. Tujikite kwenye Makosa Mawili ya kumashifu Rais Samia.

Wakili wa Serikali Daniel Masambu na Mwendesha mashitaka wa Polisi Johndon Buhure Walidai Makosa hayo alitenda kwenye Group la WhatsApp la "Simiyu Breaking News".

Walidai Kosa la kwanza alilitenda 3/12/2021 kwamba aliandika:
"Mzazi mwenzao anawatetea Wazazi Wenzake, Mkiongozwa na Mwanamke Lazima mtafanywa kama wote mnanyonyesha; taifa limekuwa kama lina wanawake wote. Kila siku tunaongelea mambo ya kike kike"

Kosa la pili wanadai alilitenda 4/12/2021. Kwamba alitoa taarifa za Uongo:
"Mama yenu anakaribia kuugua ukichaa kitaalam tunaita anachokifanya hallucinations. Aka kamuungano tufungeni tumuombe Mungu kavunjwe ipo siku Hawa watu was kuvuka maji watatuingia kwenye Madeni madeni Makubwa maana Wanapenda starehe kuliko kazi"

Wakili wa Serikali Daniel Masambu alidai kuwa alikuwa akimkashifu Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
View attachment 2395648
MASWALI YANGU:

1. Ni wapi Levinus Kidanabi kamtaja Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan?

2. Mtu kusema Mama yenu inakuwa inamanisha Mheshimiwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan?

3. Ni watu gani Wanavuka maji?

4. Je, Kumuomba Mungu aingilie kati kuvunja kitu ni kosa?

Hii kesi ikibidi Kibata au Jebra Kambole, achangiwe aende kumtetea huyu Mwana CCM. Natamani kuona Tanganyika Law Society TLS, Watetezi mko wapi?
View attachment 2395811
View attachment 2395638
Kafungwa miaka 7 na atalipa Mil 15
Mtu wa kwanza kabisa hapa duniani kuitumia taaluma ya sheria vibaya kabisa kama ulivyofanya wewe hapa, alikuwa Kaini.

Kaini alimuua nduguye Habili na baada ya hapo Mungu alimwendea Kaini na kumuuliza "Yuko wapi Habili ndugu yako?" Kaini alimjibu Mungu kwa swali akisema "Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu"

Kisheia jibu la Kaini kwa Mungu lilikuwa sahihi kabisa; ila kiuhalisia au kiubinadamu lilikuwa ni upumbavu wa kiwango cha juu sana.

Kwa hiyo tahadhari yangu kwako ni kwamba unatakiwa ujue kuwa ukibobea sana kwenye sheria ni lazima uutangulize ubinadamu kwanza! Analysis yako hapa kisheria iko perfect kabisa kwa 100%, ila kibinadamu ni 0%. Principle moja kubwa kabisa ya matumizi mazuri kabisa ya sheia ni kwamba mwanasheria yeyote yule katika mazingira yoyote yale, anatakiwa atangulize ubinadamu kwanza halafu sheria ndiyo ifuate, na siyo kutanguliza sheria kwanza huku ubinadamu ukiwa uko nyuma!
 
Huyo mama aliyetajwa ni mamako au mamake? Ktk wapumbavu nchi hii we nafikiri unaongoza. Na ma..mbu yako unakuja kuandika huu utopolo. Kama unampenda sana mfuate gerezani.

Dopoma kweli. Alitakiwa afungwe maisha, unamtukana Rais wa nchi hivyo? We una Mama kweli? Alikuleaje? Na ahasiwe kabisa huyo hatakiwi ht kuwa na uzao atatuzalia vitu vya ajabu km mleta uzi huu
Hivi yule mwingine (Nyani Ngabu) alikuwa yuko Marekani anatukana viongozi wote wa Tanzania, siku hizi yuko wapi?
 
Back
Top Bottom