Hukumu zenye utata kama hii ya Askari Morogoro huwa zinasababishwa na nini?

Umeandika 'askali'. Basi story yako yote inapoteza mantiki na uzito. Ni utahira kushindwa kuandika vizuri kwa kiswahili, matamshi sio tatizo ila kuandika haivumiliki.
 
Moja ya shida ya Nchi hii, ni kila mtu ni mjuaji wa kila jambo. Si ajabu kukuta kijana mwenye Bachelor yake ya vitunguu swaumu ana mchallenge prof wa Sheria na watu wanamuunga mkono, si ajabu viongozi wengi wanaofanikiwa kufika ngazi za juu ni vilaza.
On huyu jamaa, ona alichoandika, ni wazi hata hajui hiyo Mahakama ya rufaa inafanyaje kazi, lakini tayari hapa analalamika. Poor Tanzania
 
Ushahidi pekee unaoweza kumtia mtu hatiani, ni

1.) ushuhuda wa mtu kukuona kwa macho ukifanya ubakaji

2.) ushahidi wa CCTV ukionyesha unafanya ubakaji

3.) Kukutwa live kwa kufumaniwa ukifanya ubakaji

4.) Kipimo cha DNA kionyesha mbegu zilizomo ni za kwako
 
Mkuu mtoa hoja ,President Trump alipotamka kuwa tunaishi in a shithole country hakututukana,ndio ukweli wenyewe!,wenzetu wanajielewa wana kitu kinaitwa rape evidence kit,hii ilitakuwa vituo vyote vya police viwe navyo na kila kituo kiwe na desk maalum la kukusanya ushahidi wa cases za namna hii, hatuna hizi kits matokeo yake tunahukumu suspects kimihemko na status ya suspect
 
Huu ni utupolo mkubwa,na inaonyesha ni jinsi gani middle class wana uwezo gani wa kufikiri, bila ya kuwa na raping evidence collection kit ni shida
 
Naomba tofauti ya 1 na 3 please
 
Masuala ya kisheria yana uwanja mpana kuliko unavyodhania.

Kukata rufaa na kutemwa haimaanishi mtuhumiwa hakutenda kosa.

Suala la kuachiliwa huru laweza kutokea kutokana na uzembe wa waandika mashitaka kuadika mashitaka kizembe zembe wakiacha vifungu muhimu nk nk.

Rufaa hufuatilia kipengele kwa kipengele kuanzia ukamataji hadi hukumu kama procedure ilifuatwa.

Dosari yoyote katika mfumo mzima wa mashitaka waweza kumwachilia huru mhalifu.

Lawama hapo ni kuzipeleka kwenye sheria zetu zenye utata, kuwa na matundu mengi ambayo wajanja hutumia kulikwepa rungu la adhabu na kupoteza haki za watu.
 
Nimekuelewa
 
Umeandika 'askali'. Basi story yako yote inapoteza mantiki na uzito. Ni utahira kushindwa kuandika vizuri kwa kiswahili, matamshi sio tatizo ila kuandika haivumiliki.
Tatizo ni ujinga kuamini kila mtu anajua kiswahili! Mi sikijui kiswahili bro!
Usifikili wote tulisoma kiswahili! Wahindi kibao kariakoo wanafanya biashara kwa kiswahili hikohiko kibovu!
Unataka watu wote tuwe kama wafanyakazi wa BAKITA
 
Sijaongelea report ya Dr, nimeongelea definition ya kubaka. Kwa mfano mtu akagusisha uume wake juu ya uke wa mwanamke bila kumuingilia kabisa, je atakuwa amebaka?
Ndo hapo sasa
 
Kabaka MTOTO!
Anaachiwa kwa sababu zipi huyo alipaswa akatwe uume wake na aendelee kutumikia taifa akiwa jela
 
Naomba tofauti ya 1 na 3 please
Hiyo 1 inaweza ikawa ni rafiki yako aliyekuwa amekusaidia kumleta huyo mhanga wa kubakwa, pengine hakutegemea ubake, ila nae akaogopankusema akabaki amekaa anakuangalia tu unavyobaka. Hiyo ya 3 ni mtoto umefumwa nae na wazazi au ndugu, hata kama huyo mtoto alikubali, bado ukifumwa ni ubakakaji
 
Awali walipomfunga mtuhumiwa walipima vipimo gani! Na je hiyo bikira ya sasa ni original?
Nafikiri hukumu kama hizo zinatakiwa abebe hakimu wa mwanzo. Apewe hiyo miaka kwa ujinga alioufanya mwanzo. Sheria zinafilishwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…