GE2025 Humphrey Polepole: Kama ulishakuwa Spika, Waziri Mkuu, au Makamu wa Rais hutakiwi kugombea urais

GE2025 Humphrey Polepole: Kama ulishakuwa Spika, Waziri Mkuu, au Makamu wa Rais hutakiwi kugombea urais

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ndiyo maana mwaka 2021 walitaka asiwe Rais...

Wakaheshimu katiba. Lakini sasa anawapanda vichwani wenzake...

Tunajua Wazanzibari ndio wako nyuma yake akisaidiwa na Watanganyika wachache...

Kama anang'ang'ania yeye na hilo genge lake la utekaji na mauaji, basi hakuna namna nyingine ya kufanya, bali ni kuhakikisha pamba ziko puani mwake au APINDULIWE KWA NGUVU..!!
Lawama zote ziende kwa aliyekuwa mkuu wa majeshi. Hiki kibibi wengi tulijua ni kitupu kichwani siku nyingi. Sijui ni kwa nini mtu aliyetakiwa kuwa na good understanding ya usalama wa nchi kama mkuu wa majeshi alishindwa kuona uwezo wake mdogo.
 
Kwanza kabisa nchi na chama haviendeshwi kwa tamaduni na desturi, vinaendeshwa kwa katiba.

Kama kitu ni muhimu sana, wakiweke katika katiba. Kusiwe na shida ya habari zisizoandikwa kikatiba. Mambo ya utamaduni kila mtu anaweza kusema yake.

Waweke katika katiba kuwa mtu akiwa VP, PM, Spika hatakiwi kuwa rais.

VP ndiye backup ya rais. Rais akifariki, kikatiba, VP automatically anaapishwa kuwa rais. Kimsingi ukimchagua mtu VP umemchagua kuwa rais wakati wowote. Alivyofariki JPM Samia alipata kuwa rais kikatiba bila hata uchaguzi.

Sasa hapo unasemaje VP hatakiwi kugombea urais wakati ukimchagua mtu VP tayari umempitisha kuwa rais wakati wowote?
Vinaendeshwa kwa tamaduni na desturi, ndio maana raisi aliyesailiwa akiwa anawania awamu ya pili huwa inatolewa form moja tu, lakini Kariba yao na taratibu zao haziruhusu form moja, lakini wao kwa miaka yote utamaduni wao Ni huo wa form moja kwa aliye madarakani
 
Na utamaduni huu umeanza lini? Mbona rais wa pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi alikuwa VP?
Kumbe kwanza majibu yangu hukuyasoma vizuri. Kuna mahali nimesema tangu kuingia Kwa mfumo wa vyama vingi.

Lakini pia hizo tamaduni zao hazivunji Katiba ya chama chao. Hakuna mahali mtu aliyeshika nyadhifa hizo alizuiwa kuchukua fomu na kupitia mchakato wa ndani ya chama hicho.

Ila vikao vya uchujaji wajumbe wake huangalia kama huyo mtaka Urais toka timu inayomaliza muda wake hana makando kando ya kushindwa Kwa timu inayomaliza muda?

Jambo la pili ni wazo kuwa Kila baada ya miaka kumi inapokuja timu Mpya huja na fikra Mpya pia.

Ingawa hakusema labda pia alimaanisha Kwa mtindo wa viongozi wa chama chao mtu kuwa kwenye nafasi hizo labda hufanya uchafu ambao akiendelea atajenga mfumo imara wa kihalifu.
 
Aseme anayotaka kusema cha msingi hasiishie na yeye kulalamika tu kama Gwajima (Askofu), aje na suluhisho na utaratibu wa kutekeleza suluhisho hilo. Kama kweli ameona Kuna tatizo ama changamoto.
Ameshatoa suluhisho kwamba Samia ajitoe kugombea na kuwatoa wahuni wote halafu taratibu, katiba, michakato ya chama ifuatwe kikamilifu.
 
Wakati huu ndio anaongea wakati akiwa ndani ya Chama hakuyaona hayo?, alikuwa nje ya Chama akavutwa akaingia Kwa Nini hakukataa kama CCM ina mapungufu anayoyasema Sasa? wakati ule wa Magufuli watu walipohitaji katiba mpya akasema sio kipaumbele chake kwa wakati huo mbona alikaa kimya?
 
Kwa hiyo mama hakutakiwa kuchukua form ya Urais?
Wee nawe mzito kuelewa, lini Chama chetu kimetoa fomu za urais? tumeshamchagua Samia wetu awe Rais tena kupeperusha chama chetu
 
Vinaendeshwa kwa tamaduni na desturi, ndio maana raisi aliyesailiwa akiwa anawania awamu ya pili huwa inatolewa form moja tu, lakini Kariba yao na taratibu zao haziruhusu form moja, lakini wao kwa miaka yote utamaduni wao Ni huo wa form moja kwa aliye madarakani
Hilo ndilo tatizo.

Kama kuna umuhimu sana wa kutolewa fomu moja tu, jambo hilo liwekwe kwenye katiba liwe wazi kikatiba.

Haya mambo ya utamaduni ndiyo mwanzo wa kuzua habari kiholela kwa sababu ya chuki binafsi na mtu mmoja halafu kusema ni suala la utamaduni.

Mfano, mtu anasemaje hatuna utamaduni wa VP kuwa rais wakati Mwinyi alikuwa VP na akawa rais?

Ukitumia point ya utamaduni hata habari za Polepole kusema utaratibu haukufuatwa kumpata Samia kama mgombea zinakosa nguvu.

Utaratibu gani ufuatwe wakati utamaduni unasema rais aliyepo madarakani hapingwi?
 
Kumbe kwanza majibu yangu hukuyasoma vizuri. Kuna mahali nimesema tangu kuingia Kwa mfumo wa vyama vingi.

Lakini pia hizo tamaduni zao hazivunji Katiba ya chama chao. Hakuna mahali mtu aliyeshika nyadhifa hizo alizuiwa kuchukua fomu na kupitia mchakato wa ndani ya chama hicho.

Ila vikao vya uchujaji wajumbe wake huangalia kama huyo mtaka Urais toka timu inayomaliza muda wake hana makando kando ya kushindwa Kwa timu inayomaliza muda?

Jambo la pili ni wazo kuwa Kila baada ya miaka kumi inapokuja timu Mpya huja na fikra Mpya pia.

Ingawa hakusema labda pia alimaanisha Kwa mtindo wa viongozi wa chama chao mtu kuwa kwenye nafasi hizo labda hufanya uchafu ambao akiendelea atajenga mfumo imara wa kihalifu.

Kwa nini unachagua hiyo point ya siasa za vyama vingi kama ndiyo cutoff point? Kwani CCM haikuwapo kabla ya hapo?

Unasemaje utamaduni hauvunji katiba wakati katiba haimkatazi PM, Spika au VP kugombea urais na mnasema utamaduni unakataza?

Huoni kuwa utamaduni unapingana na katiba hapo?
 
Polepole atufumbua macho ndani ya CCM kuwa wanataratibu zao kama ulishakuwa Spika, Waziri Mkuu au Makamo wa Rais hutakiwi kuchukuwa fomu ya kugombea Urais.

Ina maana kijiti alichonacho leo kushika uraisi alitakiwa asichukue fomu.
Katiba ya ccm ina hivyo vipengele??
 
Polepole atufumbua macho ndani ya CCM kuwa wanataratibu zao kama ulishakuwa Spika, Waziri Mkuu au Makamo wa Rais hutakiwi kuchukuwa fomu ya kugombea Urais.

Ina maana kijiti alichonacho leo kushika uraisi alitakiwa asichukue fomu.
NO REFORMS, NO ELECTION.
 
Watanzania tuacheni ujinga kidogo na tuwe werevu kidogo hapa. Huyu huyu Humphrey Polepole alikuwa akimsifu mama Samia. Tena na kuteuliwa kuwa Balozi Cuba hii leo anajifanya anatetea nini?.

Huyu anatetea Chama chake?. Nafasi ya urais ateuliwe mgombea mwengine au anataka misingi ya haki ya Watanzania wote?. Kwanini alikuwa kimya miaka yote hio mpaka kipindi hiki cha uchaguzi?. Kuna mtu anajaribu kutaka amuone awe rais ili yeye apate nafasi nzuri kama shukurani yake?. Kwanini asiwe mpigania haki kama mzee Joseph Warioba?.
 
Back
Top Bottom