Humphrey Polepole: Nataka CCM itafute mgombea mwingine wa u - Rais na sio Bi Samia Suluhu Hassan!!

Humphrey Polepole: Nataka CCM itafute mgombea mwingine wa u - Rais na sio Bi Samia Suluhu Hassan!!

1753509668130.png
 
Leo ndo nimemwelewa pole pole anachokimaanisha!!

Yani katibu ya JMT iliposema kuwa ikiwa makamu wa rais atachukuwa madaraka baada ya rais kufariki ,kwa utaratibu wa chama imara kama CCM ,ilitakiwa kuwepo utaratibu wa kutia Nia Yani kuomba kugombea kwa tiketi ya chama kwa kuomba udhamini nchi nzima. Sasa ni kama katiba imempa automatically rais aliyepo madarakani uhalali wa kugombea bila kufuata utaratibu wa chama. Hilo lipo hata kwa vyama vingine vya siasa.utasikia mtu anajitangaza kuwa nitagombea uraisi.

Nafikiri Sasa CCM ibadiri utaratibu kwamba wadhamini wa mgombea uraisi itakuwa ni kamati kuu na siyo wananchi ( wanachama wa kawaida pengine na wenye nyadhifa) .Lakini tuwe na tahadhali sana.kuna hatari ya kutengeneza kundi au ukoo Fulani wa kuwa na nguvu ya kupeana uogonzi kwa njia ya kihuni na kidigiteta kama vile Rwanda,Urusi,Iran,na mataifa mengine ya kihuni!!

Kumbe Sasa baada ya October 2025 ,kama yanayotokea Sasa ni uchakavu wa katiba ya 1977,hatuna budi kuharakisha mchato wa katiba mpya ya JMT.kwenye katiba mpya tusirihisu kamwe makamu wa rais kuchukua madaraka ya uraisi kwa muda mrefu baada ya rais kufariki Dunia!!
 
Kwa upepo huu nafikiri Makamu wa Rais asiwe na nafasi hata ya kurithi nafasi ya Urais pale Rais aliyepo madarakani anapofariki, Makamu wa Rais aendelee na nafasi yake na kuwe na kipindi kifupi cha mpito cha kupata Rais mpya atakayechaguliwa na Wananchi.

Rais hawezi kupatikana kwa kurithi. Never na ni risky kwa Rais aliyepo madarakani kuweza kuwa na mrithi ambaye hajachaguliwa na wananchi.
 

View: https://youtu.be/NoNTvQOy-z0?si=-8Jq2-K-sm5qoVoZ
➡Humphrey Polepole amefungua valve nyingine kubwa zaidi na kwa uwazi kabisa kwa genge la utekaji na mauaji la Samia Suluhu Hassan kuelekea uchaguzi mkuu 2025 kama tutaufanya as scheduled this year....

➡Amesema, CCM kama ilivyo desturi na utamaduni wake lazima ijifanyie "service". Samia Suluhu Hassan hapaswi kuwa mgombea u - Rais wa CCM tena. Amemaliza muda wake. Chama ni lazima kimwage oil ili kujihuisha, kukipa uhai..🤔

Kwa muhitasari sana, haya ni maswali aliyoulizwa na mtangazaji wa StarTV Aloyce Nyanda na yeye kujibu kwa ufasaha👇🏻​

MTANGAZAJI ALOYCE NYANDA: Msimamo wako ni dhahiri haujabadilika na unataka Chama Cha Mapinduzi kitafute mgombea mwingine wa uchaguzi ktk uchaguzi wa mwaka huu 2025 (kama utafanyika), Je ni sahihi...?

HUMPHREY POLE: Ni sahihi kabisa...

MTANGAZAJI ALOYCE NYANDA: Kwanini asiwe Bi Samia Suluhu Hassan ambaye mkutano mkuu umempitisha? Dosari iko wapi...?

HUMPHREY POLEPOLE: Kuna mambo mawili ya msingi ndani ya CCM ambayo nataka yaeleweke vyema.

➡MOSI, kwa muda mrefu CCM kimekuwa na utaratibu wa kujihuisha kila baada ya miaka 10 za awamu za uongozi wa dola na hasa ktk nafasi ya u - Rais. Kwa kiingereza huu utaratibu unaitwa internal regime changes. Na utaratibu huu wa kukihuisha chama umekifanya CCM kuendelea kuwa madhubuti na kuendelea kuaminiwa na wananchi. Tumefanya hivyo baada ya awamu za uongozi wa dola mwaka 1995 - 2005; 2005 - 2015 na hii awamu hii chini John P. Magufuli na Samia Suluhu Hassan (2015 - 2025) ni LAZIMA tufanye mabadiliko, ni lazima tufanyie service chombo chetu kabla kukiruhusu kuendelea na safari nyingine...!

➡PILI, ni desturi na utamaduni wa kikanuni ndani ya CCM. Ni kweli katiba ya nchi ya 1977 inampa haki Samia Suluhu Hassan kufanya hiki anachotaka kukifanya. Lakini katiba ya nchi haitambui utamaduni na desturi za CCM na haituambii namna tunavyopaswa kuji - conduct ktk masuala yetu ya ndani ya namna ya kumpata mgombea wetu wa u - Rais. Unaweza kuwa na haki kwa mujibu wa katiba ya JMT ya kugombea u - Rais lakini chama kikashindwa au kikakataa kukuteua kuwa mgombea kwa sbb kuna vigezo na sifa fulani kimeweka kwa ajili ya mgombea wake kwa ajili ya uimara na umadhubuti wa chama.

Sasa CCM inaweza kuamua kitangulize maslahi mapana ya chama kwanza kwa manufaa ya wanachama wote badala ya mtu mmoja kwanza au kiamue kulinda maslahi ya mtu mmoja na kukiangamiza chama na wanachama wote..

Mfano Mama Samia amekuwa Vice President kwa miaka 6 na Rais kamili kwa miaka 4 ktk awamu hii inayomaliza muda wake mwaka huu 2025. Ni nini kipya atakifanya amvacho ameshindwa kukifanya kwa miaka 10 akiwa VP na Rais kamili? Hiki ni moja ya kigezo chama hukizingatia...


Huu ni mwaka wa kufanya INTERNAL REGIME CHANGES. CCM ni LAZIMA ipate mgombea u - Rais mpya...!!
 
Back
Top Bottom