Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 26,483
- 40,130
Mdogo wangu Polepole heshima nyingi kwako. Kiumri ninakuzidi lakini umenizidi mengi kwenye taaluma na uzoefu. Najua unanifahamu maana tangu tukiwa wanafunzi tumefahamiana na hata ulipokuwa Mwenezi wa Mbogamboga nimeonana nawe sana pale Ofisi Ndogo Lumumba. Ingawa nilikushauri memgi ukanipinga lakini leo umekuja kufanya mengi ya baadhi niliyokushauri
Nashukuru umeweza kuunga mkono kilio na struggle ya Wapambaniaji Demokrasia nchini.
Nina ushauri hapa kwako mdogo wangu ndugu Polepole
Hayo ni baadhi ya mengi wanayohitaji kuelimishwa wananchi kuamsha ari ya kuidai Tanzania yao
Nashukuru umeweza kuunga mkono kilio na struggle ya Wapambaniaji Demokrasia nchini.
Nina ushauri hapa kwako mdogo wangu ndugu Polepole
- Kwenye public address zako, jikite sana kuelezea madhara yatokanayo na chaguzi mbovu. Kwa sehemu elezea matokeo kama vile Mtandao, Mafisadi nk
- Hitaji la Katiba mpya na manufaa yake kwa nchi
- CCM ilivyojipenyeza kwenye mifumo ya dola. Haitoshi tu kusema wameunga mfumo wa NIDA na NEC kudhibiti kura bali tuelezee namna CCM inavyonufaika na mifumo yetu ya ulinzi na usalama huku Watanzania wakiachwa nje
- Tuelezee namna CCM inavyoshirikiana na Dola kuvunja katiba na sheria za nchi.
- Watekaji ni kina nani na wanashirikiana watawala kuhujumu maisha ya wananchi
- Kujibizana na Rostam iwe sehemu ndogo isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
- Mhimili wa Mahakama
Hayo ni baadhi ya mengi wanayohitaji kuelimishwa wananchi kuamsha ari ya kuidai Tanzania yao