Humphrey Polepole popote ulipo, nakuomba fanya hivi

Humphrey Polepole popote ulipo, nakuomba fanya hivi

Magu alikuwa na nafasi nzuri sana sana ya kutupeleka kwenye Tanzania mpya lakini akaweka chama mbele. Hakujua kuwa kwenye chama kumejaa mafisi ambao shinda yao ni maslahi binafsi. Ni kulewa madaraka. Mtu anapokuwa na madaraka akili zote hupotea na zinarudi anapoondoka.
Naam wanakilinda sana chama, hali ya kuwa kimeshaleta madhara mengi sana kwenye mifumo
 
Nakuunga mkono mkuu, mabadiliko tutayaleta sisi wenyewe, tukiungana wote, na ndo maana mimi nasubiri Mama aapishwe aongeze hili gari mpaka 2030. Wala hakutakua na nguvu kubws kuwashawishi wananchi tuikomhoe nchi yetu.

Tutakua tumeshapata wote lengo moja kuichomoa ccm na yeyote atakayekaa atatakiwa kuwajibika kwa wananchi
Unabariki huu uchaguzi feki?
 
Kwamba walijaribu kumfuga kumbe jamaa wa kubagaza na kubananga yeye hafugiki?

Hatari sana.

Nadhani hiyo ndiyo sifa mojawapo ya kiongozi bora - kukataa kufungiwa kwenye chupa.
Waliomshauri Samia kumpeleka jamaa Cuba walichemsha. Wao walidhani kumpeleka mbali ni kumkomoa, kumbe kule ndiyo kaenda kupigwa msasa wa kimapinduzi.
 
Mkuu 'Msanii'. Heshima mkuu kwa maelezo yako ya kina kwa rafiki yako Polepole..

Sikutaka kunyanyua yote uliyo mshauri na kuyatolea maoni hapa. Kwa kifupi tu, Polepole ni mwanachama mtiifu sana wa chama chake cha CCM. Hili liko wazi kabisa katika mazungumzo yake.
Tatizo ni hili moja; hata CCM ikitumiwa na watu wabaya; bado wanaCCM kindakindaki, kama Polepole watabaki hawaamini kuwa chama chao kinavurugika.

Nisiende mbali. Maneno yaliyo nigusa katika maoni yako ni hayo hapo juu.
Kwa mtu yeyote anaye weka maslahi ya nchi yetu mbele; wakati huu siyo wakati wa kusambaza nguvu kwenye maeneo mengi na kudhoofisha uhitaji wa hayo uliyo yaweka hapo juu.

namsihi sana rafiki yako; aweke juhudi zake juu ya kuwaelimisha waTanzania wasishiriki uchaguzi wa kuwaweka chini ya utawala usiojali maslahi yao katika miaka mitano inayo fuata.
Hili kwa sasa ndilo jambo la dharura linalo hitaji kutekelezwa.
Well
Ushauri mzuri
 
Polepole kwa sasa aeleweka uzuri tu.

Hata Youtube kwa kuzingatia namba ya wafuatiliaji, wameamua kutokata video zake kwa matangazo wao waweka matangazo huku Polepole akiendelea na mjadala.

Kwa maana ingine hii ni shule ya Uongozi imekuja kivingine.

Tuendelee kuelimishana.
 
Mambo ya muhimu kabisa hayo ntamkumbusha akiingia live pale kwenye comments section
 
Unabariki huu uchaguzi feki?
Hapana mkuu, ila hakuna mbinu za kuzuia kwa sasa, huyu akipata mi5 tena watanzania ndo tutafungua akili na kuwa na umoja
 
Tatizo la HP bado yeye ni mwana CCM na hataki itoke madarakani. Lakini anataka irekebishwe mafisadi waondoke ili waendelee wao waadilifu bila kujua veggies yote imeoza inatakiwa matawi yakatwe mpaka mzizi wa mti ndio pona ya shamba..!!
 
Kuna ubaya akibaki CCM ilimradi mambo yote yakae sawa?

Au umesimuliwa tu kuhusu maongezi yake? Umemwelewa kweli?
 
Ni kosa kusafiri kwa chombo kinachomilikiwa kihalali na Mboga2?
Tena kosa kubwa, chombo chenye harufu ya damu unatakiwa ukiogope..!!
Ndiomana kabila letu ukipata ajali na gari lako mwiko kulitumia tena, coz lina historia mbaya na wewe..!!
 
Nadhani hujamfatilia Polepole tokea mwanzo au kama unamfatilia basi humalizi katika yale anayoyaeleza, yote unayomshauri alishayasema na kuhusu Rostam hatajibizana naye tena ameshasema hilo, kuanzia wiki ijayo ataanza na afya na jinsi mifumo ya bima ya afya ilivyo ya kihuni lakini pia amesema atazungumzia kuhusu Bandari na mikataba mibovu iliyosainiwa.

Kwahiyo usikae mbali na akaunti zake ili upate faida zaidi na ikibidi uungane naye katika kupambania haki za wanyonge badala ya kukaa pembeni nakusubiri majaliwa au huruma ya CCM
 
Tena kosa kubwa, chombo chenye harufu ya damu unatakiwa ukiogope..!!
Ndiomana kabila letu ukipata ajali na gari lako mwiko kulitumia tena, coz lina historia mbaya na wewe..!!
Unahisi CCM wote ni wabaya na kwamba sera yake ni mbaya 100%?

Tuseme CCM imesambaratika kabisa, halafu hao watu wakahamia CDM, italeta tofauti yoyote?
 
Mdogo wangu Polepole heshima nyingi kwako. Kiumri ninakuzidi lakini umenizidi mengi kwenye taaluma na uzoefu. Najua unanifahamu maana tangu tukiwa wanafunzi tumefahamiana na hata ulipokuwa Mwenezi wa Mbogamboga nimeonana nawe sana pale Ofisi Ndogo Lumumba. Ingawa nilikushauri memgi ukanipinga lakini leo umekuja kufanya mengi ya baadhi niliyokushauri

Nashukuru umeweza kuunga mkono kilio na struggle ya Wapambaniaji Demokrasia nchini.

Nina ushauri hapa kwako mdogo wangu ndugu Polepole
  1. Kwenye public address zako, jikite sana kuelezea madhara yatokanayo na chaguzi mbovu. Kwa sehemu elezea matokeo kama vile Mtandao, Mafisadi nk
  2. Hitaji la Katiba mpya na manufaa yake kwa nchi
  3. CCM ilivyojipenyeza kwenye mifumo ya dola. Haitoshi tu kusema wameunga mfumo wa NIDA na NEC kudhibiti kura bali tuelezee namna CCM inavyonufaika na mifumo yetu ya ulinzi na usalama huku Watanzania wakiachwa nje
  4. Tuelezee namna CCM inavyoshirikiana na Dola kuvunja katiba na sheria za nchi.
  5. Watekaji ni kina nani na wanashirikiana watawala kuhujumu maisha ya wananchi
  6. Kujibizana na Rostam iwe sehemu ndogo isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
  7. Mhimili wa Mahakama

Hayo ni baadhi ya mengi wanayohitaji kuelimishwa wananchi kuamsha ari ya kuidai Tanzania yao
Kweli kabisa, na sijui hata tunamwamini nini huyu mwehu maana inaonekana tu miguu yake yote miwili bado imo ndani ya ccm
 
Unahisi CCM wote ni wabaya na kwamba sera yake ni mbaya 100%?

Tuseme CCM imesambaratika kabisa, halafu hao watu wakahamia CDM, italeta tofauti yoyote?
Veggies yote imeoza, km ni wema kwanini wako kimya? Wote wanaangalia maslahi yao ndiomana HP naye hasemi kuhusu kuikataa mbogamboga..!!

Ikisambaratika kuna marekebisho yatafanyika na hata wakihamia chama kingine au wakirudi kupitia chama chao kuna fundisho watakuwa wamelipata..!!

Hiyo itawatia uoga watajua tukifanya ndivyo sivyo tutakipata cha mtema kuni..!!
 
Kusambaratika ndilo neno hasa alilotumia Polepole.

Bila shaka unamsapoti bila kujua.

Umesema "au wakirudi kupitia chama chao."

Awali nimekuuliza kuna ubaya gani jamaa akipigania mabadiliko akiwa huko kwao, ilimradi mabadiliko ni ya kweli?

Ni wazi hujui unalozungumzia au mko wawili mawazoni mwako.
 
Nimeandika mengi nimefuta ila naunga mkono hoja.

Jamaa namuunga mkono na na appreciate sadaka anayoifanya kwa watu ila anagusa gusa vitu vingi juu juu sana na anajiruhusu kuwa distracted na small minds.

Mfano ishu ya lile waya kubwa, hakutakiwa kabisa kuichanganya na kitu kingine chochote na alitakiwa aipige hiyo hiyo mfululizo hata vipindi 10 watu waelewa madhara yake na nafasi ya kila mmoja kwenye kulikataa hilo ndo ahamie hoja nyingine.

Au ziara ya mwisho ya JPM kwanini hakuipa airtime ya maana na mengine mengi?

Pia dagaa kama Wassira au Kamwaga, anawajadili ili iweje?
Umeona vizuri sana mkuu.

Nakuunga mkono 100%
 
Kusambaratika ndilo neno hasa alilotumia Polepole.

Bila shaka unamsapoti bila kujua.

Umesema "au wakirudi kupitia chama chao."

Awali nimekuuliza kuna ubaya gani jamaa akipigania mabadiliko akiwa huko kwao, ilimradi mabadiliko ni ya kweli?

Ni wazi hujui unalozungumzia au mko wawili mawazoni mwako.
Mabadiliko akiwa kwao? Uko serious au unatania??

Hata jeshi likiasi lazima litoke likajipange vichakani unajua ni kwanini??
 
Back
Top Bottom