Humphrey Polepole popote ulipo, nakuomba fanya hivi

Humphrey Polepole popote ulipo, nakuomba fanya hivi

Keyboard warrior kwanini wewe usielezee yote unayotaka Polepole aelezee wakati tayari umesema kuwa anachokifanya sasa hivi wewe ndo ulimshauri?
Waagize na kuwaamrisha walio chini ya himaya yako.

Mimi ni free soul nafanya kile nifanyacho.
 
Nimekuuliza sijakuamrisha. Uwezo wako kiakili ni mdogo sana.
Read between the LINES ya ushauri wako.

Najua tunayopambania ni none of your interests. Tulia usitutingishe
 
Hahaha jana nilimshangaa sana Polepole, anawashauri ccm waongelee haki wakati wa kampeni ambazo mgombea wake anasema ni haramu.

Yani unapinga mchakato, unapinga utaratibu, unapinga, mgombea, unasema uchaguzi unatakiwa usifanyike, halafu unawashauri hao hao ccm waongelee HAKI kwenye kampeni.

Kaanza kukosa maana.
 
Mdogo wangu Polepole heshima nyingi kwako. Kiumri ninakuzidi lakini umenizidi mengi kwenye taaluma na uzoefu. Najua unanifahamu maana tangu tukiwa wanafunzi tumefahamiana na hata ulipokuwa Mwenezi wa Mbogamboga nimeonana nawe sana pale Ofisi Ndogo Lumumba. Ingawa nilikushauri memgi ukanipinga lakini leo umekuja kufanya mengi ya baadhi niliyokushauri

Nashukuru umeweza kuunga mkono kilio na struggle ya Wapambaniaji Demokrasia nchini.

Nina ushauri hapa kwako mdogo wangu ndugu Polepole
  1. Kwenye public address zako, jikite sana kuelezea madhara yatokanayo na chaguzi mbovu. Kwa sehemu elezea matokeo kama vile Mtandao, Mafisadi nk
  2. Hitaji la Katiba mpya na manufaa yake kwa nchi
  3. CCM ilivyojipenyeza kwenye mifumo ya dola. Haitoshi tu kusema wameunga mfumo wa NIDA na NEC kudhibiti kura bali tuelezee namna CCM inavyonufaika na mifumo yetu ya ulinzi na usalama huku Watanzania wakiachwa nje
  4. Tuelezee namna CCM inavyoshirikiana na Dola kuvunja katiba na sheria za nchi.
  5. Watekaji ni kina nani na wanashirikiana watawala kuhujumu maisha ya wananchi
  6. Kujibizana na Rostam iwe sehemu ndogo isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
  7. Mhimili wa Mahakama

Hayo ni baadhi ya mengi wanayohitaji kuelimishwa wananchi kuamsha ari ya kuidai Tanzania yao
Sasa kama unamjua na mnafahamiana kwanini kwa kuokoa tu muda usingempigia Simu ili umueleze haya yote au uende kabisa Nyumbani kwake mkayamalize?
 
Mbona anaelezea hayo na zaidi, tatizo watanzania MNAPENDA sana umbea ,kujitoa kupigania nchi hamtaki

Bado wanaojitolea kuwasemea mnawapangia chakuongea
Asante maana ndo anachokiongea
Halafu wanataka kumpangia instead of wao pia waongee wanayoona hayako sawa au pole hajayaongea...

Ndio maana napenda sn Pole2, Gwajima ,mange Kila mmoja anaongea kivyake kadri anavyoona hakuna kupangiana
 
isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
Mkuu 'Msanii'. Heshima mkuu kwa maelezo yako ya kina kwa rafiki yako Polepole..

Sikutaka kunyanyua yote uliyo mshauri na kuyatolea maoni hapa. Kwa kifupi tu, Polepole ni mwanachama mtiifu sana wa chama chake cha CCM. Hili liko wazi kabisa katika mazungumzo yake.
Tatizo ni hili moja; hata CCM ikitumiwa na watu wabaya; bado wanaCCM kindakindaki, kama Polepole watabaki hawaamini kuwa chama chao kinavurugika.

Nisiende mbali. Maneno yaliyo nigusa katika maoni yako ni hayo hapo juu.
Kwa mtu yeyote anaye weka maslahi ya nchi yetu mbele; wakati huu siyo wakati wa kusambaza nguvu kwenye maeneo mengi na kudhoofisha uhitaji wa hayo uliyo yaweka hapo juu.

namsihi sana rafiki yako; aweke juhudi zake juu ya kuwaelimisha waTanzania wasishiriki uchaguzi wa kuwaweka chini ya utawala usiojali maslahi yao katika miaka mitano inayo fuata.
Hili kwa sasa ndilo jambo la dharura linalo hitaji kutekelezwa.
 
Asante maana ndo anachokiongea
Halafu wanataka kumpangia instead of wao pia waongee wanayoona hayako sawa au pole hajayaongea...

Ndoaana napenda sn Pole2, Gwajima ,mange Kilamoja anaongea kivyake kadri anavyoona hakuna kupangiana
Duh!
 
Apunguze Porojo na kujikita kwenye Concrete Issues sababu mara nyingine ni kama anataka fillers na kuongezea vitu vingine ambavyo ni vigumu ku-verify au vina chembe chembe za uzushi Case in Point issue ya bei ya Mtungi buku Mbili Cuba ilitutoa kwenye issue ya Kuwabana kwanini wanapigia chepuo gesi ambayo hatuna na ni gharama badala ya Umeme na kumaliza Bwawa..., hatujakaa sawa tunepelekwa kwenye issue za sijui nani alimpigia simu nani akiomba kuwa Waziri Mkuu (yaani vijembe); Kwa ushauri angetenga maongezi haya mara mbili kwenye maongezi ateme vitu concrete vijembe, mambo ya kusadikika n.k. ayape muda wake pia
Couldn't have said it any better!
 
Mkuu 'Msanii'. Heshima mkuu kwa maelezo yako ya kina kwa rafiki yako Polepole..

Sikutaka kunyanyua yote uliyo mshauri na kuyatolea maoni hapa. Kwa kifupi tu, Polepole ni mwanachama mtiifu sana wa chama chake cha CCM. Hili liko wazi kabisa katika mazungumzo yake.
Tatizo ni hili moja; hata CCM ikitumiwa na watu wabaya; bado wanaCCM kindakindaki, kama Polepole watabaki hawaamini kuwa chama chao kinavurugika.

Nisiende mbali. Maneno yaliyo nigusa katika maoni yako ni hayo hapo juu.
Kwa mtu yeyote anaye weka maslahi ya nchi yetu mbele; wakati huu siyo wakati wa kusambaza nguvu kwenye maeneo mengi na kudhoofisha uhitaji wa hayo uliyo yaweka hapo juu.

namsihi sana rafiki yako; aweke juhudi zake juu ya kuwaelimisha waTanzania wasishiriki uchaguzi wa kuwaweka chini ya utawala usiojali maslahi yao katika miaka mitano inayo fuata.
Hili kwa sasa ndilo jambo la dharura linalo hitaji kutekelezwa.
Mkuu nami nimeelimika sana kwenye maoni yako.

Sasa tutambue kuwa tuyachuje maneno ya wanaCCM na kuyachukua yanayotusaidia kwenye harakati hizi chanya lakini katu tusiamini kupata ukombozi wa kweli kutokea CCM
 
Haya maneno yako yamenifanya nitabasamu, nikielekea kucheka mwenyewe nilipo waza: Hivi CCM ni nani?

Nikaanza kuwapanga viongozi wote wa juu kichwani mwangu. nikakutana na akina Stephen Wasira, Emmanuel Nchimbi, na hawa vijana vijana wengi wao ambao siwajui. Hata majina ya wastaafu yakaniijia kichwani: akina Kikwete, akina Pinda, na wengineo.

Hivi kweli CCM kama chama bado ipo hai; au limebaki kuwa kundi tu la watu wanaopata maslahi yao kupitia kwenye jina lake!

Hawa wanachama milioni 13; hivi kweli wapo, na wanaamini wanacho chama cha siasa kilicho imara, bila ya mbeleko wa vyombo vya dola?

Aaah! Acha nisijaze maneno mengi kwenye mada yako nzuri.
 
NAam mkuu, safi hii thinking mimi naiunga mkono , tukiwa na mfumo imara chama chochote kiongoze tu hatutakua na shida.

Magu nayeye mimi naona wale wale wanaweka ccm mbele tu, mfano mkuu 2020. Ule uchaguzi umevurugwa na nani mtandao au magu?

Mimi Lissu naona ndo atatupa break-through. Kukumbatia umoja wa ulaya ni matokeo ya ccm kumezs mifumo ya nchi kiasi kwamba njia rahisi ni kuomba external support ,
EU siyo wajomba wale, hiyo external support haiwezi kututoa.

Ona Ukraine, nchi imeharibika, kizazi kizima kimeenda, kwa kutegemea external support. Lakini wao EU hawajali, wanaangalia maslahi yao tuu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hizo tuhuma zote au masuala unayomshauri ayafanyie kazi kama yana ukweli basi yeye alikuwemo na aliyashupalia aliokua kwenye serikali.
Maneno yake hayana ukweli au lepe la uaminifu ni mtu mwenye tamaa ya shavu tu
Polepole kaacha ubalozi. Polepole angekuwa shida yake ni shavu basi angekuwa kwenye nafasi nzuri mno ya kupewa nafasi nzuri kwa sababu Samia angetaka sana kumtumia ili kuvuta wale mashabiki wa Magufuli. meona kina Biteko wamepewa mpaka vyeo vya unaibu waziri mkuu ambavyo havipo?
 
NAam mkuu, safi hii thinking mimi naiunga mkono , tukiwa na mfumo imara chama chochote kiongoze tu hatutakua na shida.

Magu nayeye mimi naona wale wale wanaweka ccm mbele tu, mfano mkuu 2020. Ule uchaguzi umevurugwa na nani mtandao au magu?

Mimi Lissu naona ndo atatupa break-through. Kukumbatia umoja wa ulaya ni matokeo ya ccm kumezs mifumo ya nchi kiasi kwamba njia rahisi ni kuomba external support ,
Magu alikuwa na nafasi nzuri sana sana ya kutupeleka kwenye Tanzania mpya lakini akaweka chama mbele. Hakujua kuwa kwenye chama kumejaa mafisi ambao shinda yao ni maslahi binafsi. Ni kulewa madaraka. Mtu anapokuwa na madaraka akili zote hupotea na zinarudi anapoondoka.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
EU siyo wajomba wale, hiyo external support haiwezi kututoa.

Ona Ukraine, nchi imeharibika, kizazi kizima kimeenda, kwa kutegemea external support. Lakini wao EU hawajali, wanaangalia maslahi yao tuu.
Nakuunga mkono mkuu, mabadiliko tutayaleta sisi wenyewe, tukiungana wote, na ndo maana mimi nasubiri Mama aapishwe aongeze hili gari mpaka 2030. Wala hakutakua na nguvu kubws kuwashawishi wananchi tuikomhoe nchi yetu.

Tutakua tumeshapata wote lengo moja kuichomoa ccm na yeyote atakayekaa atatakiwa kuwajibika kwa wananchi
 
Polepole kaacha ubalozi. Polepole angekuwa shida yake ni shavu basi angekuwa kwenye nafasi nzuri mno ya kupewa nafasi nzuri kwa sababu Samia angetaka sana kumtumia ili kuvuta wale mashabiki wa Magufuli. meona kina Biteko wamepewa mpaka vyeo vya unaibu waziri mkuu ambavyo havipo?
Kwamba walijaribu kumfuga kumbe jamaa wa kubagaza na kubananga yeye hafugiki?

Hatari sana.

Nadhani hiyo ndiyo sifa mojawapo ya kiongozi bora - kukataa kufungiwa kwenye chupa.
 
Back
Top Bottom