Humphrey Polepole popote ulipo, nakuomba fanya hivi

Mdogo wangu Polepole heshima nyingi kwako. Kiumri ninakuzidi lakini umenizidi mengi kwenye taaluma na uzoefu. Najua unanifahamu maana tangu tukiwa wanafunzi tumefahamiana na hata ulipokuwa Mwenezi wa Mbogamboga nimeonana nawe sana pale Ofisi Ndogo Lumumba. Ingawa nilikushauri memgi ukanipinga lakini leo umekuja kufanya mengi ya baadhi niliyokushauri

Nashukuru umeweza kuunga mkono kilio na struggle ya Wapambaniaji Demokrasia nchini.

Nina ushauri hapa kwako mdogo wangu ndugu Polepole
  1. Kwenye public address zako, jikite sana kuelezea madhara yatokanayo na chaguzi mbovu. Kwa sehemu elezea matokeo kama vile Mtandao, Mafisadi nk
  2. Hitaji la Katiba mpya na manufaa yake kwa nchi
  3. CCM ilivyojipenyeza kwenye mifumo ya dola. Haitoshi tu kusema wameunga mfumo wa NIDA na NEC kudhibiti kura bali tuelezee namna CCM inavyonufaika na mifumo yetu ya ulinzi na usalama huku Watanzania wakiachwa nje
  4. Tuelezee namna CCM inavyoshirikiana na Dola kuvunja katiba na sheria za nchi.
  5. Watekaji ni kina nani na wanashirikiana watawala kuhujumu maisha ya wananchi
  6. Kujibizana na Rostam iwe sehemu ndogo isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
  7. Mhimili wa Mahakama

Hayo ni baadhi ya mengi wanayohitaji kuelimishwa wananchi kuamsha ari ya kuidai Tanzania yao
Mi nilidhani utamshauri atueleze jinsi alivyoshiriki kumdungua risasi Lissu!
Au kwenu issue ya Lissu ni so petty!?
Mshauri atueleze alivyoasisi na kushiriki biashara ya kununua wapinzani.
 
Wazo lako siyo baya pia
 
Mabadiliko akiwa kwao? Uko serious au unatania??

Hata jeshi likiasi lazima litoke likajipange vichakani unajua ni kwanini??
Polepole alipo sasa ni zaidi ya vichakani.

Leta hoja nyingine babu!
 
Kumbuka Polepole ni mwana CCM mtiifu, tatizo lake ni wana mtandao tu. Maono na dhamira yake ni CCM iendelee kutawala milele kama ilivyo CCP ya China. Kwa maana hiyo basi hawezi kuongea mambo yatakayo hatarisha utawala wa CCM.
CCP ya wachina haina unafiki kama CCM, imejitanabaisha ni chama kimoja. Tofauti na CCM inayoongoza serekali zinazoua wapinzani usiku na mchana ikiwapa ruzuku. ....... Bure kabisa.
 
Mbona anaelezea hayo na zaidi, tatizo watanzania MNAPENDA sana umbea ,kujitoa kupigania nchi hamtaki

Bado wanaojitolea kuwasemea mnawapangia chakuongea
Tunatakuka kujua mfump wa Tume huru unavyobagaza wapiga kura
 
Mdogo wangu Polepole heshima nyingi kwako. Kiumri ninakuzidi lakini umenizidi mengi kwenye taaluma na uzoefu. Najua unanifahamu maana tangu tukiwa wanafunzi tumefahamiana na hata ulipokuwa Mwenezi wa Mbogamboga nimeonana nawe sana pale Ofisi Ndogo Lumumba. Ingawa nilikushauri memgi ukanipinga lakini leo umekuja kufanya mengi ya baadhi niliyokushauri

Nashukuru umeweza kuunga mkono kilio na struggle ya Wapambaniaji Demokrasia nchini.

Nina ushauri hapa kwako mdogo wangu ndugu Polepole
  1. Kwenye public address zako, jikite sana kuelezea madhara yatokanayo na chaguzi mbovu. Kwa sehemu elezea matokeo kama vile Mtandao, Mafisadi nk
  2. Hitaji la Katiba mpya na manufaa yake kwa nchi
  3. CCM ilivyojipenyeza kwenye mifumo ya dola. Haitoshi tu kusema wameunga mfumo wa NIDA na NEC kudhibiti kura bali tuelezee namna CCM inavyonufaika na mifumo yetu ya ulinzi na usalama huku Watanzania wakiachwa nje
  4. Tuelezee namna CCM inavyoshirikiana na Dola kuvunja katiba na sheria za nchi.
  5. Watekaji ni kina nani na wanashirikiana watawala kuhujumu maisha ya wananchi
  6. Kujibizana na Rostam iwe sehemu ndogo isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
  7. Mhimili wa Mahakama

Hayo ni baadhi ya mengi wanayohitaji kuelimishwa wananchi kuamsha ari ya kuidai Tanzania yao
Uliyoyasema hawezi kufanya maana anataka kurudi CCM baada ya uchaguzi. Mtu aliahidi atatoa siri zitakazovunja chama mpaka leo anaongela mambo ambayo yashasemwa hakuna jipya.
 
Makelele mengi mnataka mabadiliko, kumbe ndio tunajua mnataka mabadiliko ndani ya ccm, ili iendelee kutawala....
 
Back
Top Bottom