Waagize na kuwaamrisha walio chini ya himaya yako.Keyboard warrior kwanini wewe usielezee yote unayotaka Polepole aelezee wakati tayari umesema kuwa anachokifanya sasa hivi wewe ndo ulimshauri?
Nimekuuliza sijakuamrisha. Uwezo wako kiakili ni mdogo sana.Waagize na kuwaamrisha walio chini ya himaya yako.
Mimi ni free soul nafanya kile nifanyacho.
Wacha tuone🤔
Oktoba hakuna uchaguzi
Sasa kama unamjua na mnafahamiana kwanini kwa kuokoa tu muda usingempigia Simu ili umueleze haya yote au uende kabisa Nyumbani kwake mkayamalize?Mdogo wangu Polepole heshima nyingi kwako. Kiumri ninakuzidi lakini umenizidi mengi kwenye taaluma na uzoefu. Najua unanifahamu maana tangu tukiwa wanafunzi tumefahamiana na hata ulipokuwa Mwenezi wa Mbogamboga nimeonana nawe sana pale Ofisi Ndogo Lumumba. Ingawa nilikushauri memgi ukanipinga lakini leo umekuja kufanya mengi ya baadhi niliyokushauri
Nashukuru umeweza kuunga mkono kilio na struggle ya Wapambaniaji Demokrasia nchini.
Nina ushauri hapa kwako mdogo wangu ndugu Polepole
- Kwenye public address zako, jikite sana kuelezea madhara yatokanayo na chaguzi mbovu. Kwa sehemu elezea matokeo kama vile Mtandao, Mafisadi nk
- Hitaji la Katiba mpya na manufaa yake kwa nchi
- CCM ilivyojipenyeza kwenye mifumo ya dola. Haitoshi tu kusema wameunga mfumo wa NIDA na NEC kudhibiti kura bali tuelezee namna CCM inavyonufaika na mifumo yetu ya ulinzi na usalama huku Watanzania wakiachwa nje
- Tuelezee namna CCM inavyoshirikiana na Dola kuvunja katiba na sheria za nchi.
- Watekaji ni kina nani na wanashirikiana watawala kuhujumu maisha ya wananchi
- Kujibizana na Rostam iwe sehemu ndogo isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
- Mhimili wa Mahakama
Hayo ni baadhi ya mengi wanayohitaji kuelimishwa wananchi kuamsha ari ya kuidai Tanzania yao
Asante maana ndo anachokiongeaMbona anaelezea hayo na zaidi, tatizo watanzania MNAPENDA sana umbea ,kujitoa kupigania nchi hamtaki
Bado wanaojitolea kuwasemea mnawapangia chakuongea
Mkuu 'Msanii'. Heshima mkuu kwa maelezo yako ya kina kwa rafiki yako Polepole..isikudistract kwenye kuelimisha Watanzania wasishiriki uchaguzi
Duh!Asante maana ndo anachokiongea
Halafu wanataka kumpangia instead of wao pia waongee wanayoona hayako sawa au pole hajayaongea...
Ndoaana napenda sn Pole2, Gwajima ,mange Kilamoja anaongea kivyake kadri anavyoona hakuna kupangiana
Couldn't have said it any better!Apunguze Porojo na kujikita kwenye Concrete Issues sababu mara nyingine ni kama anataka fillers na kuongezea vitu vingine ambavyo ni vigumu ku-verify au vina chembe chembe za uzushi Case in Point issue ya bei ya Mtungi buku Mbili Cuba ilitutoa kwenye issue ya Kuwabana kwanini wanapigia chepuo gesi ambayo hatuna na ni gharama badala ya Umeme na kumaliza Bwawa..., hatujakaa sawa tunepelekwa kwenye issue za sijui nani alimpigia simu nani akiomba kuwa Waziri Mkuu (yaani vijembe); Kwa ushauri angetenga maongezi haya mara mbili kwenye maongezi ateme vitu concrete vijembe, mambo ya kusadikika n.k. ayape muda wake pia
Mkuu nami nimeelimika sana kwenye maoni yako.Mkuu 'Msanii'. Heshima mkuu kwa maelezo yako ya kina kwa rafiki yako Polepole..
Sikutaka kunyanyua yote uliyo mshauri na kuyatolea maoni hapa. Kwa kifupi tu, Polepole ni mwanachama mtiifu sana wa chama chake cha CCM. Hili liko wazi kabisa katika mazungumzo yake.
Tatizo ni hili moja; hata CCM ikitumiwa na watu wabaya; bado wanaCCM kindakindaki, kama Polepole watabaki hawaamini kuwa chama chao kinavurugika.
Nisiende mbali. Maneno yaliyo nigusa katika maoni yako ni hayo hapo juu.
Kwa mtu yeyote anaye weka maslahi ya nchi yetu mbele; wakati huu siyo wakati wa kusambaza nguvu kwenye maeneo mengi na kudhoofisha uhitaji wa hayo uliyo yaweka hapo juu.
namsihi sana rafiki yako; aweke juhudi zake juu ya kuwaelimisha waTanzania wasishiriki uchaguzi wa kuwaweka chini ya utawala usiojali maslahi yao katika miaka mitano inayo fuata.
Hili kwa sasa ndilo jambo la dharura linalo hitaji kutekelezwa.
Mkuu yeye anamshauri tu.Unampangia cha kuongea we kama nani
Haya maneno yako yamenifanya nitabasamu, nikielekea kucheka mwenyewe nilipo waza: Hivi CCM ni nani?Mkuu nami nimeelimika sana kwenye maoni yako.
Sasa tutambue kuwa tuyachuje maneno ya wanaCCM na kuyachukua yanayotusaidia kwenye harakati hizi chanya lakini katu tusiamini kupata ukombozi wa kweli kutokea CCM
EU siyo wajomba wale, hiyo external support haiwezi kututoa.NAam mkuu, safi hii thinking mimi naiunga mkono , tukiwa na mfumo imara chama chochote kiongoze tu hatutakua na shida.
Magu nayeye mimi naona wale wale wanaweka ccm mbele tu, mfano mkuu 2020. Ule uchaguzi umevurugwa na nani mtandao au magu?
Mimi Lissu naona ndo atatupa break-through. Kukumbatia umoja wa ulaya ni matokeo ya ccm kumezs mifumo ya nchi kiasi kwamba njia rahisi ni kuomba external support ,
Polepole kaacha ubalozi. Polepole angekuwa shida yake ni shavu basi angekuwa kwenye nafasi nzuri mno ya kupewa nafasi nzuri kwa sababu Samia angetaka sana kumtumia ili kuvuta wale mashabiki wa Magufuli. meona kina Biteko wamepewa mpaka vyeo vya unaibu waziri mkuu ambavyo havipo?Hizo tuhuma zote au masuala unayomshauri ayafanyie kazi kama yana ukweli basi yeye alikuwemo na aliyashupalia aliokua kwenye serikali.
Maneno yake hayana ukweli au lepe la uaminifu ni mtu mwenye tamaa ya shavu tu
Magu alikuwa na nafasi nzuri sana sana ya kutupeleka kwenye Tanzania mpya lakini akaweka chama mbele. Hakujua kuwa kwenye chama kumejaa mafisi ambao shinda yao ni maslahi binafsi. Ni kulewa madaraka. Mtu anapokuwa na madaraka akili zote hupotea na zinarudi anapoondoka.NAam mkuu, safi hii thinking mimi naiunga mkono , tukiwa na mfumo imara chama chochote kiongoze tu hatutakua na shida.
Magu nayeye mimi naona wale wale wanaweka ccm mbele tu, mfano mkuu 2020. Ule uchaguzi umevurugwa na nani mtandao au magu?
Mimi Lissu naona ndo atatupa break-through. Kukumbatia umoja wa ulaya ni matokeo ya ccm kumezs mifumo ya nchi kiasi kwamba njia rahisi ni kuomba external support ,
Nakuunga mkono mkuu, mabadiliko tutayaleta sisi wenyewe, tukiungana wote, na ndo maana mimi nasubiri Mama aapishwe aongeze hili gari mpaka 2030. Wala hakutakua na nguvu kubws kuwashawishi wananchi tuikomhoe nchi yetu.EU siyo wajomba wale, hiyo external support haiwezi kututoa.
Ona Ukraine, nchi imeharibika, kizazi kizima kimeenda, kwa kutegemea external support. Lakini wao EU hawajali, wanaangalia maslahi yao tuu.
Kwamba walijaribu kumfuga kumbe jamaa wa kubagaza na kubananga yeye hafugiki?Polepole kaacha ubalozi. Polepole angekuwa shida yake ni shavu basi angekuwa kwenye nafasi nzuri mno ya kupewa nafasi nzuri kwa sababu Samia angetaka sana kumtumia ili kuvuta wale mashabiki wa Magufuli. meona kina Biteko wamepewa mpaka vyeo vya unaibu waziri mkuu ambavyo havipo?