Humphrey Polepole popote ulipo, nakuomba fanya hivi

Naam wanakilinda sana chama, hali ya kuwa kimeshaleta madhara mengi sana kwenye mifumo
 
Unabariki huu uchaguzi feki?
 
Kwamba walijaribu kumfuga kumbe jamaa wa kubagaza na kubananga yeye hafugiki?

Hatari sana.

Nadhani hiyo ndiyo sifa mojawapo ya kiongozi bora - kukataa kufungiwa kwenye chupa.
Waliomshauri Samia kumpeleka jamaa Cuba walichemsha. Wao walidhani kumpeleka mbali ni kumkomoa, kumbe kule ndiyo kaenda kupigwa msasa wa kimapinduzi.
 
Well
Ushauri mzuri
 
Polepole kwa sasa aeleweka uzuri tu.

Hata Youtube kwa kuzingatia namba ya wafuatiliaji, wameamua kutokata video zake kwa matangazo wao waweka matangazo huku Polepole akiendelea na mjadala.

Kwa maana ingine hii ni shule ya Uongozi imekuja kivingine.

Tuendelee kuelimishana.
 
Mambo ya muhimu kabisa hayo ntamkumbusha akiingia live pale kwenye comments section
 
Unabariki huu uchaguzi feki?
Hapana mkuu, ila hakuna mbinu za kuzuia kwa sasa, huyu akipata mi5 tena watanzania ndo tutafungua akili na kuwa na umoja
 
Tatizo la HP bado yeye ni mwana CCM na hataki itoke madarakani. Lakini anataka irekebishwe mafisadi waondoke ili waendelee wao waadilifu bila kujua veggies yote imeoza inatakiwa matawi yakatwe mpaka mzizi wa mti ndio pona ya shamba..!!
 
Tatizo la HP bado yeye ni mwana CCM na hataki itoke madarakani. Lakini anataka irekebishwe mafisadi waondoke ili waendelee wao waadilifu bila kujua veggies yote imeoza inatakiwa matawi yakatwe mpaka mzizi wa mti ndio pona ya shamba..!!
Kuna ubaya akibaki CCM ilimradi mambo yote yakae sawa?

Au umesimuliwa tu kuhusu maongezi yake? Umemwelewa kweli?
 
Ni kosa kusafiri kwa chombo kinachomilikiwa kihalali na Mboga2?
Tena kosa kubwa, chombo chenye harufu ya damu unatakiwa ukiogope..!!
Ndiomana kabila letu ukipata ajali na gari lako mwiko kulitumia tena, coz lina historia mbaya na wewe..!!
 
Nadhani hujamfatilia Polepole tokea mwanzo au kama unamfatilia basi humalizi katika yale anayoyaeleza, yote unayomshauri alishayasema na kuhusu Rostam hatajibizana naye tena ameshasema hilo, kuanzia wiki ijayo ataanza na afya na jinsi mifumo ya bima ya afya ilivyo ya kihuni lakini pia amesema atazungumzia kuhusu Bandari na mikataba mibovu iliyosainiwa.

Kwahiyo usikae mbali na akaunti zake ili upate faida zaidi na ikibidi uungane naye katika kupambania haki za wanyonge badala ya kukaa pembeni nakusubiri majaliwa au huruma ya CCM
 
Tena kosa kubwa, chombo chenye harufu ya damu unatakiwa ukiogope..!!
Ndiomana kabila letu ukipata ajali na gari lako mwiko kulitumia tena, coz lina historia mbaya na wewe..!!
Unahisi CCM wote ni wabaya na kwamba sera yake ni mbaya 100%?

Tuseme CCM imesambaratika kabisa, halafu hao watu wakahamia CDM, italeta tofauti yoyote?
 
Kweli kabisa, na sijui hata tunamwamini nini huyu mwehu maana inaonekana tu miguu yake yote miwili bado imo ndani ya ccm
 
Unahisi CCM wote ni wabaya na kwamba sera yake ni mbaya 100%?

Tuseme CCM imesambaratika kabisa, halafu hao watu wakahamia CDM, italeta tofauti yoyote?
Veggies yote imeoza, km ni wema kwanini wako kimya? Wote wanaangalia maslahi yao ndiomana HP naye hasemi kuhusu kuikataa mbogamboga..!!

Ikisambaratika kuna marekebisho yatafanyika na hata wakihamia chama kingine au wakirudi kupitia chama chao kuna fundisho watakuwa wamelipata..!!

Hiyo itawatia uoga watajua tukifanya ndivyo sivyo tutakipata cha mtema kuni..!!
 
Kusambaratika ndilo neno hasa alilotumia Polepole.

Bila shaka unamsapoti bila kujua.

Umesema "au wakirudi kupitia chama chao."

Awali nimekuuliza kuna ubaya gani jamaa akipigania mabadiliko akiwa huko kwao, ilimradi mabadiliko ni ya kweli?

Ni wazi hujui unalozungumzia au mko wawili mawazoni mwako.
 
Umeona vizuri sana mkuu.

Nakuunga mkono 100%
 
Mabadiliko akiwa kwao? Uko serious au unatania??

Hata jeshi likiasi lazima litoke likajipange vichakani unajua ni kwanini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…