Hayo ni maneno yaliyotamkwa na Katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole, kwenye mdahalo kuhusiana na Katiba mpya ya nchi iliyokuwa ikiitwa Rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba.
Hapo ilikuwa ni "flashback" Desemba ya mwaka 2017.
Polepole wa Leo siyo tena yule wa mwaka 2017 na hata ukimwambia kuwa ni wewe ulitamka maneno hayo, ataruka maili 1000, kukanusha maneno hayo, kuwa hayajatoka kinywani mwake!
Huo ni mkweli mchungu, ambao Humphrey Polepole aliamua kuusema, wakati huo bado hajavalishwa, hizo sare za kijani, za ukatibbu wa itikadi na uenezi wa CCM Taifa.