Huna Wajibu wa kumtunza au kumhudumia Mzazi wako akiwa chini ya miaka 60 kama haumwi

Hiyo ndio HAKI
 
😂😂😂 Tatizo babu mliwatafuta watoto km kina mtibeli mkiwa maji
 
Ubinafsi ndio umaskini wa waafrika wengi.
 
😂😂😂 Tatizo babu mliwatafuta watoto km kina mtibeli mkiwa maji
Hahaha...............wakati mwingine stimu zinakuwa high ukiwa Maji....Kila ukijaribu kutofikiria unajikuta mnara bado upo hewani tu

Kuja kutahamaki mechi heavy ya saa 8 usiku

Ndiyo hapo tunawapata akina Mtibeli

Bora tumezeeka sasa 😜
 
☹️ 😞😞

Kwa namna hii mzazi akiwa na Mali mtoto atawaza nimuondoe Baba Ili nirithi...

Ivi ni vipi kama ungezaliwa mlemavu wa kusaidiwa kulishwa mzigo kiasi Gani wangeubeba Wazazi wako na hatujui ungekufa Mzee sana?

Robert tafuta msaada wa viongozi wa kiroho haraka kuna jambo haliko sawa...
 
Nazungumzia Haki na wajibu Mkuu.
Waafrika wengi tunatatizo la kutotenda Haki na wajibu wetu.

Mtu akiwa mgonjwa hiyo inafahamika nini kinatakiwa kufanywa.
 
Waambie vijana wa hovyo ndio watakuelewa mzazi wangu hata angekua na miaka 10 ningemsaidia ukitanguliza upendo hakuna uyakaloona kikwazo ila ukiweka hisia mbele mzazi utamuona kama paka tu
 
Waambie vijana wa hovyo ndio watakuelewa mzazi wangu hata angekua na miaka 10 ningemsaidia ukitanguliza upendo hakuna uyakaloona kikwazo ila ukiweka hisia mbele mzazi utamuona kama paka tu

Hakuna upendo wa hivyo.
Waafrika na upendo wapi kwa wapi
 
Huu uzi unachekesha, wanavyokushambulia mtibeli na ww unavyopangua mashuti 😂😂
 
Huu uzi unachekesha, wanavyokushambulia mtibeli na ww unavyopangua mashuti 😂😂

Hawa hawanaga hoja. Walishashindwa mambo mengi mno. Babu zao walishindwa na leo watoto wao ndio hawahawa ambao watashindwa tena.
Ni kizazi kilichoshindwa. Kwa sababu kuwekeza kwenye Past badala ya future.
 
Nazungumzia Haki na wajibu Mkuu.
Waafrika wengi tunatatizo la kutotenda Haki na wajibu wetu.

Mtu akiwa mgonjwa hiyo inafahamika nini kinatakiwa kufanywa.
Haki ni Upendo na Upendo ni Haki.

Ama hatukubaliani?

Sasa unawezaje kuvumilia huzuni ya mtu unayempenda(mzazi), na ikiwa unao uwezo wa kumpa furaha?

Kigezo ni umri?
 
Mzazi kumuhudumia mtoto chini ya miaka 20 ni wajibu...
Mtoto kumuhudumia mzazi ni hisani.
Na ndio maana mzazi usipomuhudumi mtoto unaweza shtakiwa.
Ila si mtoto atashtakiwa hamtunzi mzazi.
Tuwasaidie wazazi kadli tuwezavyo. Ila wazazi tusiwatweshe majukumu vijana wanaojitafuta na hawajasimama bado.
 
Hakuna upendo wa hivyo.
Waafrika na upendo wapi kwa wapi
Usilazimishe mkuu kama hupendi wazazi wako ni ww mm najua walivyonipambania na kunipenda hivyo sioni shida kuwapenda kama wakwako walikosa kipato na ww ukashindwa kuona namna gani wamepambana pole sana maana unajijengea msingi wa laana duniani
 
Pole mkuu ama kweli vichwa vya watu vimejaa
 
Usilazimishe mkuu kama hupendi wazazi wako ni ww mm najua walivyonipambania na kunipenda hivyo sioni shida kuwapenda kama wakwako walikosa kipato na ww ukashindwa kuona namna gani wamepambana pole sana maana unajijengea msingi wa laana duniani

Huwezi kubarikiwa kwa hiyari yako. Mtu anabarikiwa kwa wajibu kwa kutekeleza yanayompasa.
Kukupambania ni wajibu wao.
Na wewe unawajibu wa kuwapambania muda sahihi ukifika yaani wakiwa wazee.

Ndio maana kadiri ulivyokuwa unakua mkubwa ndivyo walivyokuwa wanakuacha na wajibu wao kwako ulikuwa unapungua ikiwemo kukutafutia chakula, mavazi na malazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…