Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Fainali uzeeni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
TOTO HASARA MAJUTO KWA MZAZI!!!
Wazazi wengi wa kiafrika wanazaa watoto wengi ili wakishakuwa wakubwa waje kuwafanya watumwa nao wazazi wabaki kuwa mabwana wanaotumikiwa na watoto wao(hizi ni fikra za kimaskini na ufukara wa kutupwa); toka nimeligundua hilo na hali ya dunia iliyopo sasa nimejiapiza nitazaa watoto wachache hawatazidi wawili, ili nipate nafasi ya kujiimarisha kiuchumi na wao wakiwa wakubwa waendelee na maisha yao bila mimi kuwasumbua. am done.
Fainali uzeeni
😂😂😂 Tatizo babu mliwatafuta watoto km kina mtibeli mkiwa majiKama watoto wenyewe ndiyo hawa akina Mtibeli alafu ndiyo tuwategemee waje watusitiri tukizeeka tuhesabu maumivu tu Wazee wenzangu.
Ndiyo maana nimefungua akaunti yangu ya Siri, najiwekea hela zangu ili kuepusha aibu ya kudharilishwa na Watoto tunaotegemea watupe Faraja Uzeeni.
Kama nitakufa mapema bora wale watu wa Benki tu 🥲
Ubinafsi ndio umaskini wa waafrika wengi.Mtoa mada katumia akili nyingi sana huenda ni Uzi mzuri zaidi ktk hii wiki.
Wachangiaji wengi hawana critical thinking na wanakurupuka kumkosoa mtoa mada bila kuwaza mara mbilimbili na kufanya analysis.
Binafsi nitashare experience yangu:
Baada ya kupata kazi tu.. nikaanza kujumuishwa ktk ishu za familia hasa kulipia ADA wadogo zangu (Hapo mwanzo walikuwa wanalipiwa na Wazazi na Shule waliyosoma wao ni ghali sana na wapo watatu) haya nikawa najibana nalipa angalau nusu ya ada kwa wote watatu.
Ikumbukwe mimi nimesoma shule ya kidumu na mfagio na wazee walikuwa nauwezo wa kunisomesha ktk mabas ya njano ila wakanitupa huko.
Wananyumba huwa wamepangisha na wanakusanya kodi kila mwisho wa mwezi, kama mtoto ktk swala la mgao wala sijawahi kupata hata mia.. na wakikusanya maokoto hata taarifa hupati ila ww utapata taarifa za majanga tu kuna hiki kimeharibika kuna kile kinataka hela etc.. ila.maswala positive hutosikia taarifa achilia mbali mgao (siutaki mgao wenyewe).
Haya ilifikia muda nataka kuoa, wakaniwekea ngumu nisioe (akili yangu ikawa imejiongeza na kujua nini sababu ya wao kunikataza kuoa wakisema ni mapema kwamba nina umri mdg hapo nina 28), jambo ambalo wao walikuwa hawataki ni mm kuwa na majukumu na familia yangu ntakayoanzisha hivyo sitaendelea kuwapa hivyo vihela vya hapa na pale..
Familia za kimaskini ukiziendekeza hupigi hatua sana sana unabaki palepale kila siku.. mshahara unaingia unapitiliza kusolve ishu zao sometimes ubinafsi unasaidia sana kupata maendeleo.
Wazazi wawaache wototo wajiimarishe kiuchumi ndio wafaidike na sio mtu kajipata kdg tu tyr majukumu mnamjazia hapo hata kujiweka sawa bado na mnaenda mbali kumzuia ishu za msingi kbs kama kuanzisha familia yake ili muendelee kula hela zake kwa uhuru..
Kwani nan kasema nikiwa na familia yangu sitawasaidia? Mawazo ya kimaskini sana..
Hahaha...............wakati mwingine stimu zinakuwa high ukiwa Maji....Kila ukijaribu kutofikiria unajikuta mnara bado upo hewani tu😂😂😂 Tatizo babu mliwatafuta watoto km kina mtibeli mkiwa maji
Pole yao wanaopata pressure ya kusaidia wazazi, kuna baadhi ya wazazi wanazaa ili mtoto aje kuwasaidia
☹️ 😞😞
Kwa namna hii mzazi akiwa na Mali mtoto atawaza nimuondoe Baba Ili nirithi...
Ivi ni vipi kama ungezaliwa mlemavu wa kusaidiwa kulishwa mzigo kiasi Gani wangeubeba Wazazi wako na hatujui ungekufa Mzee sana?
Robert tafuta msaada wa viongozi wa kiroho haraka kuna jambo haliko sawa...
Waambie vijana wa hovyo ndio watakuelewa mzazi wangu hata angekua na miaka 10 ningemsaidia ukitanguliza upendo hakuna uyakaloona kikwazo ila ukiweka hisia mbele mzazi utamuona kama paka tuHUNA WAJIBU WA KUMTUNZA AU KUMHUDUMIA MZAZI WAKO AKIWA CHINI YA MIAKA 60 KAMA HAUMWI.
Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Mada hii inaweza kuwa ngumu kwa baadhi ya Watu. Lakini nitakachojadili hapa ni Haki, kweli, akili na upendo kama ilivyo kwa Watibeli wote.
Kama ilivyo kwa mzazi hana wajibu wa kukutunza na kukuhudumia pindi ufikishapo umri wa kujitegemea yaani kuanzia miaka 21 hivi kwa sisi Watibeli. Na kwa sheria za dunia ni miaka 18. Basi ndivyo hivyohivyo kuwa mtoto hana wajibu wa kumtunza na kumhudumia mzazi au mlezi ambaye yupo chini ya miaka 60 ambaye HAUMWI(hana tatizo la kiafya).
Kuna kijitabia fulani cha kinyonyaji, dhulma, uvivu, na ukandamizaji ambao unafanywa na wazazi kwenda kwa watoto wao. Ambapo mzazi anazaa watoto idadi fulani anawapa na kuwatunza(wajibu wake) alafu wakishafikisha miaka 20 tuu wakaenda kujitafutia basi inakuwa nongwa. Mzazi hata miaka 50 haujui, miaka 60 ndio kabisa hatarajii leo wala kesho kuifikia. Mzazi ananguvu kabisa lakini kutwa kusumbua watoto na kuwatia watoto katika shinikizo isivyostahili.
Sio jukumu la mtoto kukulea na kukutunza ukiwa na umri huo. Wewe bado upo umri wa kujitegemea na kujihudumia. Kwa nini umpe mtoto mzigo? Kwa nini umdhulumu mtoto haki zake?
Kama sababu ni kuzaa na kumtunza hata yeye atazaa na kutunza watoto wake.
Kama ishu ni wajibu basi subiri muda ukifika mtoto atekeleze wajibu wake. Na kama atakutunza au kukuhudumia iwe kwa uwezo na mapenzi yake kwako na shukran na sio shinikizo.
Ni laana kubwa kumhudumia mtu isivyo halali. Kuhudumia mzazi kwa kushinikizwa yaani kunyonywa na kudhulumiwa ni laana ambayo wengi inawatafuna.
Sio ajabu unakuta Watu wengi tangu wakiwa vîjana wanateseka kuhudumia wazazi isivyostahili wakifikiria ndio baraka lakini miaka inaenda maisha yao hayabadiliki zaidi ya kuzidi kuwa maskini na fukara zaidi.
Ni sawasawa na mzazi amuone mtoto keshafikia umri wa kujitegemea alafu bado awe anamhudumia na kumtunza huo ni umaskini wa akili na roho. Lazima kizazi hiki kiwe fukara.
Ninajua ndoa nyingi zilizoharibika na familia nyingi kuanguka kisa wazazi kushinikiza huduma. Ni laana tupu. Wakati huo wazazi wananguvu kabisa.
Ninajua mabinti wengi wanaoteseka kwenye ndoa kisa wazazi wao wamewashinikiza watoto wao wabaki kwenye mateso ili wao wanufaike au walishanufaika na kumuuza binti yao.
Wengine huwashinikiza binti zao waolewe na wanaume wenyewe pesa hata kama hawapendwi na binti zao kwa kulenga kuhudumiwa na pesa za mkwilima wao.
Wapo vibinti vya kazi za ndani wanalipwa mishahara kiduntu kama elfu 30 mpaka 60 na bado wazazi wanataka gawiwo licha ya kuwa wazazi hao bado kiumri wanauwezo wa kufanya kazi na kujitafutia.
Wapo wazazi kiumri ni wadogo lakini wanawakosea watoto wao haki kwa kuwashinikiza watoto wao kwa matusi na kejeli kuwa hawafanyi kazi huko mjini kisa tuu hawatumiwi pesa. Jambo ambalo sio Haki na sio Upendo.
Wapo watoto wanajitutumua kuhakikisha wanahudumia wazazi wao kiugumuugumu, kwa kujikamua, na malalamiko ya nafsi wazazi kwa ubinafsi wao huona ni sahihi lakini sio sahihi kabisa.
Acheni watoto wakiwa na umri wa kujitafutia watafute na kujitegemea alafu wao kwa roho ya upendo wawatumie kwa hiyari yao na sio kuwadhulumu maisha na nguvu zao.
Watoto pia, acheni kudhulumu nguvu za wazazi wenu huku mkujua kuwa tayari mmefikia umri wa kujitegemea na sio kuwapa wazazi wenu mzigo, kuwanyonya na kuwakatili.
Mzazi asifurahie utu uzima wake aanze kukufikiria mtu mzima na ndevu zako kisa ati ni mtoto wake. Hiyo sio HAKI
Kumhudumia mzazi wako aliyemzee sio hiyari yako wala sio mapenzi yako kwake. Hiyo ni lazima, wajibu.
Bahati nzuri wazee hawana mahitaji mengi kama ilivyo kwa watoto.
Lakini kuhudumia mzazi aliyechini ya miaka 60 na haumwi hiyo ni hiyari na mapenzi tuu na sio lazima/wajibu. Unaweza ukafanya au usifanye na hakuna lolote litakupata.
Kumhudumia mtu anayeweza kujitegemea ni laana na kurudisha nyuma kizazi na ukoo wenu.
Lazima Watu wafanyekazi na wawajibike kwa maisha yao na ya wale wanaowahusu.
Huo ndio Utibeli. Ukweli, haki, upendo na Haki
Mimi nimemaliza, mwenye maswali anaweza kuuliza.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Waambie vijana wa hovyo ndio watakuelewa mzazi wangu hata angekua na miaka 10 ningemsaidia ukitanguliza upendo hakuna uyakaloona kikwazo ila ukiweka hisia mbele mzazi utamuona kama paka tu
Huu uzi unachekesha, wanavyokushambulia mtibeli na ww unavyopangua mashuti 😂😂
Haki ni Upendo na Upendo ni Haki.Nazungumzia Haki na wajibu Mkuu.
Waafrika wengi tunatatizo la kutotenda Haki na wajibu wetu.
Mtu akiwa mgonjwa hiyo inafahamika nini kinatakiwa kufanywa.
Usilazimishe mkuu kama hupendi wazazi wako ni ww mm najua walivyonipambania na kunipenda hivyo sioni shida kuwapenda kama wakwako walikosa kipato na ww ukashindwa kuona namna gani wamepambana pole sana maana unajijengea msingi wa laana dunianiHakuna upendo wa hivyo.
Waafrika na upendo wapi kwa wapi
Mtoa mada katumia akili nyingi sana huenda ni Uzi mzuri zaidi ktk hii wiki.
Wachangiaji wengi hawana critical thinking na wanakurupuka kumkosoa mtoa mada bila kuwaza mara mbilimbili na kufanya analysis.
Binafsi nitashare experience yangu:
Baada ya kupata kazi tu.. nikaanza kujumuishwa ktk ishu za familia hasa kulipia ADA wadogo zangu (Hapo mwanzo walikuwa wanalipiwa na Wazazi na Shule waliyosoma wao ni ghali sana na wapo watatu) haya nikawa najibana nalipa angalau nusu ya ada kwa wote watatu.
Ikumbukwe mimi nimesoma shule ya kidumu na mfagio na wazee walikuwa nauwezo wa kunisomesha ktk mabas ya njano ila wakanitupa huko.
Wananyumba huwa wamepangisha na wanakusanya kodi kila mwisho wa mwezi, kama mtoto ktk swala la mgao wala sijawahi kupata hata mia.. na wakikusanya maokoto hata taarifa hupati ila ww utapata taarifa za majanga tu kuna hiki kimeharibika kuna kile kinataka hela etc.. ila.maswala positive hutosikia taarifa achilia mbali mgao (siutaki mgao wenyewe).
Haya ilifikia muda nataka kuoa, wakaniwekea ngumu nisioe (akili yangu ikawa imejiongeza na kujua nini sababu ya wao kunikataza kuoa wakisema ni mapema kwamba nina umri mdg hapo nina 28), jambo ambalo wao walikuwa hawataki ni mm kuwa na majukumu na familia yangu ntakayoanzisha hivyo sitaendelea kuwapa hivyo vihela vya hapa na pale..
Familia za kimaskini ukiziendekeza hupigi hatua sana sana unabaki palepale kila siku.. mshahara unaingia unapitiliza kusolve ishu zao sometimes ubinafsi unasaidia sana kupata maendeleo.
Wazazi wawaache wototo wajiimarishe kiuchumi ndio wafaidike na sio mtu kajipata kdg tu tyr majukumu mnamjazia hapo hata kujiweka sawa bado na mnaenda mbali kumzuia ishu za msingi kbs kama kuanzisha familia yake ili muendelee kula hela zake kwa uhuru..
Kwani nan kasema nikiwa na familia yangu sitawasaidia? Mawazo ya kimaskini sana..
Usilazimishe mkuu kama hupendi wazazi wako ni ww mm najua walivyonipambania na kunipenda hivyo sioni shida kuwapenda kama wakwako walikosa kipato na ww ukashindwa kuona namna gani wamepambana pole sana maana unajijengea msingi wa laana duniani