Aliyekuwa Gwiji wa utakatishaji fedha aliyejipatia umaarufu mitandaoni hasa Instagram, anayejulikana Kwa jina la Hushpuppi amefunguliwa mashtaka mapya na waendesha mashitaka wa Marekani wakimtuhumu kufanya ulaghai na kutakatisha zaidi ya dola za marekani 400,000 (zaidi ya Tsh Milioni 900) akiwa gerezani.
- Tunachokijua
- Ramon Olorunwa Abbas alizaliwa 11 Oktoba 11, 1982 nchini Nigeria, anajulikana kama Hushpuppi , Hush, au Ray Hushpuppi, ni mshawishi wa zamani wa Instagram na mhalifu aliyepatikana na hatia.
Hadi alipokamatwa na Polisi wa Dubai mnamo Juni 2020 na kupelekwa Marekani baadaye, Abbas alichapisha picha na video za matumizi yake ya kifahari kwenye magari ya kigeni, saa, nguo za wabunifu, mifuko kutoka chapa za bei ghali kama vile Gucci, Fendi, na Louis Vuitton na yeye mwenyewe kupanda helikopta, pamoja na watu mashuhuri, wanasoka, na wanasiasa wa Nigeria au wakiwa kwenye ndege za kukodi.
Usiku ambao nyumba yake huko Palazzo Versace ilivamiwa katika operesheni iliyopewa jina la Fox Hunt 2, Abbas alikamatwa pamoja na watu wengine kumi na moja katika uvamizi sita kwa wakati mmoja. Maafisa wa upelelezi walinasa pesa taslimu zaidi ya dirham milioni 150 (takriban dola milioni 40), magari 13 ya kifahari yenye thamani ya Dh 25 milioni ($7M), kompyuta mpakato 21, simu janja 47, vifaa 15 vya kuhifadhia kumbukumbu, diski kuu tano za nje na barua pepe 800,000 za waathiriwa kando ya masanduku kamili ya fedha.
Kukamatwa kwake ilikuwa sehemu ya uchunguzi wa FBI ambao ulimshtaki kama "mhusika mkuu" katika mtandao wa kimataifa wa uhalifu wa mtandao ambao ulitoa "mahali salama kwa pesa zilizoibiwa duniani kote."
Ukweli wa tukio la kutapeli akiwa gerezani
Machi 17, 2023, habari za Mwanamtandao anayefahamika kwa jina la Hashpuppi zilianza kusambaa mtandaoni zikidai kuwa amefanya tena utapeli wa zaidi ya Tsh. Bilioni 900 nchini Marekani akiwa gerezani.
Nyaraka za mahakama zilizowekwa wazi zinaonesha katika tukio moja, Hashpuppi alijaribu kumtapeli dola milioni 1 za Marekani (zaidi ya Tsh. bilioni 2.3) mtu mmoja aliyetaka kufadhili shule moja ya watoto nchini Qatar baada ya kujifanya benki kwa kuonesha nyaraka feki na kutengeneza tovuti feki.
Pamoja na kuwa na sifa za kipekee za utapeki, Serikali ya Marekani imetupilia mbali madai kwamba mshawishi raia wa Nigeria aliyezuiliwa Ramon Abbas, anayejulikana kama Hushpuppi, alitekeleza ulaghai wa mtandao wa $400,000 (£304,000) kutoka gerezani.
Hati hii iliyoibuka kwenye mitandao ya kijamii ilidai kuwa FBI iliwasilisha ushahidi mpya dhidi ya Hushpuppi ilimtuhumu kwa kuwalaghai Wamarekani kwa kutumia mitambo ya mtandao wa gereza. Haijulikani hati hiyo ilitoka wapi lakini imeenea kwenye Mitandao na kuripotiwa na mashirika mengi ya habari.
Hata hivyo, afisa wa Idara ya Sheria ya Marekani anasema Ofisi ya Mwanasheria wa Marekani mjini Los Angeles, ambayo ilifungua kesi dhidi ya Hushpuppi, haijawasilisha hati yoyote kama hiyo.
"Waraka huo unaonekana kuwa wa kubuni. Tumewasiliana na FBI ambao inadaiwa waliandika hati hiyo, na wanathibitisha kuwa ni ya uongo" afisa mmoja alisema.
Mamlaka ya Marekani, aliongeza wafungwa wana ufikiaji mdogo wa simu, video, mtandao na matumizi ya kompyuta kwa sababu ya haki yao ya faragha katika kufungua mahakamani.
Ramon Olorunwa Abbas (Hushpuppi) akiwa pembeni ya mojawapo ya magari yake ya kifahari kabla ya kukamatwaKama wafungwa wengine, Hushpuppi alipewa ufikiaji wa mtandao wa kompyuta, kulingana na mamlaka. Hushpuppi anajulikana kwa kuweka picha za maisha yake ya kifahari kwenye Instagram, ambapo hadi anakamatwa alikuwa na wafuasi milioni 2.5. Katika mpango mmoja, Hushpuppi alijaribu kuiba zaidi ya $1.1m kutoka kwa mtu ambaye alitaka kufadhili shule mpya ya watoto nchini Qatar, nyaraka za mahakama zilisema.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka nchini Marekeni, kama ilivyochapishwa Novemba 7, 2022, Hushpuppi alihukumiwa kifungo cha miaka 11 jela baada ya kupatikana na hatia ya makosa aliyokuwa anatuhumiwa nayo.
JamiiForums imebaini kuwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni zikimhusisha Hushpuppi na utapeli wa zaidi ta Tsh. Bilioni 900 hazina ukweli.