Hussein Bashe acha kufokea na kutishia raia walipa kodi kwa sababu ya kutopendezwa na ukosoaji wao

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Bashe fanya kazi yako na timiza wajibu wako, unalipwa kuleta masuluhisho katika sekta ya kilimo. Acha kufokea raia kwamba watu wanakosoa tu bila kuletea masuluhisho kwa hiyo unawanyima huduma za serikali kwa mamlaka yako uliyo nayo.

Kwanza huna mamlaka ya kuwanyima huduma raia walipa kodi wanaokulipa mshahara wako, hata kama wangekutukana achilia mbali kukosoa tu ubora wa huduma zinazotolewa na wizara yako.

Soma pia: Bashe anamfananisha Mpina na Dr Kigwangalla, ngoja tuone!

Pili wewe, watu wa wizara yako, idara zilizo chini yake na wafanyakazi wa Halmashauri ndio mmeajiriwa kuleta masuluhisho ya matatizo na changamoto za raia katika kilimo. Kama hamuwezi mnatikwa muache kazi muondoke ofisini badala ya kutishia kutopoleka huduma kwa wakosoaji.

Nyie ndio mnawajibika kuleta masuluhisho na majawabu, walipa kodi hawana wajibu huo ila wanazo haki kikamilifu kuwakosoa kama hawapendezwi na utendaji wenu. Kama mnaona hilo ni tatizo acheni kazi.

Bashe anawakilisha kundi kubwa la viongozi wa nchi hii wasioelewa vizuri dhana ya uwajibikaji kwa raia.
 
Fikra za watawala na watawaliwa ni kwamba watawala eti wanawapa msaada watawaliwa. Yani kwa kauli yake ilibidi leo asiwe ofisini. Hii ina maana kwamba mbunge akimhoji na kumtuhumu waziri bungeni, basi waziri anaweza kuamua kutopeleka maendeleo jimboni kwake. matokeo yake ni kwamba kwa wabunge kuogopa kuwatuhumu mawaziri bunge litazidi kuwa butu.
 
Huyo msomali arudi kwao Mogadishu. Yeye na nywele zake zile ni wa kusema watanzania halisi atawanyima huduma kweli ?
 
Chanjo za Korona zichunguzwe kwa wote waliozitumia!

Tutajua mengi
 
Back
Top Bottom