Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,637
- 8,947
Uislam unatesa sana wanawake. Kwaninin wanaume wao wasiwekewe sheria za kutowatamani? Afughanistan, Taliban sasa madirisha ya jikoni yazibwe, nyumba ambazo zimeelekea eneo wanawake hujikusanya mfano kisimani madirisha yafungwe au yazibwe, wanawake hata sauti yao isisikiwe hata wakiwa jikoni, ukiacha kujifunika hadi anakuwa kituko, Kusoma ndio kabisaaa hawaruhusiwi, wala ajira.
Uislam hujaribu kupambana na dhambi kwa mtulinga ya misuli hii ya Gym wakati akili ambayo ndio inahitaji dawa inaachwa wazi. Ndio maana unajaribu kuenezwa kwa nguvu za kumwaga damu. Kama wakiacha uhuru watu wachague waabudu nani hata huu MDAHALO anayekuja nao asingepata mtu.
Kosa lingine la mdahalo huu ni kuwashindanisha ambao hawapo halafu unaweka mwingine awe badala yao.
Huu mdahalo kama hawa
Jesus of Nazaret Vs Mohammad s.w.a wangekuwepo. Hivi nani angetoboa kwa hoja za piga nikupige? Leta hoja nijibu hoja.
Kifupi Jesus ni zaidi ya Nabii, hilo neno Zaidi ya Nabii ZINGATIA.
Jambo lingine huwezi kusema Wafuasi wa Jesus Wakajibu hoja, mdahalo umeandaliwa pasipo kuhusisha upande wa pili ili waandae wanazuoni kwenda kujibu kwa hiyo atajiuliza na kujijibu mleta mada na atajipa ushindi. Ila huku kitaa wafuasi lazima tuwaburuze kama wakija kwa hoja moja moja ..
Tahadhari; Naweka angalizo. Sijasema mtu, wala kushambulia dini, ukiona kama umeshambuliwa ni mawazo yako tu, maana mimi naishi na ndugu , marafiki na jamaa wa imani hiyo kwa amani na furaha.
Hata hivyo Mungu hapiganiwwi na wanadamu bali hujipigania Mwenyewe
Na unaamini kila unachoambiwa , mateso ya wanawake yako kwa hao wanaokuambia hivyo , kwani huko wanawake wanatolewa akili na kutengeneza filamu za uchi huku wengine wakichukuliwa farasi kuwaingilia
Hebu tuiache Biblia itueleze:
Yesu akaondoka huko, akaenda kando pande za Tiro na Sidoni. Na tazama, mwanamke Mkananayo wa mipaka ile akatokea, akampazia sauti akisema, Unirehemu, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu amepagawa sana na pepo. Wala yeye hakumjibu neno. Nao wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakisema, Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu. Akajibu, akisema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Naye akaja akamsujudia, akisema, Bwana, unisaidie. akajibu, akasema, Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa. Akasema, Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yaangukayo mezani za bwana zao. Ndipo Yesu akajibu, akamwambia, Mama, imani yako ni kubwa; na iwe kwako kama utakavyo. Akapona binti yake tangu saa ile.
Mathayo 15.21-28
Kwa maneno yasiotatanisha Yesu Kristo anasema kuwa yeye hakutumwa ila kwa "kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli."
Hakuwajia Waarabu, wala Wazungu, wala Wahindi, wala Waafrika, wala Machina.
Kama hayo hayakutosha kuonyesha kuwa yeye hakuwajia wasio Mayahudi anazidi kufahamisha kwa mfano wa kumkata mtu kiu: Si vema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
Mtume Muhammad SAW alikuja kwa watu wote