Asante kwa majibu, sasa kama mambo yako hivi, huu mfumo una maana gani? Waache tu mambo yafanyike locally, wamewaongezea matatizo wafanyakazi wenye matatizo badala ya kuwasaidia, maana sasa uende kwenye mfumo halafu ufanye yote yale ya awali.
Wakati huo huo mfumo haukusaidii kukuenesha wapi kuna fursa ya kuhamia kwa kada yako, hauna sehemu watumishi wanaweza kuwasiliana, haumuwezeshi mtumishi hata kuweka namba za mawasiliano yake...
Kuhusu taarifa za mtumishi ambazo HR anazijua kama suspension, probation, au kuwepo shuleni, kwanini mfumo usimuwezeshe HR ku-update status hizo za mtumishi, nini maana ya mfumo unaoshidwa kuweka taarifa muhimu kama hizi kwenye uhamisho?