KERO Huu mfumo wa Employee Self Service wa Utumishi haufanyi kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Kwenye mambo ya kumkandamiza mtumishi wako fasta ila kwenye masuala ya kumsaidia mtumishi mfumo unamkandamiza zaidi inasikitisha sana
 
Mkuu samahani, unamaanisha nini unaposema wilaya zinatofautiana? Kuna halmashauri ina idara au muundo tofauti na halmashauri nyengine?

Kila mtumishi ana namba zake tofauti na mtumishi mwengine zinazomtambulisha, ndio maana ya kuwa NIDA na check number.

Hayo ya kumjua mtu personally hayahusiani na uhamisho, ndio mianya ya rushwa na upendeleo.
 
Jambo gani utumishi waliwahi kufanikiwa zaidi ya kuinua inua mabega na kuweka tai zao sawa
 
mimi hapa niliwahi kusaidiwa na IT

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app

Wanasaidia ikiwa unawapita kiwango cha mshahara, au unao ushawishi wa kubadilisha mapato yao, au kuna personal relationship, au yeye ana shida flani kwako, au kwa kuwapa hela ya soda, or something of that kind.
 
Umeweka vizuri sana
 
Mkuu Mahotera habari,
Naba nikukumbushe kuwa katika Sheria kuna Sheria kuu na pia kuna By laws..

Sheria kuu Hutumika Nchi nzima ila By laws hutumika Katika eneo fulani na Kila halmashauri ina By laws Zake ambazo hutungwa na Baraza la Madiwani..

Kwahyo kulingana na Sheria Halmashauri hazilingani kwa Sheria na Taratibu mchi nzima..japo zimaweza kuwa.na mfanano wa kimadaraka..

Kuhusu Mtumishi na Taarifa zake kama nilivyosema sema awali..

Uhamisho una Vigezo vyake na masharti yake..
Anayejua umetimiza vigezo vyote ni HR wako na Mwajiri wako huko Halmashauri..

Kwa mfano anayejua Uko shule kwa sasa ni Mwajiri wako (Na ndo unayesaini naye mkataba wa kutokuhama huwapo shuleni)..

Anayejua kuwa Unashida ya kinidhamu na upo kwenyr Probation ya Kinidhamu ni wilaya yako na Si tamisemi hivyo ni vyema Kutoku-centralise hii huduma ili wale wanaostahili waipate na wale wasio stahili wasiipate..

mbona tunajifanya kama hatujui Lazma supervisors wako wakujue na hata mwajiri wako ajue information zako ajiridhishe kweli una vigezo...

Nafikiri nimekujibu kama una swali la nyongeza karibu
 
Asante kwa majibu, sasa kama mambo yako hivi, huu mfumo una maana gani? Waache tu mambo yafanyike locally, wamewaongezea matatizo wafanyakazi wenye matatizo badala ya kuwasaidia, maana sasa uende kwenye mfumo halafu ufanye yote yale ya awali.

Wakati huo huo mfumo haukusaidii kukuenesha wapi kuna fursa ya kuhamia kwa kada yako, hauna sehemu watumishi wanaweza kuwasiliana, haumuwezeshi mtumishi hata kuweka namba za mawasiliano yake...

Kuhusu taarifa za mtumishi ambazo HR anazijua kama suspension, probation, au kuwepo shuleni, kwanini mfumo usimuwezeshe HR ku-update status hizo za mtumishi, nini maana ya mfumo unaoshidwa kuweka taarifa muhimu kama hizi kwenye uhamisho?
 
Umewahi kusikia Kitu kinaitwa Local Public?
Au Public but Locally?
Ndo mfumo huu unavyofanya kazi..

VItu vyote vimewekwa Public but kwa manufaa yanayofanyika local na hata maelezo yake yako clear kabisa.. Nitayaweka..baadae..

Kuhusu Sehemu ya kuweka Namba sio kweli (Nahisi mfumo huujui)..Kuhusu wanaobadilishana kubadilishana namba kwenhe mfumo ipo kuna namba yako na hata namba ya mwingine kuna sehemu ya Transfer incoming na outgoing utaona wanaotaka kuja Sehemu ulipo na namba zao ukiridhishwa unaweza kuwacontact na mkapanga kubadilishana..
Upitie mfumo ndugu utauelewa..
Na hii ndo process nzma ya uhamisho..Mkuu

Kuna kosa lolote hapo niulize nitakujibu
 
Tangu mfumo uanze kuna mtumishi yeyote aliyefanikiwa kupata uhamisho wa let's say kutoka mkoa A kwenda mkoa B baada ya kuomba uhamisho huo kupitia mfumo?
Mfumo umewekwa ili kuzuia watu wasiwe wanahama. Au kama ikitokea wanahama isiwe simple, matokeo yake wakate tamaa waendelee kutumika na halmashauri zao.
 
Nimecheka Sana Sana, ukute jamaa labda ndio lengo lao, ukosee ujikute mfumo unakuletea Meseji " Ombi lako la kuacha KAZI ndani ya saa 24 limefanikiwa"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…