KERO Huu mfumo wa Employee Self Service wa Utumishi haufanyi kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nilikuwa ninamjibu huyo aliyesema kuwa watu wote wamefundishwa kutumia huo mfumo kitu ambacho siyo kweli. Afterall wengine hata account za Facebook wala Instagram hatuna na hatutumii hiyo mitandao. Mfumo ufanyiwe marekebisho una mapungufu mengi.
Nadhani kuliko kulalamika ungeweza kuweka mapungufu unayokutana nayo kwenye huu uzi najua wataalamu wa huo mfumo na serikali kwa ujumla wanapitia huu uzi ili kuweza kuwasaidia watu wenye changamoto. Kuendelea kuilalamikia serikali bila kusema una changamoto zipi utaendelea kuteseka.
 
Watumishi wa serikali wengi niliowasikiliza ni uzembe tu na uvivu wa kujifunza hakuna jambo lolote gumu kwenye huu mfumo wa ess. Imagine mtu analalamika hana email na hawezi kujiunga na email. Huyo ni msomi na anakesha kwenye magrupu ya WhatsApp
Hizo cases zipo nyingi tu, sio watu wote ni watundu wa teknolojia. Waelekezeni watu na sio kutoa vitisho na kuasume kila unachojua wewe basi kila mtu anajua.
 
Kwani matumizi ya huo mfumo ni kwa faida ya nani? Hela ya nauli uliyokua unalipa kufuatilia uhamisho TAMISEMI na sasa unaweza ku browse kwenye computer au simu yako si uweke bando?
Mpaka sasa so far sijajua huu mfumo ni kwa faida ya nani. Maana sijaona kilichopungua zaidi ya kuongezeka. Na kwani mfumo upo kwaajili ya uhamisho tu? Mie sifuatilii uhamisho hivyo nipe bando.

Tena hao wa uhamisho ndio wa kuwahurumia, wanajiuliza na kujijibu wenyewe maana hawapewi majibu ya kueleweka na huko mfumoni ni tafrani!!
 
Mzeee Kuna watumishi wako uvinza huko sijui Tanganyika ..... . mtandao Hadi kupanda milimani mvua zikinyesha hakuendeki maduka ya kutafuta wamejaribu kuwafikiria watu wa chakaaa
 
Zamani ulikua ukitaka mkopo mpaka ukamuone afisa mikopo wa benki na ukamtie posho na hela utapata baada ya wiki siku hizi unabonyeza kwenye mfumo tuu ndani ya saa 24 hela imeingia. bado hujaona faida ya mifumo ndugu mtumishi?
 
Weeeh wapi huko kulikuwa na huo urasimu!! Sijawahi experience hicho kitu.
 
Acha uwongo , Kwan watu wa TAMISEMI hawawez kujua taarifa zako kupitia check number yako au NIDA yako ? Wakiangalia wanajua huyu NI mtumish halmashauri fulan
 
Yani mkopo mnatoa mpaka Rushwa[emoji3][emoji1787][emoji1787] bongo sijui mnafeli wapi ,
Mimi Nina mikopo ya utumish sijawah kuwaza et nimpe Rushwa Afisa mikopo

Nina mikopo ya biashara ambayo haihusiani na utumish , niliwauliza nahitaji niwe na nini ili nipate mkopo wa biashara nikapeleka wanavyohitaji nikawaacha wajiridhishe wenyewe baada ya wiki nikaona mzgo huo umeingia,
Afisa mikopo akanipigia Tu simu kuuliza kama nimeona kibunda nikamwambia nimeona , sijawah kuwaza kutoa Rushwa ,

Kutoa Rushwa NI ishara kwamba huna sifa za kukopesheka na uhakika wa kulipa deni lao unatia mashaka ,

Mikopo ndo inaleta Faida kwa bank , wale maafisa mikopo wanapewa tasks kuhakikisha watu wanakopa kwa wingi
 
Acha uwongo , Kwan watu wa TAMISEMI hawawez kujua taarifa zako kupitia check number yako au NIDA yako ? Wakiangalia wanajua huyu NI mtumish halmashauri fulan
Wanajua Vyote ulivyosema ila kuna Baadhibya Taarifa wanakosa kama Taarifa za utendaji kazi zako kituo ulichopp kwa sasa maendeleo yako kituoni na kinidhamu..hata kwa wale watumishi ambao wako Masomoni pia..na taarifa zote ambazo zipo chini ya Maamuzi ya Baraza la madiwani na halmashauri husika..

Taarifa hizo hazipo TAmisemi ila zipo halmashauri kwako!
Umenielewa mkuu
 
Mzeee Kuna watumishi wako uvinza huko sijui Tanganyika ..... . mtandao Hadi kupanda milimani mvua zikinyesha hakuendeki maduka ya kutafuta wamejaribu kuwafikiria watu wa chakaaa
Hahahaha kuna Shule pale Wilaya ya Tanganyika iko kati kati ya Pori
 
Weeeh wapi huko kulikuwa na huo urasimu!! Sijawahi experience hicho kitu.
Tanzania hii hii nchi kubwa hii unadhani watumishi waliopo maeneo ya vijijini kabisa huko pembezoni maisha yao yalikuaje.kwanza mpaka afike benki ni km 100 kwahiyo atapoteza siku 3 au 4 nje ya kituo cha kazi kushughulikia mkopo na hapo lazima amwachie loan officer wa benki chochote. Serikali inajitajidi sana kuhakikisha huduma zinakuwa rahisi kupitia hii mifumo.
 
Hongera ila wenzako waliopitia hii changamoto hapo zamani wanajua namaanisha nini.
 
Sasa hao wa pembezoni huko ambako hata umeme hamna wala mtandao ndio mmewasaidia nini sasa!!
 
Waongo hao wanatafuta tu kichaka cha kujitetea. Hao maafisa mikopo wanavyobembeleza watu kuchukua mikopo ndio watake rushwa!!
 
Si mna huo mfumo wenu, why msiziweke?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…