Atoto
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 86,410
- 169,862
Mnafanya mambo kwa mazoea as usual, hapo ndio mwisho wenu wa kufikiri na mkiona hamna la maana mmefanya mnahamia kwenye vitisho.Asante sana Elli Umeeleza vizuri sana..
Hata hao masupervisor wanaosemwa hawajui mfumo Cha ajabu wana mifumo lukuki wanaitumia kabla ya Mfumo huo Kuja Upande wa Elimu Kuna ffars, PlanRep ,Na hata Ule wa Wanafunzi..
Upande wa Afya na idara zingine kuna mifumo Vile vile GotHomis, Ffars ,Dhis2, na Mingine mingi...
Yote hiyo hamuitumii?
Sasa kwnini wanafikiria kuwa kila kitu lazma ufunfishwe wakati unakijua?
Wewe unajua Kusoma Ubaoni unataka tena Ufundishwe Kusoma kutumia kitabu?
Hebu tujifunze kuwa Nashkrani..
Ndo maana nimesema ikiwa unaona Weww ni supervisor na hautaki kufanya kazi yako,Au wewe ni mtumishi hautaki kufanya kazi yako utaona kitakachokutokea..
Na sasa hivi taarifa Za PEPMIS Zinatakiwa zijazwe kila siku sasa zembeeni kujaza tena mseme.hamjafundishwa..
Mtu anatumia Simu yake ana Bando la kuingia Whatsapp kuingia Jamiiforum na kujibu email ila eti hana Bando la kuingia Kwenye mfumo..
"Usiulize Serikali itakufanyia nini wewe ,Bali jiulize Utaifanyia nini Serikali"...
CC: Kisesetusese Atoto
Hilo bando analotumia kuingia kwenye social media ni ameweka kwaajili ya matumizi yake binafsi. Ingekuwa hivyo basi haina haja pia kununua magari ya serikali kwasababu tayari mnao uwezo wa kujinunulia magari yenu mnayotumia kwenye safari zenu binafsi, basi yatumieni pia katika kazi za serikali. Pia msilipane posho mnazopeana kwakuwa mpo katika kutekeleza majukumu yenu ya kikazi ambayo mmeajiriwa kwayo.
Hiyo mifumo unayoongelea, ililetwa na wakaitumia bila maelekezo? Mnaasume tu vitu bila kufuatilia ni wapi mnakwama kwaajili ya kuboresha. Mfumo wenyewe uko hovyo kuingia tu ni kizungumkuti hizo taarifa mnazotaka kila siku mmefikiria kwa mapana? Au ni kichaka cha kufichia uozo wenu!!!
No wonder allmost everything is a failure huko serikalini.