KERO Huu mfumo wa Employee Self Service wa Utumishi haufanyi kazi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Asante sana Elli Umeeleza vizuri sana..
Hata hao masupervisor wanaosemwa hawajui mfumo Cha ajabu wana mifumo lukuki wanaitumia kabla ya Mfumo huo Kuja Upande wa Elimu Kuna ffars, PlanRep ,Na hata Ule wa Wanafunzi..
Upande wa Afya na idara zingine kuna mifumo Vile vile GotHomis, Ffars ,Dhis2, na Mingine mingi...

Yote hiyo hamuitumii?
Sasa kwnini wanafikiria kuwa kila kitu lazma ufunfishwe wakati unakijua?

Wewe unajua Kusoma Ubaoni unataka tena Ufundishwe Kusoma kutumia kitabu?

Hebu tujifunze kuwa Nashkrani..
Ndo maana nimesema ikiwa unaona Weww ni supervisor na hautaki kufanya kazi yako,Au wewe ni mtumishi hautaki kufanya kazi yako utaona kitakachokutokea..

Na sasa hivi taarifa Za PEPMIS Zinatakiwa zijazwe kila siku sasa zembeeni kujaza tena mseme.hamjafundishwa..

Mtu anatumia Simu yake ana Bando la kuingia Whatsapp kuingia Jamiiforum na kujibu email ila eti hana Bando la kuingia Kwenye mfumo..

"Usiulize Serikali itakufanyia nini wewe ,Bali jiulize Utaifanyia nini Serikali"...

CC: Kisesetusese Atoto
Mnafanya mambo kwa mazoea as usual, hapo ndio mwisho wenu wa kufikiri na mkiona hamna la maana mmefanya mnahamia kwenye vitisho.

Hilo bando analotumia kuingia kwenye social media ni ameweka kwaajili ya matumizi yake binafsi. Ingekuwa hivyo basi haina haja pia kununua magari ya serikali kwasababu tayari mnao uwezo wa kujinunulia magari yenu mnayotumia kwenye safari zenu binafsi, basi yatumieni pia katika kazi za serikali. Pia msilipane posho mnazopeana kwakuwa mpo katika kutekeleza majukumu yenu ya kikazi ambayo mmeajiriwa kwayo.

Hiyo mifumo unayoongelea, ililetwa na wakaitumia bila maelekezo? Mnaasume tu vitu bila kufuatilia ni wapi mnakwama kwaajili ya kuboresha. Mfumo wenyewe uko hovyo kuingia tu ni kizungumkuti hizo taarifa mnazotaka kila siku mmefikiria kwa mapana? Au ni kichaka cha kufichia uozo wenu!!!
No wonder allmost everything is a failure huko serikalini.
 
Ni kuwashughulisha watu na ma-mifumo ambayo hayana tija yoyote ile zaidi ya kuongeza usumbufu na kupunguzia watu morale ya kazi, kila siku wabaki kuwaza kuingiza taarifa kwenye mfumo badala ya kuwajibika na kazi za kila siku....​
Watu kama nyie ni mzigo kwa nchi. Wenzetu wapo mbali kwa matumizi ya sayansi na teknolojia serikali inataka kuwasaidia ila ndio hivyo mambumbu hamjielewi. Nikuulize tu kwa mfano matumizi ya mifumo kulipa bill za serikali mf.umeme , maji nk huoni ni kwa namna gani inaongeza ufanisi na kupunguza mianya ya rushwa?
 
Mpwa, Mimi sio mwajiriwa ila niliingia kwenye huo unaitwa Mfumo kwa ajili ya kumsaidia Wife. Ukweli ni kwamba hakuna kitu chochote cha maana cha kusema eti hadi ufundishwe ....

Mfumo Una lugha mbili, kikristo na kiarabu, unachagua, unajaza unachotaka au unatafuta unachotaka, inakupa maelekezo mengine. Wala hakuna jipya.

Ni Aibu eti mwajiriwa WA Serikali kwa position ya IT anashindwa kuutumia huo "mfumo"! Mbona Gmail na kwengine tuna uwezo WA kuandika, kupost, ku reply, ku edit, etc? Nani alifundisha??
Kama unaongelea IT ni sawa, ila kama unaongelea watumishi wa kawaida basi umekosea sana. Hivi una habari kuwa kuna watumishi hata smartphone kutumia tu hawajawahi na hawawezi!!!

Kilicho rahisi kwako usiassume kuwa ni rahisi kwa kila mtu. Jihakikishie kwanza.
 
Tuko watu wengi sana ambao hatujafundishwa huu mfumo na TUMELAZIMISHWA kuendelea nao hivyo hivyo tunajifunza kadri tunavyofanya kazi.

Ila ninachokiona kuwa bado mfumo ni mpya na mgeni kwa watu wengi. Mfano sisi kazini kwetu tumeufahamu wiki ya Christmas na kulazimishwa kujaza kabla ya 31 Dec 2023. Mfumo hata miezi miwili hauna!! Kwanza registration yenyewe ilisumbua siku 4 mtu unashindwa kujisajili.

Mimi nadhani tuupe muda ni mapema mno kulalamika. Wanaweza kutatua tatizo ni kama ulivyosema HR na watu wa IT

Elli
Shida ya watanzania ni uvivu hata kwa jambo lenye manufaa kwake binafsi na taifa kwa ujumla. Matumizi ya TEHAMA kwa mambo ya msingi mtu anaona kama kashikiwa panga shingoni ila mwambie mange kimangi kapost fumanizi la diamond uone atakavyoingia Instagram kama ana kichaa.
 
Acheni siasa kwenye maisha ya watu. Nyie mnaujua mfumo basi mnahisi kila mtu anaujua. Hicho anachoongea ni kweli kabisa, huu mfumo una mizengwe lukuki na hamjatoa elimu ya kutosha kwa hao mnaowaita supervisors. Wanahaha nao balaa. Achilia mbali watumishi wa kawaida ndio tunaburuzwa tu hata hatuelewi kitu.

Malalamiko ni mengi, yafanyieni kazi kuliko kushupaza shingo ionekane mlichofanya ni cha maana sana.

Halafu hivii mlifikiria na wanaokaa kwenye maeneo ambayo mtandao ni shida? Vipi na bando mtakuwa mnatupatia au mnatuchosha tu!!!
Ukiingia Instagram kusoma ubuyu wa mambe kimangi nani anakuwekea bando?
 
Serikali inajitajidi kufanya utumishi uwe wa kisasa na kurahisisha mambo kwa teknolojia watumishi ambao tunaamini ni wasomi mnalalamika sasa mwananchi kule kijijini atasemaje?
Tunalalamikia mapungufu makubwa yaliyo katika mfumo huo. Na namna unavyolazimishiwa kutumika ukiwa na mapungufu makubwa. Badala muyachukue myafanyie kazi mnajifanya kuwatukana watu!!
 
Mpwa, Mimi sio mwajiriwa ila niliingia kwenye huo unaitwa Mfumo kwa ajili ya kumsaidia Wife. Ukweli ni kwamba hakuna kitu chochote cha maana cha kusema eti hadi ufundishwe ....

Mfumo Una lugha mbili, kikristo na kiarabu, unachagua, unajaza unachotaka au unatafuta unachotaka, inakupa maelekezo mengine. Wala hakuna jipya.

Ni Aibu eti mwajiriwa WA Serikali kwa position ya IT anashindwa kuutumia huo "mfumo"! Mbona Gmail na kwengine tuna uwezo WA kuandika, kupost, ku reply, ku edit, etc? Nani alifundisha??
Asante sana .hata watumishi wa serikali unashangaa analalamika hawezi kuunganishwa unajiuliza huyu msomi hawezi je mkulima huko kijijini atasaidiwa na nani? Nilichogundua siyo kuwa hawawezi bali ni uvivu na kupuuzia mambo ya msingi yani mpaka eti watishiwe kufutwa kazi ndio mtu ajishughulishe pumbavu sana .unajiuliza huku JF Instagram tick tok nani anawaunganisha?
 
Mfumo wa ESS ni closed loop Public system,

Kwa sababu Ukihitaji kitu kubadili au kuweka sawa unamcontact IT wako wa wilaya au HR wako...

hUu mfumo unataarifa sensitive za kiutumishi hivyo kushughilka na taarifa sensitive kama hizo kwa online help haitakuwa jambo zuri.

Ndo maana unashauriwa umconsult HR wako kwa sababu ndo.anakujua ila TAMISEMI Wala UTUMISHI hawajui maendeleo yako ofisini.

Ni tofauti na mifumo mingine
Kwa hili,leo mi napingana na wewe. Maana ya centrelized sysytem ni nini? Hao HRs na wengine,lazima wawe na kitengo kikuu. Na wao,wajaze taarifa za kila mtu. Sasa,jiulize unaenda Dar au Dodoma kiofisi,labda umetokea Kigoma au Mtwara. Unaambiwa taarifa zako hatuna. HR anatakiwa aulizwe na ajibu mtandaoni(approval),vinginevyo,basi hapo walipo,wapewe full mamlaka.
Ikiwa hivyo,basi taasisi inayosimamia hicho kitengo,haiaminiki. Kama jeshi linawateua watu wanasimamia taarifa nyeti za usalama wa nchi,hizo za sekta nyingine zitakosaje watu wa kuzisimamia. Kama nchi haina wafanyakazi wazalendo,si iuzwe basi🤣🤣🤣🤣
 
Mnafanya mambo kwa mazoea as usual, hapo ndio mwisho wenu wa kufikiri na mkiona hamna la maana mmefanya mnahamia kwenye vitisho.

Hilo bando analotumia kuingia kwenye social media ni ameweka kwaajili ya matumizi yake binafsi. Ingekuwa hivyo basi haina haja pia kununua magari ya serikali kwasababu tayari mnao uwezo wa kujinunulia magari yenu mnayotumia kwenye safari zenu binafsi, basi yatumieni pia katika kazi za serikali. Pia msilipane posho mnazopeana kwakuwa mpo katika kutekeleza majukumu yenu ya kikazi ambayo mmeajiriwa kwayo.

Hiyo mifumo unayoongelea, ililetwa na wakaitumia bila maelekezo? Mnaasume tu vitu bila kufuatilia ni wapi mnakwama kwaajili ya kuboresha. Mfumo wenyewe uko hovyo kuingia tu ni kizungumkuti hizo taarifa mnazotaka kila siku mmefikiria kwa mapana? Au ni kichaka cha kufichia uozo wenu!!!
No wonder allmost everything is a failure huko serikalini.
Atoto twende polepole..
Uko serious kabisa Unasema Bando umeweka kwa matumizi yako binafsi na unashindwa kutuma na ku-Update taarifa zako kwa sababu mfumo sio mambo yako Binafsi?
Nyie ndo wale mkiachiwa Ofisi. Za umma hamzichukulii Kama ni zenu bali mnazichukulia kama Za umma na ndo maana ofisi nyingi ziko Hovyo hovyo..

Kwanini usipende kazi yako..
Maana ndo inayokuletea kipato hicho unachonunua Vocha na kujiunga bando halafu leo hii unasema Mfumo wa kujaza taarifa zako za kiutumishi sio Priority?

Hii ni sawa.na wachungaji Wanaowadhihaki wafuasi wao na bado wanataka Sadaka kutoka kwa wafuasi hao hao!..

Kila mtu afanye majukumu Yake tu mfumo sio mgumu Kwa matumizi yoyote una maalekezo yote manual zipo Ukiona huwezi kufanya Mpe Taarifa kiongozi wa TEHAMA wilayani kwako..
Kwani kuna ugumu Gani?
Unataka watu waamini kwamba Hamko Competent kuclaim ofisi mlizonazo?
 
Tunalalamikia mapungufu makubwa yaliyo katika mfumo huo. Na namna unavyolazimishiwa kutumika ukiwa na mapungufu makubwa. Badala muyachukue myafanyie kazi mnajifanya kuwatukana watu!!
Watumishi wa serikali wengi niliowasikiliza ni uzembe tu na uvivu wa kujifunza hakuna jambo lolote gumu kwenye huu mfumo wa ess. Imagine mtu analalamika hana email na hawezi kujiunga na email. Huyo ni msomi na anakesha kwenye magrupu ya WhatsApp
 
Asante sana Elli

Mtu anatumia Simu yake ana Bando la kuingia Whatsapp kuingia Jamiiforum na kujibu email ila eti hana Bando la kuingia Kwenye mfumo..

"Usiulize Serikali itakufanyia nini wewe ,Bali jiulize Utaifanyia nini Serikali"...

CC: Kisesetusese Atoto

Vitisho on the way!
Una uhakika watumishi wote wanaingia mitandaoni kila siku?
Mlizingatia mazingira sawa ya upatikanaji wa internet Kwa watumishi wote ndani ya Jamuhuri ya muungano wa TZ?

Msije mkaleta taflani Kwa watumishi ambao wanafanyia Kazi ktk mazingira duni sana (Hakuna Umeme, internet hakuna, n.k.)
 
Asante sana Elli Umeeleza vizuri sana..
Hata hao masupervisor wanaosemwa hawajui mfumo Cha ajabu wana mifumo lukuki wanaitumia kabla ya Mfumo huo Kuja Upande wa Elimu Kuna ffars, PlanRep ,Na hata Ule wa Wanafunzi..
Upande wa Afya na idara zingine kuna mifumo Vile vile GotHomis, Ffars ,Dhis2, na Mingine mingi...

Yote hiyo hamuitumii?
Sasa kwnini wanafikiria kuwa kila kitu lazma ufunfishwe wakati unakijua?

Wewe unajua Kusoma Ubaoni unataka tena Ufundishwe Kusoma kutumia kitabu?

Hebu tujifunze kuwa Nashkrani..
Ndo maana nimesema ikiwa unaona Weww ni supervisor na hautaki kufanya kazi yako,Au wewe ni mtumishi hautaki kufanya kazi yako utaona kitakachokutokea..

Na sasa hivi taarifa Za PEPMIS Zinatakiwa zijazwe kila siku sasa zembeeni kujaza tena mseme.hamjafundishwa..

Mtu anatumia Simu yake ana Bando la kuingia Whatsapp kuingia Jamiiforum na kujibu email ila eti hana Bando la kuingia Kwenye mfumo..

"Usiulize Serikali itakufanyia nini wewe ,Bali jiulize Utaifanyia nini Serikali"...

CC: Kisesetusese Atoto
Bando la kuweka ili nihangaike na hii mifumo natoa kwenye mshahara huu huu uliojaa makato?

Nyinyi watu mna dhambi sana.
 
Ukisafiri safari ya kikazi nani anayekulipia nauli na posho?
Kwani matumizi ya huo mfumo ni kwa faida ya nani? Hela ya nauli uliyokua unalipa kufuatilia uhamisho TAMISEMI na sasa unaweza ku browse kwenye computer au simu yako si uweke bando?
 
Kwa hili,leo mi napingana na wewe. Maana ya centrelized sysytem ni nini? Hao HRs na wengine,lazima wawe na kitengo kikuu. Na wao,wajaze taarifa za kila mtu. Sasa,jiulize unaenda Dar au Dodoma kiofisi,labda umetokea Kigoma au Mtwara. Unaambiwa taarifa zako hatuna. HR anatakiwa aulizwe na ajibu mtandaoni(approval),vinginevyo,basi hapo walipo,wapewe full mamlaka.
Ikiwa hivyo,basi taasisi inayosimamia hicho kitengo,haiaminiki. Kama jeshi linawateua watu wanasimamia taarifa nyeti za usalama wa nchi,hizo za sekta nyingine zitakosaje watu wa kuzisimamia. Kama nchi haina wafanyakazi wazalendo,si iuzwe basi🤣🤣🤣🤣
Kama unafanya kazi chini ya Tamisemi Sio Centralised system ni Decentralised Maana ni lazma taarifa zote zitoke chini Ziende Juu!

Mfumo wa Zamani wa (HCMIS), ambao kwa sasa Wanatumia Wakurugenzi pekee na Kiongozi wa Ofisi ya Utumishi ina Taarifa zako zote..

Sasa utaendaje Wizarani Na hukuanzia Chini?
Lazima Uanze chini ili ukifika juu Kuwe na taarifa na unaenda kufanya nini na kwa kusudi gani...
 
Vitisho on the way!
Una uhakika watumishi wote wanaingia mitandaoni kila siku?
Mlizingatia mazingira sawa ya upatikanaji wa internet Kwa watumishi wote ndani ya Jamuhuri ya muungano wa TZ?

Msije mkaleta taflani Kwa watumishi ambao wanafanyia Kazi ktk mazingira duni sana (Hakuna Umeme, internet hakuna, n.k.)
Mkuu Unafahamu kuwa unapoingia kwenye simu yako na Kuwasha Data Simu yangu inatuma Cockies kwa baadhi ya Sites Kuwa uko online?

Avarage coverage ya Mfumo Imezingatia Pilot zilizofanywa Kwanza kabla ya kuuweka Mfumo online..
 
Shida ya watanzania ni uvivu hata kwa jambo lenye manufaa kwake binafsi na taifa kwa ujumla. Matumizi ya TEHAMA kwa mambo ya msingi mtu anaona kama kashikiwa panga shingoni ila mwambie mange kimangi kapost fumanizi la diamond uone atakavyoingia Instagram kama ana kichaa.
Nilikuwa ninamjibu huyo aliyesema kuwa watu wote wamefundishwa kutumia huo mfumo kitu ambacho siyo kweli. Afterall wengine hata account za Facebook wala Instagram hatuna na hatutumii hiyo mitandao. Mfumo ufanyiwe marekebisho una mapungufu mengi.
 
Atoto twende polepole..
Uko serious kabisa Unasema Bando umeweka kwa matumizi yako binafsi na unashindwa kutuma na ku-Update taarifa zako kwa sababu mfumo sio mambo yako Binafsi?
Nyie ndo wale mkiachiwa Ofisi. Za umma hamzichukulii Kama ni zenu bali mnazichukulia kama Za umma na ndo maana ofisi nyingi ziko Hovyo hovyo..

Kwanini usipende kazi yako..
Maana ndo inayokuletea kipato hicho unachonunua Vocha na kujiunga bando halafu leo hii unasema Mfumo wa kujaza taarifa zako za kiutumishi sio Priority?

Hii ni sawa.na wachungaji Wanaowadhihaki wafuasi wao na bado wanataka Sadaka kutoka kwa wafuasi hao hao!..

Kila mtu afanye majukumu Yake tu mfumo sio mgumu Kwa matumizi yoyote una maalekezo yote manual zipo Ukiona huwezi kufanya Mpe Taarifa kiongozi wa TEHAMA wilayani kwako..
Kwani kuna ugumu Gani?
Unataka watu waamini kwamba Hamko Competent kuclaim ofisi mlizonazo?
Na haya ndio majibu mnapenda na ndio mnayatoa hata tukija huko maofisini kwenu. Hamtaki kufanyia kazi yanayowahusu ila mnataka sisi tufanyie kazi yanayotuhusu.

Kazi tunafanya ila nanyi fanyeni nafasi yenu, msiwe na majibu ya jumla jumla tu na kufanya kazi kwa mazoea huku mkiona watumishi wa umma wa chini ni wajibu wao kutumia fedha zao kutekeleza majukumu yao. Mbona ninyi huko juu hamfanyi hivyo? Au Unataka watu waamini kwamba Hamko Competent kuclaim ofisi mlizonazo?
 
Back
Top Bottom