Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Huu mjadala wa kususia bidhaa na huduma ni hatari kwa uchumi wa nchi

Nipo Space ya Maria Sarungi ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA na Wanaharakati wanajenga hoja juu ya kususia bidhaa na huduma mbalimbali ili kuikosesha serikali mapato.

Wanaanza na kutoa historia ya Boycotting ambapo kwa wakati fulani, watu wa Uingereza walikuwa hawapendezwi na biashara ya Utumwa. Ili kuukomesha, wakaacha kutumia Sukari ambayo ilikuwa ikitengenezwa na Watumwa. Na hivyo ikasabisha kiwanda kufungwa kwa sababu bidhaa hazitoki.

Wanasema kuwa, jamii ya Watanzania wakipunguza matumizi ya bidhaa na huduma kama vile unywaji wa Bia, kupunguza matumizi ya sukari, maji ya kunywa, kupunguza miamala isiyo ya lazima na vyakula katika hoteli zilizosajiliwa.

Wanaamini kuwa kupunguza huko matumizi ya huduma na bidhaa itasababisha serikali kukosa kiasi kikubwa cha mapato.

Na kukosa huko mapato itasababisha serikali ishindwe kujiendesha kwa sababu mapato yamepungua. Na bila shaka, kutafuta namna ya kukaa na wadau na kuzungumza nao ili kuweza kutatua yaliyomo.

Wanaamini kuwa, njia hii ya kususia bidhaa na huduma 'Boycotting' itakuwa na ufanisi kwa sababu hakuna polisi watakaokuja kuwalazimisha watu watumie.

Wanaona kuwa njia hii ni ya amani na hivyo itawalazimisha serikali kurudi katika Misingi ya Utawala bora na kuleta uchocheo wa Katiba mpya.

Je, CHADEMA watafanikiwa kwa njia hii?
Ni njia ya amani iliyofanikiwa sana kote ulimwenguni dhidi ya watawala dhalimu.

Naona mwisho wa kiburi na jeuri ya CCM(pesa)
 
Lema na Lisu waliwahi kuja na kampeni kwamba wafuasi wao wasusie laini za voda,, na kweli wafuasi wajinga wakawa wanatuma vipicha eti wamevunja laini za voda.

Siku walipokamatwa hao kina Lema wakatoa namba zao za voda kwa ajili ya kupokelea michango [emoji23][emoji23][emoji23]

Ni ujinga
This time tumejifunza haitatokea tena kurudi nyuma,tunasusia bidhaa moja kwa moja,ccm wakose hela jeuri kisha!

Wanatumia nguvu,sisi tunatumia akili.
 
Hili halitafanikiwa Mkuu.

Labda niweke hili wazi! Chadema imeshapoteza mbinu/akili ya kupambana na CCM. MBOWE akili yake imesha staafu. Imma aombe watu wengine wamchoree mipango au atoke aruhusu akili nyengine iingie ifanye kazi. Kwa haya madrama mnayokwenda nayo yaani hamna kitu.
Kama Mbowe akili imestaafu muacheni huru, mnamuogopa nini sasa?

Mwenye akili anadhibitiwa kwa kufungwa ila wewe usie na akili wanakuacha huru maana hauna madhara yoyote.
 
Kuna mjadala unaendelea space pale twitter aisee kama haya maazimio ya kususia bidhaa na huduma yatafanikiwa hakika itakuwa hatari kwa uchumi.

Ushauri serikali wakutane na wapinzani haraka maana hata mishahara ya mapolisi inaweza kukosa huko mbeleni.

Ni ushauri tu mnaweza kuufanyia kazi au kuupuza ila kama hatua hizi zitafanikiwa hata kwa 25% makusanyo yataporomoka sana.
View attachment 1877729
Achana na walevi wa faru john hao, kwani twitter kunauzwa bidhaa? Waliwahi kuhamasisha eti wana- Chadema wasusie mtandao wa Vodacom lkn walipokuwa na kesi wakahukumiwa kulipa faini wakatoa namba za simu za Vodacom kukusanyia michango, huo si ni uendawazimu..!!
 
Ni njia ya amani iliyofanikiwa sana kote ulimwenguni dhidi ya watawala dhalimu.

Naona mwisho wa kiburi na jeuri ya CCM(pesa)
Susieni hospitalini, ukikuta doctor ni mwana CCM ahirisha kutibiwa urudi nyumbani na kama itawezekana msiende hata huko hospitalini maana mtachangamana na Wana CCM.
 
Ndio mtapata tabu Sana na hoja zenu za sijui gas,sukari mara luku ,miamala haya mambo hayawahusu Vijijini,, serikali ikiwaambia tumewwka tozo watu wa mjini walipe Ili tuwajengee barabara, zahanati na maji au shule ni makofi kwa kwenda mbele .

Nyie machadema hamjui hata kuchambua bajeti za serikali,hamjui hoja za kutoka nazo mnakomaa na Katiba,nani kijijini anataka Katiba?

Kijijini hata mijini wakiambiwa wanataka walete vita wamefadhiliwa na bwana zeenu Ulaya fasta mnapuuzwa na watu..Hii nchi ina wajinga wengi haijawa tayari kwa vyama vingi,hata wanaotumia mitandao ya kijamii ni watu wa mjini kijijini hawana huo mda.

Hao watu wa vijijini wenyewe wanafuata lolote linaloamuliwa mjini. Kama mngekuwa mnawathamini hao watu wa vijijini viongozi nao wangeishi huko vijijini.
 
Nipo Space ya Maria Sarungi ambapo baadhi ya makada wa CHADEMA na Wanaharakati wanajenga hoja juu ya kususia bidhaa na huduma mbalimbali ili kuikosesha serikali mapato.

Wanaanza na kutoa historia ya Boycotting ambapo kwa wakati fulani, watu wa Uingereza walikuwa hawapendezwi na biashara ya Utumwa. Ili kuukomesha, wakaacha kutumia Sukari ambayo ilikuwa ikitengenezwa na Watumwa. Na hivyo ikasabisha kiwanda kufungwa kwa sababu bidhaa hazitoki.

Wanasema kuwa, jamii ya Watanzania wakipunguza matumizi ya bidhaa na huduma kama vile unywaji wa Bia, kupunguza matumizi ya sukari, maji ya kunywa, kupunguza miamala isiyo ya lazima na vyakula katika hoteli zilizosajiliwa.

Wanaamini kuwa kupunguza huko matumizi ya huduma na bidhaa itasababisha serikali kukosa kiasi kikubwa cha mapato.

Na kukosa huko mapato itasababisha serikali ishindwe kujiendesha kwa sababu mapato yamepungua. Na bila shaka, kutafuta namna ya kukaa na wadau na kuzungumza nao ili kuweza kutatua yaliyomo.

Wanaamini kuwa, njia hii ya kususia bidhaa na huduma 'Boycotting' itakuwa na ufanisi kwa sababu hakuna polisi watakaokuja kuwalazimisha watu watumie.

Wanaona kuwa njia hii ni ya amani na hivyo itawalazimisha serikali kurudi katika Misingi ya Utawala bora na kuleta uchocheo wa Katiba mpya.

Je, CHADEMA watafanikiwa kwa njia hii?
Sio CHADEMA ni wananchi wote. Kwa sasa kipigo ni kwa UVCCM na Bavicha. Sote tuko jiko moja. Msoto kwa kwenda mbele.
 
Susieni hospitalini, ukikuta doctor ni mwana CCM ahirisha kutibiwa urudi nyumbani na kama itawezekana msiende hata huko hospitalini maana mtachangamana na Wana CCM.

Hospitali ambazo haziendekezi uccm ni za kumwaga boss. Hizi zenye ujinga wa uccm ndio hata panadol hawana.
 
Ufinyu wa kufikiri. Wewe unadhani makusanyo yoote ya serikali yanaenda kulipa askari? Hujafikiria madawa hospitali, mishahara ya walimu na watumishi wengine n.k mambo luluki.

Lkn hiyo kampeni yenu inabidi mjipange, maana hilo mnaloliwaza, hampambani ni ccm bali mnapambana na wananchi. Maana ukisema unapambana na serikali, kwa lugha nyingine ni kuwa mnapambana na wananchi. Kama lengo lenu ni kuwa dhidi ya wananchi, ni kwamba mmeshindwa kabla ya kuanza vita.

Kama serikali inavyopambana na wananchi kwa kuweka tozo za kuwakomoa. Hii mbinu inaweza kuchukua muda kushika kasi, lakini ikitangazwa vyema lazima Italeta matokeo chanya.
 
Kina Lema walitushawishi tusitumie vodacom sie wajinga tukavunja lain hee kumbe wao hawakuvunjwa
 
Kuna mjadala unaendelea space pale twitter aisee kama haya maazimio ya kususia bidhaa na huduma yatafanikiwa hakika itakuwa hatari kwa uchumi.

Ushauri serikali wakutane na wapinzani haraka maana hata mishahara ya mapolisi inaweza kukosa huko mbeleni.

Ni ushauri tu mnaweza kuufanyia kazi au kuupuza ila kama hatua hizi zitafanikiwa hata kwa 25% makusanyo yataporomoka sana.
View attachment 1877729
Tatizo ukikataa kununua bia halafu serikali ikakuzidishia kodi ya PAYE utakuwa umeacha kunywa bia na umeanza kutwanga maji.

Hizo protests zinaweza kuwa na maana kama zinakuwa targeted against a specific company, or even industry.

Lakini ukiweka protest against the economy kwanza wewe mwenyewe utashindwa kuitimiza.

Kwa sababu yatatokea mambo ambayo hayaepukiki itabidi ukubali matokeo tu.
 
Kenya waliweza 100 percent...muulize Kenyatta...Hadi magari ya kampuni zake ya kusambaza bidhaa yaliharibiwa... Hand shake ilirudisha hali
 
Mama anashindwa kuelewa

Kufunga viongozi wa upinzani na kibaya zaidi kiongozi mkuu wa upinzani kwa makosa hewa kutamletea usumbufu mkubwa sana kuliko faida

Na hii aelewe,atumie medula yake kufanya maamuzi beneficial kwake,na maamuzi haya ni according to the law,nje ya law ni benefit za muda mfupi tu siku hiyo,the rest ni usumbufu mpaka basi

Mama asiweke akili zake likizo,azitumie kwa faida yake....

Nusu ya watanzania wanapenda upinzani,just imagine one person anachukiwa na watu milioni 30,Jiwe yalimshinda akafa,mama anaelekea kwenye upumbavu ule ule
Watu milioni 30 ni wapi?
 
Back
Top Bottom